Picha ya Mbowe walipokutana na JK: Je unajifunza nini kwenye picha hii?

Nasikitika sana na upeo duni wa watu wanajiita "great thinkers", hivi kwani siasa ni uadui? Nani alikwambia au ulisoma wapi? Kimsingi Mbowe alihudhuria sherehe ile kwa nyadhifa mbili. 1. Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni na 2. Mwenyekiti wa chadema. Pia kumbuka mwaliko ulitolewa na mahakama sio ikulu. Kuna mihimili mitatu ya dola
1. Bunge - Chedema hawana tatizo nalo
2. Mahakama - Chadema hawana tatizo nayo
3. Serikali (Rais) - Chadema wanalalamikia taratibu zilizomuweka madarakani.

Jamani hebu kuweni na upeo japo kidogo tu tuoneshe tofauti yetu na watanzania wengine.
 
Kama sikosei hii ilikuwa ni mwaka 2005 baada ya uchaguzi uliomtangaza jk kuwa mshindi wa nafasi ya urais. Kwa ujumla, Chadema waliridhika na kuridhia matokeo na hapo kwenye picha inaonekana Kamanda Freeman Mbowe
akimpongeza jk bila kinyongo. Sasa kutokana na picha na maelezo haya, tunaweza kujifunza kwamba uchaguzi wa 2005 ulikuwa huru na wa haki na chadema waliridhika nao. Sasa basi, kama chadema ni chama kilekile na Mbowe, Dr. Slaa (PhD) na viongozi wengine ni walewale, kwa nini leo hii wasishikane mikono na jk? Ukweli ni kwamba uchaguzi wa mwaka huu haukuwa wa huru na wa haki.

Pia, picha hii inaonyesha umakini wa chadema katika kuendesha siasa za nchi hii na ni chama chenye msimamo thabiti wa kusimamia maamuzi yake. Hakina substandards katika kufanya mambo yake. Hongera viongozi wa chadema, wananchi tuna imani nanyi.

Tunashukuru kwa ufafanuzi huu makini, ni kweli kabisa kwa mtu mwenye busara huwezi kumununia mshindi halali kwenye uchaguzi. Inaonekana Kishongo alikuwa na lake la kuzua, mwisho wa siku kaishia patupu! Asante sana kamanda Gosbert kwa kuwasaidia ambao wangesumbuka na mambo ya Kishongo!
 
Angalia Mbowe anapetty JK
Hii ni ishara kwamba baina yao, Mbowe yuko huru zaidi ya JK, JK amejaa hofu, anaona aibu sana
kukutana na Mbowe, anasema (moyoni) kwanini huyu naye kaja apa, anaona kama waandaaji wamemsaliti kumkutanisha naye, akikumbuka tofauti zao za kisiasa, akikumbuka harakati zinazoendelea za madai ya katiba, issue nzima ya Arusha, Kampeni na matokeo ya urais kwenye uchaguzi uliopita na kwamba hawa jamaa kwa maoni yao ni kwamba nchi ina ombwe la uongozi, JK anachukia sana anapokumbuka kwamba yeye ndio Generali wa Majeshi ya Tanzania, lakini huyu Jamaa amevaa magwanda, na sasa amesababisha watu wengi zaidi kuyavaa, anasema kwanza huyu ndio alipendekeza SLAA kunivaa huyu, lakini sababu yuko kwenye public, anatoa tabasamu

viungo vya mwili wake vimeshindwa kufurahia kukutana na Kamanda
Mkono wa kushoto wa JK umekataa unafiki wa tabasamu lake, angalia uliko, unarudi nyuma zaidi, hauko active hata kidogo. JK ninayemfahamu mimi ni mtu mkakavu, lakini hapa ukimcheki ni kama amepinda hivi, WHY? anajiandaa kuondoka haraka aachana naye.

Na mbowe ni kama alifahamu ANAMPETTY,moyoni anasema "RELUX KILAZA"
 
Watu bana!!! Wasingesalimiana ungesikia Ohh fulani hajakomaa kisiasa... mara chuki binafsi....
Mnapishana kiitikadi kwa manufaa ya wananchi ikija kwenye kusalimiana, kusmile, kuchart ni kama kawaida.. :A S thumbs_down:
 
Angalia Mbowe anapetty JK
Hii ni ishara kwamba baina yao, Mbowe yuko huru zaidi ya JK, JK amejaa hofu, anaona aibu sana
kukutana na Mbowe, anasema (moyoni) kwanini huyu naye kaja apa, anaona kama waandaaji wamemsaliti kumkutanisha naye, akikumbuka tofauti zao za kisiasa, akikumbuka harakati zinazoendelea za madai ya katiba, issue nzima ya Arusha, Kampeni na matokeo ya urais kwenye uchaguzi uliopita na kwamba hawa jamaa kwa maoni yao ni kwamba nchi ina ombwe la uongozi, JK anachukia sana anapokumbuka kwamba yeye ndio Generali wa Majeshi ya Tanzania, lakini huyu Jamaa amevaa magwanda, na sasa amesababisha watu wengi zaidi kuyavaa, anasema kwanza huyu ndio alipendekeza SLAA kunivaa huyu, lakini sababu yuko kwenye public, anatoa tabasamu

viungo vya mwili wake vimeshindwa kufurahia kukutana na Kamanda
Mkono wa kushoto wa JK umekataa unafiki wa tabasamu lake, angalia uliko, unarudi nyuma zaidi, hauko active hata kidogo. JK ninayemfahamu mimi ni mtu mkakavu, lakini hapa ukimcheki ni kama amepinda hivi, WHY? anajiandaa kuondoka haraka aachana naye.

Na mbowe ni kama alifahamu ANAMPETTY,moyoni anasema "RELUX KILAZA"

Du!!!:twitch::laugh:
 
Hapo Mbowe anamwambia "Mzee lakini na wewe kwa kuchakachua ni noma!"
Mkwere akajibu " Heri lawama kuliko hasara, Ulitaka niaibike"
Wote wakacheka "teh teh teh teh"
Hiyo ndiyo SIASA!

Ha ha ha haaaa! This is funny.
 
Picha ni nzuri na wote wamependeza lakini.....Siasa sio vita na kusalimiana sio kusema ni muafaka wa katika itikadi za kisiasa.
 
Mie naona kama Mheshimiwa anaogopa/hofu hivi kwa jamaa mwenye Kombati. au nimeona vibaya jamani.
 
Tuache unafiki,angekuwa zitto hapo naamini hapa jf leo topic zingekuwa na mambo mengine kabisaaaaaa!
Mimi ni moja kati ya watu walio mpinga zitto kwa kujikomba kwa kikwete,RA,ZOKA and the like (fuatilia post zangul).....nalitegemea leo nikute topic ya kwanini watu hawa wamekutana,badala yake nakuta mnamponda mtoa mada!

Sasa naanza kuamini zitto aliposema anaonewa na "wakubwa" wa chama!
Ndo tusemeje kwamba na nyie humu mmelipwa kumshabikia mbowe au?
kwamba mbowe hakosolewi?

Ahhh,Kumbe zitto hata zitto pamoja na matatizo yake huwa tunamuonea kabisaaa hapa JF
 
Angalia Mbowe anapetty JK
Hii ni ishara kwamba baina yao, Mbowe yuko huru zaidi ya JK, JK amejaa hofu, anaona aibu sana
kukutana na Mbowe, anasema (moyoni) kwanini huyu naye kaja apa, anaona kama waandaaji wamemsaliti kumkutanisha naye, akikumbuka tofauti zao za kisiasa, akikumbuka harakati zinazoendelea za madai ya katiba, issue nzima ya Arusha, Kampeni na matokeo ya urais kwenye uchaguzi uliopita na kwamba hawa jamaa kwa maoni yao ni kwamba nchi ina ombwe la uongozi, JK anachukia sana anapokumbuka kwamba yeye ndio Generali wa Majeshi ya Tanzania, lakini huyu Jamaa amevaa magwanda, na sasa amesababisha watu wengi zaidi kuyavaa, anasema kwanza huyu ndio alipendekeza SLAA kunivaa huyu, lakini sababu yuko kwenye public, anatoa tabasamu

viungo vya mwili wake vimeshindwa kufurahia kukutana na Kamanda
Mkono wa kushoto wa JK umekataa unafiki wa tabasamu lake, angalia uliko, unarudi nyuma zaidi, hauko active hata kidogo. JK ninayemfahamu mimi ni mtu mkakavu, lakini hapa ukimcheki ni kama amepinda hivi, WHY? anajiandaa kuondoka haraka aachana naye.

Na mbowe ni kama alifahamu ANAMPETTY,moyoni anasema "RELUX KILAZA"

Tumtoe mbowe kwenye picha na tuasume ni zitto,comment yako ingekuwaje?
 
Ninajifunza kuwa kwenye siasa watu wanapingana bila kupigana. Vita iko kwenye hoja na kwa kushawishi wapiga kura kwa sera.
 
Ni picha inayobeba matumaini badala ya kukatisha tamaa.

Kama ningewashauri CHADEMA, basi, ningewaambia, kuwa , kwa kiongozi, vazi pia hutuma ujumbe kwa unaowaongoza. Magwanda yale ya CHADEMA yamekaa kijeshi zaidi. Labda yalitosha kuyatumia katika ’ mapambano’ ya kampeni za uchaguzi, lakini si sasa. Uchaguzi umeshapita.

Mjengwa, moja wa viongozi wa chadema (kama sikosei ni Zitto) aliwahi sema kuwa magwanda yanaonyesha ishara ya mapambano......hapo sikubaliani na wewe unapowashauri CHADEMA wavue magwanda......wavue magwanda kwani mapambano yameisha? au mapambano ni wakati wa uchaguzi tu kama ulisema kwenye post yako..........bado tuko kwenye mapambano na CHADEMA kikiwa ndiyo kambi ya upinzani wanajukumu la kuwa mstari wa mbele katika mapambano.........bado elimu yetu ni duni, usafiri ni shida, makazi duni, ajira na ujira duni....yote haya yanampata mwananchi wa kawaida wakati viongozi waserikali wanajirundikia mali na kunenepeana kwa rushwa za walalahoi....mapambano bado yanaendelea na kama magwanda ni ishara ya kuonyesha mko ktk mapambano basi ni vema yasivuliwe hata ikibidi wakati wa kulala maana mapambano bado.
 
Amna cha kujifunza awa jamaa ni washikaji wa siku nyingi wanajuana, wemecheza pamoja madisco ya zamani ya Dar es salaam RUNGWE na MBOWE

50335004.jpg

Yasser Arafat wa PLO na Netanyahu wa Israel. maadui wakubwa lakini kushikana mikono hakukuwa na maana ya kuacha mapambano ya kila mmoja kummaliza mwingine

_39258241_arafatrabin_ap_238.jpg

Hapa ni Yitzak Rabin na Arafat. makubaliano mazuri lakini kilichoendelea kinafahamika.

nataka kusema kwamba kupena mikono inaweza kuwa ni alama ya kutambuana kila mmoja umuhimu wa mwingine, na inaweza kuwa ni mwanzo wa kutatua tatizo kwa kuangalia maslahi ya taifa. sio jambo la aibu na kuogopwa kama wanavyodhani wengi. Nadhani historia hapa itaamua kama CHADEMA wanakusudia nini. so far wameondoka katika hard line yao na ku-soften up a bit. hiyo inaweza kuwa pia kwa sababu wamesha-score mabao kadhaa katika ile Parliamentary walkout yao. tukubaliane kwamba vuguvugu la katiba la hivi sasa lilichochewa pia na action hiyo ya CHADEMA. sasa wanasonga mbele kuangalia avenues mpya za mapambano. makes sense.
 
Kumbukeni 'Rais' wangu Dr. Slaa alisema 'Chadema' haina ugomvi na Kikwete kama Kikwete ila ina Ugomvi na 'Mfumo' uliomweka Kikwete Madarakani. This means Chadema inamtambua Kikwete Kama Mtanzania na siyo kama 'Rais' .Kwa Kuwa mfumo wetu wa Kumchagua 'Rais' Ulichakachuliwa kwa Uwazi.
Kwa Mantiki hii Mbowe Kumsalimia Kikwete hata Kama ni kesho na Keshokutwa haina Tatizo Lolote! Wale ambao wanahoji Mbowe Kumsalimia Kikwete Hawana Akili Nzuri.
Utaniuliza kwa Nini Wabunge walitoka Bungeni Kikwete alipokuwa anahutubia kama wanamtambua kama Mtanzania...Nami Nitakujibu kuwa Bungeni Kikwete alitambulishwa kama 'Rais' na siyo 'Kikwete' na Chadema kwa kuwa hawautambui Mfumo uliomweka 'Rais' Madarakani ndiyo maana wasingeweza kumsikiliza 'Rais' Huyo wa kuchakachua.
So Nje ya Ukumbi wa siasa Kikwete kama 'Kikwete' kusalimiana na Mbowe au Slaa au Wanachadema Wengine inadhihirisha Ukomavu wa Siasa na Uvumilivu Mkubwa walionao Viongozi wa CHADEMA
 
Kama ningewashauri CHADEMA, basi, ningewaambia, kuwa , kwa kiongozi, vazi pia hutuma ujumbe kwa unaowaongoza. Magwanda yale ya CHADEMA yamekaa kijeshi zaidi. Labda yalitosha kuyatumia katika ’ mapambano’ ya kampeni za uchaguzi, lakini si sasa. Uchaguzi umeshapita.

NA YALE YA KIJANI YA CCM YAPELEKWE WAPI?
Japo Umejitahidi kuweka na references.......bado Hujakomaa kiakili!
 
Mtu Huru aeleza nini kilimsibu akatoa mikono miwili kwa Kikwete, mtu ambaye Chadema inamshutumu kwa kuiba kura za urais kwenye uchaguzi wa 2010...


Mbowe: Why I shook hands with Kikwete

The Citizen Reporter
Dar es Salaam

Chadema national chairman Freeman Mbowe said yesterday that he shook hands with President Jakaya Kikwete on Wednesday because he has no personal differences with the Head of State.“I have no personal grudge against President Kikwete…people should understand that he is the lawful President of our country,” Mr Mbowe told The Citizen by telephone.

In an unexpected gesture that received wide media coverage, with a front-page picture in most newspapers, Mr Mbowe shook hands in an apparently warm encounter with the President, who was the chief guest at an official function to mark Law Day at the High Court in Dar es Salaam.

Mr Mbowe, who is also the Hai MP and Leader of the Official Opposition in Parliament, said Chadema recognised Mr Kikwete as the President of Tanzania in line with the existing laws, although the opposition party had queried the manner of his election to the highest office in the land.

“We are categorical that Mr Kikwete is Tanzania’s lawful President…it is the legitimacy of the mandate that we have problems with…if Mr Kikwete was not the lawful President of this country, we would have demanded that he resign,” he said.

Mr Mbowe was commenting on whether the handshake was a sign that Chadema had finally relaxed its hardline position, and was ready to work with President Kikwete’s government.

Chadema has boycotted a number of key national events since the General Election of October 31, including the announcement of the official results and Mr Kikwete’s subsequent swearing-in.

The party also boycotted the swearing-in of Prime Minister Mizengo Pinda and the Cabinet.

Chadema sparked controversy, when its MPs walked out of the National Assembly in Dodoma, as President Kikwete began to deliver his inaugural speech to the Tenth Parliament.

The opposition party maintained that the presidential election was rigged in favour of the CCM candidate, handing him his second and final five-year term.

Yesterday, Mr Mbowe said his attendance at the Law Day function was part of fulfilling his obligations as the Leader of the Official Opposition in Parliament.

“We all know that the Judiciary is an important link between us and the government…they invited us to the ceremony, and I had no reason to refuse to attend,” he said.

The opposition chief said he met and chatted with many other people at the function. “I’m a mature and sober politician, and I cannot snub the President or anybody else on political grounds.
“Politics is not about enmity…what we did during the President’s speech in Parliament was meant to highlight our concerns and get our message across, and we have succeeded in that,” Mr Mbowe said.

President Kikwete’s decision to appoint a constitutional review commission, Mr Mbowe added, was the result of the “relentless” pressure that Chadema had put on the Head of State.

“I doubt whether President Kikwete would have taken steps towards a new constitution were it not for our insistence because the matter is not in CCM’s manifesto.”

Mr Mbowe said Chadema was happy that some of their demands were being addressed, although the party was not entirely satisfied with the way the government wanted to conduct the constitutional review process.

In response to the news of the politicians’ handshake, several commentators lauded Mr Mbowe for the gesture and urged the party’s secretary-general, Dr Willibrod Slaa, to follow suit. Dr Slaa was Chadema’s presidential candidate in last year’s elections. He came second to President Kikwete.

For his part, Dr Slaa said Chadema had no problem with the Judiciary, adding that what they were questioning was Mr Kikwete’s legitimacy as the President. “We have not changed our position,” he said.

The head of the Department of Political Science and Public Administration at the University of Dar es Salaam (UDSM), Dr Benson Bana, said Chadema had no concrete grounds to shun President Kikwete’s government, adding that the opposition party “is just playing politics”.

“Their strategy is to be heard and remain relevant in the political arena…they are just politicking.
“Chadema keep on insisting that the presidential election was rigged, but they have not provided any evidence to support their claim,” Dr Bana said.

He added that it was easy for one to conclude from Mr Mbowe’s body language in the pictures showing him shaking hands with President Kikwete that the opposition politician was apologetic.

Mr Maggid Mjengwa, a veteran political and social commentator based in Iringa, said the handshake between the two should mark the start of the easing of political tensions heightened by results of the General Election.

“Life has to go on after elections…we should forget what happened during elections and continue with nation-building.”
He said cooperation between Chadema and the government would be in the best interests of Tanzanians and the country.

Source: Mbowe: Why I shook hands with Kikwete
 
Send to a friend Wednesday, 02 February 2011 21:08

Fidelis Butahe na James Magai

MWENYEKITI wa Chadema, Freeman Mbowe jana alikutana uso kwa uso na Rais Jakaya Kikwete ikiwa ni mara ya kwanza tangu chama hicho kilipotangaza kutotambua ushindi wa Kikwete uliompa fursa ya kuwa rais kwa kipindi kingine cha miaka mitano kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, mwaka jana.Tukio hilo la aina yake kutokea tangu kuanza kwa mwaka huu, liliwakutanisha Mbowe na Rais Kikwete katika maadhimisho ya Siku ya Sheria yaliyofanyika jijini Dar es Salaam ambapo walisalimiana kwa kupeana mikono.

Mbowe na Kikwete walikutana uso kwa uso ikiwa ni siku 85 tangu Mbowe alipowaongoza wabunge wa chama chake kususia hotuba yake ya uzinduzi wa Bunge la 10, Novemba 18 mwaka 2010 kutokana na msimamo wa chama chake kutotambua matokeo ya urais.

Mwaka jana, Mbowe alitangaza chama chake kutotambua matokeo ya rais huku akitoa madai mbalimbali kuhusu taratibu zilizotumika kumwingiza kiongozi huyo madarakani.

Madai ya Chadema ambacho mgombea wake wa urais Dk Willibrod Slaa alishika nafasi ya pili ni pamoja na kutaka kuundwa kwa tume huru ya uchaguzi, kuandikwa kwa katiba mpya na kuundwa kwa tume huru ya kuchunguza matokeo ya uchaguzi wa rais yaliyomweka madarakani Rais Kikwete kwa mara ya pili baada ya kupata kura 5,276,827 ukiwa ni ushindi wa asilimia 61.17.

Katika uchaguzi huo, Dk Slaa alipata kura 2,271,941 sawa na asilimia 26.34 huku Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF akipata kura 695,667 sawa na asilimia 8.06.

Mbali na kutohudhuria hafala ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi huo, wabunge wa Chadema pia walisusia sherehe za kumwapisha Kikwete zilizofanyika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam na pia zile za kuapishwa kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda zilizofanyika katika viwanja vya Ikulu Ndogo ya Chamwino, Dodoma.

Mbali na Sherehe hizo, pia viongozi wa Chadema hawakuonekana katika maadhimisho ya miaka 49 ya Uhuru wa Tanzania Bara yaliyofanyika katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Desemba 9, 2010.

Katika maadhimisho ya jana yaliyofanyika nje ya Mahakama Kuu Dar es Salaam, Mbowe alikuwa miongoni mwa wageni waliohudhuria katika maadhimisho hayo, akiwa ni kiongozi pekee wa chama cha upinzani huku Rais Kikwete akiwa mgeni rasmi.

Tukio hilo lilivuta hisia kwa washiriki wa maadhimisho hayo ya siku ya Sheria nchini ambapo Mbowe aliwasili katika maadhimisho hayo akiwa peke yake huku akiwa amevaa mavazi maalumu ya chama hicho maarufu kwa jina la kombati pamoja na miwani myeusi.

Baada ya kuwasili alikwenda kukaa katika viti vya mbele karibu na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa.

Katika tukio la kupiga picha za pamoja ndipo Mbowe alikutana uso kwa uso na Rais Kikwete ambapo walisalimiana kwa kupeana mikono na kupiga picha pamoja huku wote wakiwa na tabasamu pana.

Alipotafutwa na gazeti hili ili kuzungumzia tukio hilo, saa kadhaa baada ya kumalizika kwa sherehe hizo, Mbowe alisema alikwenda katika sherehe hizo kwa kuwa zilikuwa ni za mahakama na kwamba hata kungekuwa na tofauti gani kusingemzuia yeye kusalimiana na Kikwete.

"Sherehe zile si zangu wala Rais Kikwete hivyo siwezi kuwa na chuki na mahakama, ni 'Birthday' ya Mahakama yenyewe ni mhimili wa dola," alisema Mbowe.

Mbowe alisema kuwa katika maadhimisho hayo alialikwa kama mwenyekiti wa Chadema na kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.

“Hatuwezi kuwa na chuki na mahakama, pale mihimili yote mitatu ya nchi ilikuwepo, ile haikuwa 'Birthday' yangu wala ya Rais Kikwete,” alisema Mbowe.


Mbowe alisema kuwa madai waliyotoa baada ya Uchaguzi Mkuu mwaka jana haikuwa na maana kwamba hawaitambui Serikali wala kutaka Rais Kikwete ang’oke madarakani.

Alisema kuwa mambo mawili kati ya matatu yaliyokuwemo katika dai lao yameshaanza kupatiwa ufumbuzi kwa namba moja au nyingine ambayo ni katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Rais azungumzia imani ya wananchi kwake
Akizungumza katika maadhimisho hayo, Rais Kikwete alisema kuwa baadhi ya wananchi wamekosa imani naye kutokana na msimamo wake wa kukataa kuingilia uhuru wa Mahakama wanapomtaka atengue maamuzi mbalimbali ya korti.

Kikwete alikuwa akizungumzia uwelewa wa wananchi juu ya sheria mbalimbali na nafasi ya Mahakama ambapo alisema kuwa wananchi hawana budi kufahamu jinsi Mahakama inavyofanya kazi.

Rais alitoa wito kwa Mahakama kushirikiana na wadau mbalimbali vikiwamo vyombo vya habari katika kutoa elimu kuhusu sheria.

Naye Jaji Mkuu Mohamed Chande Othman alisema kuwa ingawa ni msingi wa sheria kuwa kila mtu anatarajiwa kujua sheria, lakini kwa bahati mbaya uwelewa wa wananchi kuhusu Mahakama na sheria ni mdogo na kwamba kutokujua sheria sio kinga.



source:Mwananchi
 
Mbowe na JK tofauti yao ni msimamo wa kisiasa lakini wote ni wa TZ na tofauti zao za kisiasa haziwezi kuwafanya wawe maadui!!! hivyo anaefikiri kuwa mitizamo tofauti ya kisiasa ni uadui, basi hajui nini siasa na anahitaji kozi maalum ya kuhusu Siasa!!!
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom