Picha ya Michelle Obama Yaleta Mtafaruku!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha ya Michelle Obama Yaleta Mtafaruku!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by GAMBLER, Jan 23, 2010.

 1. GAMBLER

  GAMBLER JF-Expert Member

  #1
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 22, 2009
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Picha Hii ya Michelle Obama Yamponza!
  [​IMG]
  Picha ya Michelle Obama iliyozua kashesheSaturday, January 23, 2010 3:17 AM
  Msanii wa Marekani aliyeiweka picha hii ya mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter imembidi aombe ulinzi toka FBI baada ya mamia ya watu kumtumia vitisho vya kumuua.Scott Baio msanii wa Marekani aliyetamba kwenye series za komedi za Happy Days na Charles in Charge ametumiwa vitisho kibao vya maisha yake baada ya kuweka picha mbaya ya mke wa rais wa Marekani, Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter.

  Baio aliiweka picha hii ya Michelle Obama kwenye ukurasa wake wa Twitter ikiwa na maneno "Wow, Obama anaamshwa namna hii kila siku asubuhi".

  Picha hii pamoja na maelezo yake ilichukuliwa na watumiaji wengine wa Twitter kama ubaguzi wa rangi.

  Haukupita muda mrefu Baio alianza kuandikiwa maoni kwenye ukurasa wake wa Twitter akiambiwa kuwa ni mbaguzi wa rangi na ameweka picha hiyo kumdhalilisha bi Michelle Obama.

  Baio alitumiwa vitisho vingi vya maisha yake kiasi cha kumfanya aripoti vitisho hivyo FBI.

  "Ni rahisi kuijua nyumba yako Baio na kukumaliza", Mtoa maoni mmoja aliandika huku mwingine akitishia kumdhuru Baio, Mkewe na mtoto wake.

  Hata hivyo Baio aliendelea kusisitiza kuwa alikuwa na nia ya kufanya masihara na sio kama ambavyo watu wengine walivyoichukulia picha na maandishi aliyoyaweka.

  Baio aliandika pia kwenye ukurasa wake baadhi ya vitisho vya maisha yake alivyotumiwa.
   
 2. t

  thekitoz Member

  #2
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hata mimi namsuport biao kwa hilo kwani masihara ni jamboi la kawaida katika maisha ya kila siku
   
 3. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #3
  Jan 23, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Mmh
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  Jan 23, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  masihara yasio na mipaka si mazuri
   
 5. D

  Darwin JF-Expert Member

  #5
  Jan 23, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 908
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Anayefurahi sasa ni Oprah

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Jan 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  Hizi ni inferiority complex (ugiligili) za watu weusi wala haziingii akilini. Nachukua fursa hii kuwaasa watu weusi popote walipo wajitahidi kufanya kazi kwa bidii na maarifa huku wakiweka malengo ili wasidharaulike tena (na.... of course waondokane na huu ugiligili. Watu weusi hatudharauliki kwa sababu ya rangi yetu bali ni matendo yetu. (Japo hii story haina uhusiano wowote na ubaguzi.... ni ugiligili tu... tukiendelea tutaacha...
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Jan 23, 2010
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  auwawe huyu mtu.mbona haweki picha ya mama yake kama anataka kudhihaki
   
Loading...