Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,671
- 149,843
Hiyo ni picha ya mh.Mbowe akiongea na Waandishi wa habari baada ya kutoka nje ya ukumbi wa Bunge yeye na wabunge wenzake wa upinzani.
Picha hii ukistadi vizuri utapata message fulani ikiwa ni matokeoa ya uamuzi wa shughuli za Bunge kutokuonyeshwa live.
Binafsi, picha inanipa message zifuatazo:
1.Kwa wingi hizo camera, ni wazi waandishi wa habari wamejikuta hawana kazi baada ya kuzuiwa kufanya coverage ya shughuli za Bunge na hilo tukio likawa limewapa angalau cha kuripoti kwa umma.
2.Ni wazi waandishi wa habari watakuwa wamechukizwa na uamuzi huu na hivyo wameamua ku-sympathize na wapinzani na ndio maana Mbowe amezongwa kwa kiasi hicho na waandishi wa habari na camera zao.
3.Picha hii inanipa ujumbe kwamba Mbowe na upinzani kwa ujumla unakubalika sana na hata waandishi wanatambua hilo.
4.Picha hii ni kiashiria tosha kuwa taarifa za wapinzani na shughuli za wapinzani ndani ya Bunge ndio zitakazopewa umuhimu mkubwa kuliko habari za serikali Bungeni kama utaratibu huu wa kutorusha live shughuli za vikao vya Bunge utaendelea.
5.Picha hii ni ujumbe tosha kuwa uamuzi wa kutorusha moja kwa moja kwa shughuli za vikao vya Bunge, utaipa faida UKAWA kisiasa na kuigharimu CCM na serikali yake.
6.Mwisho,ni wazi habari za upinzani Bungeni zinauza kuliko habari za serikali Bungeni.
Je,we mwanzangu unagundua nini kutokana na picha hii?
Picha hii ni kutoka katika gazeti la Mtanzania online la siku ya leo.