UZUSHI Rais Samia achapishwa ukurasa wa mbele wa Gazeti la The Scotsman la Scotland

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Ukurasa wa mbele wa Gazeti la The Scotsman la Scotland umekuwa ukisambaa mitandaoni ukiwa na kichwa kinachosema "Rais Samia aongeza matumaini mapya kwa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Scotland na Tanzania,"

Gazeti hilo linalosomeka kuwa ni toleo la 1 Novemba 2021 la gazeti la kitaifa la Scotsman, linaonesha picha ya Samia Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania.

20221026_221149.jpg
Maandishi yaliyo chini ya kichwa cha habari yanasomeka: “Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan yuko Scotland na atakutana na balozi wa Uingereza katika kuendeleza majadiliano kuhusu maendeleo ya mataifa yote mawili kupitia sekta ya Teknolojia na Viwanda.”

Ukurasa huu umesambaa katika makundi ya Facebook nchini Tanzania, huku wakimwagia sifa Samia kwa "kuchapishwa" kwenye gazeti, wakisema inaonyesha "anaheshimiwa ulimwenguni kote kama kiongozi wa nchi.

The Scotsman cover.jpg

Ukurasa halisi wa The Scotsman
 
Tunachokijua
Katika ukurasa huo, kuna mambo kadhaa ambayo yanaweza kutia shaka usahihi wa taarifa hiyo. Pamoja na makosa mengine ya kisarufi, jina la Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson limeandikwa kama "Borris", jambo linalotia shaka kama kweli huo ni ukurasa halisi wa gazeti hilo kubwa.

Lakini pia, Google Reverse Search inaonesha kuwa picha hiyo ya Rais Samia imewekwa kutoka kwenye ukurasa wa mbele wa The Scotsman wa 3 Machi 2021 na si Novemba 1, 2021.

Kama inavyoonekana pale juu, ule ndiyo ukurasa halisi wa gazeti la The Scotsman ambalo lilitumika kuweka taarifa ya kupotosha kuhusu Rais wa Tanzania.

Hivyo, Ukurasa huo wa mbele wa The Scotsman unaoonekana na picha ya Rais Samia si halisi.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom