PICHA: WATU WALIOPIGWA NA POLISI; Mmoja kwa JINA LA SALUM BAKARI MUYA asema alikatwa NGOZI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA: WATU WALIOPIGWA NA POLISI; Mmoja kwa JINA LA SALUM BAKARI MUYA asema alikatwa NGOZI

Discussion in 'Jamii Photos' started by nngu007, Oct 31, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]Wednesday, October 31, 2012[/h][h=3][/h]

  [​IMG]
  Salum Bakari Muya alidai aliteswa kwa kukatwa ngozi kwa kisu kichwani na kasha kunyonyolewa nywele
  [​IMG]

  Na Salma Said.
  Polisi wadaiwa kumtesa mbeba mizigo Zanzibar.
  MTU moja makazi wa Mkele jana alinusurika kuuawa katika msako wa kuwakamata watu wanaotuhumiwa kusababisha vurugu zilizotokea wiki moja iliyopita mjini Zanzibar.

  Vurugu hizo ziliibuka Oktoba 17 mwaka huu baada ya kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMUIKI) Sheikh Farid Ahmed Hadi kutoweka katika mazingira ya kutatanisha Oktoba 16, mwaka huu.
  Akizungumza na waandishi wa bahari mjini hapa jana, kijana aliyenusurika kuuawa, Salum Bakari Muya alidai aliteswa kwa kukatwa ngozi kwa kisu kichwani na kasha kunyonyolewa nywele polisi ambao pia walikuwa na silaha.

  Alisema kabla ya kukutwa na tukio hilo alikuwa amekaa na wenzake wakiwa wanasubiri tenda ya mizigo ya kusafirisha kwa kutumia magari ya punda.

  “Nilikuwa nabangaya – yaani kubangaiza –wakatokea polisi sita, walipofika nilipokaa wakanifunua kofia na kunikata kipande cha ngozi na nywele kichwani kwa kisu,” alisema Salum. Alidai polisi waliomfanyia ukatili huo ni wa kikosi cha FFU na kwamba baada ya kitendo hicho waliamua kumpeleka kituo cha afya cha JKU kilichopoa Saateni kwa matibabu ya awali.

  Salum alidai kuwa baada ya kupata matibabu katika kituo hicho cha JKU iliamriwa kwamba apelekwe Hospitali Kuu ya Mnazimoja kwa vile alikuwa anavuja damu nyingi. Hata hivyo alisema alishangaa kabla ya kufika Mnazimoja polisi hao waliamua kumtekeleza katika eneo la kwa Abbas Hussein, kilometa chache kutoka walipomtoa hospitali ya JKU.

  “Hawakunifikisha Manazimoja, wakaniacha na kuondoka huku wakisema ubaya ubaya mtakoma waambie na wenzio,” alisimulia Salum akiwa na bandeji aliyofungwa wakati anapata huduma ya kwanza. Alisema baada ya kutelekezwa na polisi aliamua kwenda Welesi huko Kikwajini kwa lengo la kuzungumza na waandishi wa habari juu ya mkasa uliompata.

  Baada ya kusimulia mkasa huo, Salum ambaye alifuatana na kaka zake walioomba wasiandikwe majina baadae alipelekwa hospitalini kwa matibabu zaidi. Alipoulizwa juu ya tukio hilo, Kamishana wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa alisema bado hajapopewa taarifa na kwamba iwapo mwathirika atalalamika kituoni polisi watachukua hatua ya kucunguza.

  “Tumezoea kulalamikiwa, kama mtu amefanyiwa ukatili kwanini asiripoti kituo cha polisi, hapo ujue kuna jambo anaficha,” alisema Kamishna Mussa. Lakini baada ya kuelezwa na mwamdishi wa habari hizi kwamba kijana huyo amepelekwa hospitali na kaka zake, Mussa alisema aliahidi kufuatilia tukio hilo.

  Kitendo cha Salum kufanyiwa ukatili na watu wanaodaiwa kuwa polisi kimetanguliwa na matukio ya vijana wenguine wawili kuuawa wakati wa utekelezaji wa zoezi la msako huo mjini Zanzibar mwezi Oktoba mwaka huu. Imedaiwa kuwa Hamad Ali Kaimu aliuawa Ijumaa iliyopita wakati akiwa mikononi kuwa polisi katika eneo la Magomeni, na Salum Hassan Mahanju alikufa baada ya kupigwa risasi katika maeneo ya Amani Fresh na watu waliotajwa kuwa maofisa ulinzi na usalama.

  Mbali na vijana hao, askari mmoja Koplo Said Abdulrahman aliuawa na watu wasiojulikana huko Bububu baada ya tukio la kutoweka Sheikh Farid.


  at 7:01 AM   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Is it a fair GAME or share GAME????
   
 3. a

  anin-gift Senior Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 165
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  a fair game to non sense uamsho.
   
 4. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  hahaaahah, huyu wamemtahiri kichwa hahaaha
   
 5. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mbona story yake kama haimake sense! Wamemkuta kakaa anasubir mizigo wamemkata ngozi kichwan wamempeleka zahanat then wakat wakielekea mnazi1 wakamtelekeza......
   
 6. Ngida1

  Ngida1 JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2012
  Joined: Aug 25, 2009
  Messages: 554
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  "Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, kijana aliyenusurika kuuawa, Salum Bakari Muya alidai aliteswa
  kwa kukatwa ngozi kwa kisu kichwani na kisha kunyonyolewa nywele na polisi ambao pia walikuwa na silaha".


  I say, hii inasikitisha. Haya mambo yalikuwa yafanywe na mkoloni na sio na JK!!!


  ZANZIBAR NI KWETU: POLISI WAFANYA UNYAMA MKUBWA SANA ZANZIBAR!


   
 7. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  JK alikuja huko..? Du..!
   
 8. mtwana

  mtwana JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 399
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 45
  Kaka sio la kucheka au kwa kua hayajakukuta wewe?
   
 9. i pad3

  i pad3 JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,520
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  mnafikiri mlivyoua askari mwenzao wataendelea kuwachekea tu daily.
   
 10. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Kwa nini walimchagua yeye?
   
Loading...