Picha: Watu watatu wauawa kwa kuchomwa moto kwa tuhuma za wizi wa pikipiki wilayani Kahama

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
8d788ef8746c956c6baa1f0153c4f9e7.jpg


Wananchi waliojichukulia sheria mkononi jana wamewaua kwa kuwachoma moto watu watatu ambao majina yao bado hayajafahamika katika kijiji cha Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama, mkoani Shinyanga kwa tuhuma za wizi wa pikipiki.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji ya mtu wa kwanza yamefanywa majira ya saa nane usiku kuamkia jana baada ya kutokea wizi wa pikipiki, huku watu wengine wawili wakiuawa jana majira ya saa nne asubuhi.

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa wa kwanza alipokamatwa aliwataja wenzake wawili waliouawa jana baada ya kuvunja nyumba ya mmoja wao na kukuta pikipiki tatu zimehifadhiwa kwenye shimo.

Afisa Mtendaji wa mtaa wa Kitwana, Peter Joseph amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akilaani vikali kitendo cha wananchi kujichukulia sheria mkononi, na kuwataka kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria.

Miili ya marehemu hao imechukuliwa na jeshi la polisi wilaya ya Kahama na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya wilaya ya Kahama.

f00f5d782d0f830d65f7e212123ad981.jpg
f0df749256d050b81a471cf12e6e834c.jpg
 
Habari wanaJF,

SHINYANGA: Wananchi wenye hasira kali katika kijiji cha Kitwana Wilayani Kahama wamewateketeza kwa moto vijana wa kiume watatu wakiwatuhumu kwa wizi wa Pikipiki.


Screenshot from 2017-07-05 09-00-29.png


Screenshot from 2017-07-05 09-01-11.png


Screenshot from 2017-07-05 09-05-03.png
 
Siku zote nasema tz hakuna amani ila Kna utulivu!ipo Siku hao watu wanaojichkulia sheria mkononi wataahamisha nguvu hzo Kwa wale wezi wakubwa wa rasilimali za nchi!

OvA
 
Maisha haya dah wakati wezi wa mabilioni wako uraian wanakula bata ao wachache ndo wapo lupango wanakula ugari wa bure
 
Huu utahira wa kuuwa watu km mbuzi kwanini unaendelea?

Na MTU akichomwa kmakosa itakuwaje

I wish I could be igp

Hizo sura zilizochoma watu zngezekea magereza
 
Wananchi waliojichukulia sheria mkononi leo wamewaua kwa kuwachoma moto watu watatu ambao majina yao bado hayajafahamika katika kijiji cha Kitwana kata ya Busoka wilayani Kahama,mkoani Shinyanga kwa tuhuma za wizi wa pikipiki.

Kwa mujibu wa mashuhuda, mauaji ya mtu wa kwanza yamefanywa majira ya saa nane usiku wa kuamkia leo baada ya kutokea wizi wa pikipiki, huku watu wengine wawili wakiuawa leo majira ya saa nne asubuhi.

Inaelezwa kuwa mtuhumiwa wa kwanza alipokamatwa aliwataja wenzake wawili waliouawa leo baada ya kuvunja nyumba ya mmoja wao na kukuta pikipiki tatu zimehifadhiwa kwenye shimo.

Afisa mtendaji wa mtaa wa Kitwana, Peter Joseph amekiri kutokea kwa tukio hilo huku akilaani vikali kitendo cha wananchi kujichulia sheria mkononi, na kuwataka kuacha tabia hiyo kwani ni kinyume cha sheria.

Miili ya marehemu hao imechukuliwa na Jeshi la polisi wilaya ya Kahama, na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama.
8d37f8e8ab2574a8501c41788723a88f.jpg
5773297d22bf11f8d1cc488c15af19ef.jpg
b021acad9f4fdd849deed230d98fff92.jpg
98d665bd5d1f416b01ab8bf9c5e61456.jpg
 
kuna jamaa yangu alipeleka pikpik yake kwa fundi,fundi alipomaliza akaenda kutest huko akagonga mtoto akakimbia
pikpik akapewa mwenyewe,pasipokujua akapita eneo lile lile alipogongewa mtoto,wananchi wakambana kwanini kagonga kakimbia,hawakutaka maelezo wakampa kipigo hatari,kuja kugundua kuwa sio yeye,ashauwawa
 
Nchi hii kila mtu anajichukulia sheria mikononi; kuanzia Raisi, Polisi wenyewe, wakuu wa wilaya, Spika wa Bunge, nk. Sasa kwa nini wananchi tusijichukulie sheria mkononi? It is now the name of the game.
 
Siku zote nasema tz hakuna amani ila Kna utulivu!ipo Siku hao watu wanaojichkulia sheria mkononi wataahamisha nguvu hzo Kwa wale wezi wakubwa wa rasilimali za nchi!

OvA
Hilo ni ngumu kutokea mkuu...rasilimali ni za watanzania wote..ila mali ya mtu binafsi inamgusa mwananchi moja kwa moja hivyo uchungu wake ni mkubwa sana mpaka kufikia kufanya maamuzi magumu yaliyojaa machungu.

Usiombe kuibiwa ndipo utajua kwanini wezi wanauawa kikatili.Hicho ndicho wanachostahili..Maana ukiwapeleka polisi watatoka tu na kuendelea na ujambazi huo otherwise serikali iweke adhabu kali ndipo itashawishi uma kuamini vyombo vya dola.Arabuni hawataki upumbavu..mwizi ukidakwa ni kukata mkono.
 
Back
Top Bottom