Picha ya leo - Waliopitia JKT enzi hizo itawakumbusha makubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha ya leo - Waliopitia JKT enzi hizo itawakumbusha makubwa

Discussion in 'Jamii Photos' started by Candid Scope, Jul 4, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 2. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #2
  Jul 4, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  mateso gani haya, ili iweje!!.
   
 3. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #3
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Watu legelege watasema ni mateso, kumbuka huwezi kuwa jasiri bila kupitia hatua mbalimbali za majaribu na kujenga ukakamavu. Kama umepitia jeshi utaelewa la sivyo huwezi kupambana na adui kama hujawa na ukakamavu.

  Maisha yahitaji ukakamavu kama huo unaojenga mtu kiakili na kimwili kuhimili misukosuko ya maisha hadi kieleweke.
   
 4. paty

  paty JF-Expert Member

  #4
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,257
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  kwa mshahara wa shiling ngapi ????labda wawe wananilipa milioni hamsini kwa mwezi , hapa nashika kalamu nakula zaidi yao , anyway ndo matatizo ya kufanya kazi ambayo anyfool can do, big wana JKT hu hu huuuuu
   
 5. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #5
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kama utakumbuka utaratibu huu ulikuwepo wa kuwaandaa vijana baada ya kuhitimu kidato cha sita kupitia jeshi kwa miezi sita au mwaka mmoja. Hii ilikuwa kuwaandaa kwa maisha kuwa wakakamavu na watendaji wazuri.

  Angalia vijana siku hizi walivyo legelege na hakuna ukakamavu, hawajitumi, inatia huruma sana.

  Vijana wa leo wanapenda kazi laini ambazo hata hazilipi kama za kuuza vocha za simu, kwa njia hii tutafika?
   
 6. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #6
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Hilo zoezi mbona cha mtoto, karibu Kinyerezi ushuhudie mazoezi yangu ya Kung-FU yaliyonipa cheo cha SENSEI!
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  Jul 4, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Hili ni zoezi la kuvunja shindo, ukweli ni ukweli tu, kiwiliwili chote hapo kinategemezwa na shingo tu, huu ukuruta kazi kweli kweli,
   
 8. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #8
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Mkuu Candid Scope, 99% mliopita JKT, ukakamavu imebaki historia tu, wengi wenu ni ma boss vitambi meneja. Kazi yenu ni bia nyama choma na ktmoto. Ole wenu vita itokee mtawekwa front. Tobah!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!:israel:
   
 9. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #9
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Namkumbuka Babu wa Vibwende. OP Program ya Chama 832 KJ mpooooo? Enzi za Col.Meena, Dr Omar (Maj.), Maj Mwakitosi, Sgt. Manzani, Cpl Nyundo, Sgt Basekana, Sgt Sahani, Maj Lugaimukamu, RSM Kitomari na wengineo. Tukumbushane
   
 10. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #10
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Duh,Mkuu umenikumbusha mbali sana. Unajua mm niliingia baada ya Meena tu wakati wa Kanali Urio. Na hyo list yote ilikuwepo. Hapo anaongezeka afande Kibuyu afu kule Eagle na F-coy walikuwepo afande Sanga,Lucas na Salehe. Memories are made of this!
   
 11. Tram Almasi

  Tram Almasi JF-Expert Member

  #11
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 755
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwa waliopitia Ruvu watakumbuka kulikuwa na stori eti kuna mdada ktk anaitwa 'Malela' ktk harakati za kutoroka alipotea na hakupatikana tena. Cjui ilikuwa kweli au ilikuwa vitisho tusitoroke cjui. Mpaka kuna wimbo wake ''Malela, Malela Malela. Malela namtafuta Malela.....Mkuu umenipa flashbacks heavy!
   
 12. m

  mamajack JF-Expert Member

  #12
  Jul 4, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ukakamavu???mbona wengi wao wakipewa nafasi wanakuwa wezi????
   
 13. paty

  paty JF-Expert Member

  #13
  Jul 4, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 1,257
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  yuuuuuuuuuuu, this is fake, mafisadi wote wa leo ni product ya JKT, waakina Mr.dhaifu , waakina komba ndo product za huko huko Candid Scope kimsingi sioni chochote cha ziada, zaidi ili corrupt mind za hawa wanaotuibia sasa ivi na kuwapa mitazamo ya kifisadi , hawa mafisadi wote walipita huko , saa wana uzalendo gani ?? mbona wanachumia tumbo ??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. andishile

  andishile JF-Expert Member

  #14
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 1,430
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  umenikumbusha mbaliii kanali urio akiwa CO,sisi ndio wale wa mwisho wa mwaka mmoja,afande nyundo alihamia B-coy!wengine kina samtata,matron hadija n.k nakumbuka f coy mlikuwa mnajiita makondeko! uongo mbaya jamani jeshi lilisaidia sana kuondoa matabaka na kutufanya kuwa wakakamavu! na kubwa kabisa wote mnakuwa sawa,hakuna cha mtoto wa mkubwa,wala nini,wote full ujeshi!hakukuwa na upendeleo!safi kabisa.
   
 15. Kibwebwe

  Kibwebwe JF-Expert Member

  #15
  Jul 4, 2012
  Joined: Jun 26, 2012
  Messages: 797
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mambo ya kupiga chenja
   
 16. E

  ELIAS SABLAKI Member

  #16
  Jul 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hakika umekumbusha jambo la msing sana, kwani sasa nakumbuka Makutupora na Edmund Mjengwa CO. MPs waliniamsha saa nane usiku na kuanza kunipigisha kuchanuwa kama ndege huku nakimbizwa Quorter Guard na kusulibiwa hadi asubuhi kwa kosa dogo tu. Lakini pia zoezi la kupali mraba wa mizabibu ukifika mwaisho ndo unakuta nyuka na ukianza kurudi na mraba wa pili unakuta ugali. Eh bwana nisikumbuke kwa ng'ombe na mbuzi ni kula nyama kwa kwenda mbele. Hii iliniweka fiti ele mbaya. Wote tuliopitia huko ni shupavu ile mbaya. Kazi mtindo mmoja.
  Naomba serikali irudishe haraka sana maana wanetu wanakwisha kwa kuwa laini.
   
 17. grafani11

  grafani11 JF-Expert Member

  #17
  Jul 4, 2012
  Joined: May 24, 2011
  Messages: 15,534
  Likes Received: 342
  Trophy Points: 180
  Unafikiri ukakamavu unakuja kirahisi rahisi tu, ukitoka hapo kichwa kinakuwa kigumu kama cha kondoo.

  Ukimtwisha mtu ndoo atadhani kagongwa na fuso.
   
 18. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #18
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 500
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mkuu una kumbukumbu sana, na mimi nilikuwa program ya chama Makutupora CO akiwa Col. Matingas, na OC wetu alikuwa Capt. Mahwaga, na kuna OC wa E-Coy kama nakumbuka alikuwa anaitwa Mwakilema, sifa yake kubwa ilikuwa kila operation lazima awe na mwanamke. Mgulani alikuwa Fabian Massawe kama mkuu wa shule na Kipingu msaidizi wake. Kweli JKT ilikuwa ni sehemu vijana wa kitanzania bila kujali wanakotoka kuishi pamoja bila madaraja. Tulipokuwa Makutupora, tulikuwa na mdogo wa Salim Ahmed Salim tena kaka yake akiwa Waziri wa ulinzi, yeye hakuwa na tofauti na sisi akina yakhe wengine. JKT ilijenga mshikamano baina ya vijana wa makabila/status mbalimbali.
   
 19. M

  Mzawa Halisi JF-Expert Member

  #19
  Jul 4, 2012
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 500
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Paty, JKT kwa vijana wengi ilikuwa ni lazima kwenda kwa mujibu wa sheria. Isipokuwa kwa wachache tuliokuwa tunawaita Volunteers, wengi wetu ilikuwa compulsory, na yeyote aliyemaliza kidato cha sita au kozi ya miaka miwili na kuendelea baada ya kumaliza kidato cha nne (walimu na waganga) ilikuwa ni lazima kwenda JKT kabla ya kupata ajira au kuendelea na masomo ili kuweza kupata ajira au kuendelea na masomo.
   
 20. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #20
  Jul 4, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sio kwa style hiyo. Kwenye hilo akili zaidi inahitajika, sio mambo kama hayo kujongezea madhara kwenye mwili wako kwa sababu gani. zipo njia salama za kujifunza hivyo na zaidi ni akili jinsi ya kupambana na adui na maisha.
   
Loading...