Picha ya kwanza ya Jupiter yatolewa

Cendy

JF-Expert Member
Mar 28, 2015
1,248
2,306
Chombo cha anga za juu cha shirika la Marekani la NASA kilichopewa jina Juno kimetuma picha za kwanza za sayari ya Jupiter.

Moja ya hizo, iliyotolewa na NASA Jumanne inaonesha sayari hiyo ikiwa imezungukwa na miezi mitatu kati ya miezi yake minne mikubwa.

Miezi inayoonekana ni Lo, Europa na Ganymede. Mwezi huo mwingine uitwao Callisto hauonekani.

Picha hiyo ilipigwa Jumamosi sayari Juno ilipokuwa inazunguka sayari hiyo ikiwa umbali wa maili milioni tatu.

Setilaiti ya Juno yafika Jupiter
Hata katika umbali huo, Shimo Jekundu, lililosababishwa na dhoruba kali kwenye sayari hiyo karne nyingi zilizopita, linaonekana.

Juno iliingia katika mzingo wa Jupiter wiki iliyopita na kuanza kuizunguka sayari hiyo ambalo pia hufahamika kama Zohali au Zozali.

Safari yake kutoka duniani hadi ilichukua miaka mitano.

Juno itachunguza na kupeleleza sayari hiyo kwa miezi 20, lengo kuu likiwa kusaidia wanasayansi kubaini asili ya sayari hiyo ambayo wanaamini inaweza kuwasaidia kuelewa zaidi asili ya mfumo wa jua.

Chombo hicho cha juu kilipokuwa kinaikaribia Jupiter, kamera zake na mitambo mingine muhimu vilizimwa kuzuia visiharibiwe na miali nururishi. Baadaye, vilifunguliwa.

Wanasayansi wanatarajia picha za karibu zaidi za Jupiter zitapokelewa mwezi ujao.
Jupiter ina ukubwa mara 11 kuzidi Dunia na uzito wake ni mara 300 zaidi.

Sayari hiyo hutumia miaka 12 ya dunia kulizunguka jua; siku moja huko hudumu saa 10.

Muundo wake ni kama wa nyota , sana haidrojeni na helium.

Nasa inapanga kuitumia Juno hadi Februari 2018.

a7196a0e2dca0da6b75df4599c82e06e.jpg
 
I think kina be controlled kutoka dunia

Labda watalamu waje watwambie
 
Hicho chombo Juno kina wana anga ndani yake au ni drone?
Hakuna wanaanga kunakuwa na bands za electromagnetic spectrum ambapo mara nyingi kwa vyombo vya anga la mbali huwa wanatumia x band kwa ajili ya mawasiliano, kama wewe ni mfutaliaji wa maswala ya ungo na digital tv nadhani ushawahi sikia vitu kama c-band, ku-band hizi ni mode ambazo satellite hutumia kutuma data ili zipokelewe na LNB ya kwenye ungo ili kunasa beams zilizotumwa na satellite husika sasa hiyo x band ni moja ya njia kusafirisha data, hiyo spacecraft inakuwa na antena zenye nguvu pamoja na sensors zingine hivyo inakuwa raisi kwa kile kituo kinachokontro hiyo spacecraft kujua nini kinaendelea.
Mfano hiyo juno inaundwa na vyombo vifuatavyo
Microwaves radiometer ambayo hii inahusisha antena 6, pia hii juno ina spacecraft computer ambayo yenyewe kazi ni kuprocess command ambazo zinatumwa kutoka hapa duniani, ili kuilewa zaidi unaweza tembelea hii link,
Juno (spacecraft) - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Wewe jamaa uko njema na ndio maana ulikuwa unani chalenji kwenye ule uzi wako wa Unajuaje kama dunia inalizunguka jua? Hivi ulishapata jibu au bado ....... kama vipi ingia na huku ukatuelimishe pia kuhusu haya makitu kuna bonge la mijadala hautojuta kuingia.Ifahamu sayari ya Saturn kiundani zaidi
Ifahamu sayari ya Mars...
Ifahamu sayari ya Jupiter
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom