PICHA: Wenje atikisa Geita, amvalisha Gwanda mwenyekiti wa zamani wa CCM wilaya

Magwangala

JF-Expert Member
Oct 4, 2011
2,381
1,493
Mjumbe wa kamati kuu ya CDM amewavutia maelfu ya watu katika mji wa Geita kwa hotuba yake hadi kupelekea watu wengi kumkabidhi kadi za CCM akiwemo kada maarufu na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita ndg Sunzu Ntinonu.Akihutubia leo jioni katika uwanja wa Magereza, aliwaambia waalimu,manesi na maaskari polisi kuwa iwapo CDM itaingia madarakani watawezeshwa kununua bidhaa katika maduka maalum ambayo yana msamaha wa kodi kama yaliyopo katika kambi za JWTZ.
attachment.php

attachment.php



attachment.php
attachment.php
 

Attachments

  • w.JPG
    w.JPG
    31.3 KB · Views: 2,806
  • umma.JPG
    umma.JPG
    46.9 KB · Views: 2,791
  • Ntinonu.JPG
    Ntinonu.JPG
    31.4 KB · Views: 2,751
  • W&Nt.JPG
    W&Nt.JPG
    19.1 KB · Views: 2,723
Askari Polisi tayari wanayo maduka hayo kama ya JWTZ ya Duty free shops!, jihadharini na mchezo wa kuchukua Skrepa za kisiasa toka CCM!
 
Chadema mjitahidi sana majimbo ya mwanza ambayo mnayo kama Ilemela na Jimbo Nyamagana. Kuna kila dalili hayo majimbo yatarudi CCM. Wabunge wake wanatakiwa waende ngazi ya chini kabisa kuwaelimisha umma na kufanya mrejesho wa majukumu yao ya kibunge. Pia wanataiwa wasuluhishe mifarakano midogomidogo ndani ya chama hapo Mwanza ili wawe kitu kimoja kuelekea 2015. Huu ni ushauri tu. Maana naona tunaweza kupoteza hayo majimbo.
 
Askari Polisi tayari wanayo maduka hayo kama ya JWTZ ya Duty free shops!, jihadharini na mchezo wa kuchukua Skrepa za kisiasa toka CCM!
Na walimu je? Km Askari polisi wananunua bidhaa duty free kwa nini walimu wasiwe nayo? Wote si watumishi wa umma?
 
Majimbo yote ya mwanza yanarudi ccm 2015 wanamwanza wamechoka na migogoro yenu wana cdm
 
Majimbo yote ya mwanza yanarudi ccm 2015 wanamwanza wamechoka na migogoro yenu wana cdm

Mnarudi ccm kwa sababu ccm imebadilika sasa imekuwa nzuri au ndo kumangamanga na kutojua tunakoelekea? Nyie rudini mtakuja kushutuka mmebaki peke yenu na magamba yenu! Nani bado anafikiri kurudia tena matapishi yale! Hizo ni dalili za njaa na kupenda rushwa maana ccm haiwezi kupata kura bila kununua kwa wenye njaa zenu na mliotayari kudhalilisha utu wenu kwa kunuliwa kwa 10k endeleeni maana hata wakati wa uhuru wapo waliopenda kuendelea kutawaliwa!
 
Wenje jamaa smart sana! Namkubali

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Majimbo yote ya mwanza yanarudi ccm 2015 wanamwanza wamechoka na migogoro yenu wana cdm

Nafikiri hao watu wasingekuwa wanahudhuria. Sasa mbona wanahudhuria mikutano yao bila hata ya kusombwa na maroli? Bila hata ya kupewa khanga na vitenge? Bila hata ya kupikiwa pilau? Bila kusombwa mashuleni na viwandani kama tufanyavyo cc ccm?

Haya ndiyo mambo ya viashiria tunavyopaswa Kuviangalia na kutambua kwamba Watanzania wametuchoka CCM. Tunashinda kwa msaada wa tbc, polisi, rushwa na vitisho vya shimbo. Nakuambia ukiachia wananchi waamue kwa utashi wao sisi wametuchoka. Mpaka naombea Mungu nisipangwe kwenye hizi ziara za Ccm na Kinana.
 
Hata mfanye vipi Chadema hamuwezi kuchukua Jimbo la Geita, waulizeni Cuf mwaka 2005 kilichowapata na hata nyie mwaka 2010.
 
Mlichofanya ni kuiba kura.. Sasa wewe endelea kubweteka kwa kudhani 2015 itakuwa kama 2010..

2005 walisema watahakikisha kura hazitaibiwa 20015 lakini ikawa kinyume.
EMPTY PROF
DODOMA CITY
 
Hata mfanye vipi Chadema hamuwezi kuchukua Jimbo la Geita, waulizeni Cuf mwaka 2005 kilichowapata na hata nyie mwaka 2010.

hivi tanzania ya mwaka 2012 unaweza ilinganisha na tanzania ya 2005 hakika ni ***** kama wewe ndiyo unaweza ifananisha..halafu CUF na CDM ni vitu viwili tofauti..
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom