PICHA YAKO mezani kwa mpenzi wako inakupumbaza.

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,532
1,124
mapenzi yana kauli mbiu ya uongo.
Unakuta jamaa ana wapenzi kama wanne na wote kawapiga picha,kinachotokea msichana m1 akitaka kuja jamaa anaondoa picha zote za m2,m3 na m4 na kuzificha,wewe ukiingia tu geto unakutana napicha yako mezani ama kwenye frame ukutani,kwa akili ndogo unajiaminisha kuwa hiyo picha ipo hapo muda wote kumbe ndo imetoka mafichoni kwa sababu ya ugeni wako,ukiondoka tu inarudi kifungoni.
Hata wadada nao ukute ana picha za jamaa zake tofauti tofauti,nae anazi-alternate kulingani na nani anakuja,kama hutokei ujue picha yako inasota rumande.
Alafu unaamini kupitia picha kuwa wapendwa kumbe wapi,
Wengine wakitaka kuja kwako wanaweka picha yako kwenye wall paper ama screen saver ya simu ili udanganyike,hapo ngoma droo wewe screen saver yeye picha kwenye frame.
 
Back
Top Bottom