Picha ya Maradona huenda ikachapishwa kwenye pesa ya Argentina

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Seneta Norma Durango aliwasilisha muswada bungeni ili kumfanya kiungo huyo, ambaye alifariki wiki mbili zilizopita akiwa na umri wa miaka 60, kuwa kwenye noti ya 1,000 sawa na dola ($ 12, £ 9), noti ya juu zaidi.

Noti hiyo itakuwa na uso wa Maradona upande mmoja na picha ya moja ya mabao yake maarufu, hususan dhidi ya England katika robo fainali ya 1986, kwa upande mwingine, alisema.

Seneta huyo pia alipendekeza kuweka picha yake kwenye mihuri ya kumbukumbu.
"Wazo sio tu kumtambua mtu huyu muhimu zaidi, lakini pia kufikiria suala la uchumi," Bi Durango alisema.

"Tunahisi watalii wanapokuja hapa watataka kumchukua 'Maradona' na kwenda naye.
" Alisema seneta huyoPicha ya marehemu nyota wa Argentina Diego Maradona, aliyeiongoza nchi yake kutwaa Kombe la Dunia mwaka 1986, inaweza kuwa ndio uso wa noti yenye thamani kubwa zaidi nchini Argentina hivi karibuni.

BBC
 
Nachelea Hilo wazo

Nilikuwa nafuatilia clip za maradona YouTube aisee jamaa alikuwa Ni famous mkubwa sana ameipaisha Sana Argentina katika nyanja za kimataifa. Awali kabla ya kifo chake nilikuwa sijawahi kumfuatilia kiasi hiki nakumjua kiundani

Jamaa alikuwa ni maarufu saana licha ya hivyo he was gifted haswaa. Nilikuwa na mkubali Sana Messi na Ronaldinho lakini naomba nikiri kwamba hawa watu watu hawamfikii maradona hata kidogo Cause style zote za uchezaji walizonazo ni copy toka kwa Maradona kuanzia Kasi, dribling, controling, upigaji faulo . Na mengine mengi

Itoshe tu kusema kwamba Maradona alikuwa anaishi mbele ya muda cuz vile Ambavyo vinafanywa na wachezaji wa sasa ambao ndio tunawaona wanajua Sana kucheza mpira yeye ameshavifanya miaka ya 80s
 
Hawa ndio wachezaji wangu bora kuwahi kutokea, Maradona amenifanya nipende mpira...baada ya kustaafu kwake, ikapita long time kutokua na mburudishaji mwingine, mpaka alipoingia mchawi wa soka king Messi burudani likarejea




Boca




Boca





Amazing skills in training 😀 wakina gaucho, zidane, okocha n.k wamecopy kwa huyu mwamba lakini bado walifeli, yaani hata robo yake tu hawakumfikia 😂

 
Back
Top Bottom