Picha za CCTV za tukio la Lissu kushambuliwa mbona hazitolewi hadharani kama zile za tukio la kutekwa kwa MO au hizo picha hazikupatikana?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,012
144,371
Wakati wa sakata la MO, Polisi walitoa picha ya gari liliodaiwa kumteka MO japo picha husika ziliibua maswali mengi kuliko majibu.

Sasa kwakuwa tunaambiwa katika eneo aliloshambuliwa Lissu ni eneo ambalo camera za CCTV zilikuwepo, ni kwanini basi picha za tukio hazitolewi ili raia wema wasaidie kuwabaini wahusika ambao mpaka sasa hawajabainika?

Hakuna hata kapicha ka gari na namba zake au hata sura za wahusika?

Jamani tunaomba majibu.

Samahani lakini, msidhani nimetumwa na mabeberu bali nauliza tu kama raia mwema.
 
Sisi CCTV zetu ni kali kuliko za Marekani mkuu!
Hahahahahaaaaaaa,hatari sana!
Kuna mdau anaitwa YEHODAYA alisema hizo cctv zilikuwa za high quality!
Tulipohoji kuhusu angle ya camera,maana ilikuwa sambamba mno na gari,akasema cctv ni uamuzi wako,ukiamua unaweza ifunga ikuchukue makalio yako!

Sijawahi kuyasahau majibu haya mpaka leo!
 
Back
Top Bottom