Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 15,795
- 28,447
Huenda ukadhania kwamba rais wa Ufilipino Rodrigo Durtete na mwenzake wa Korea Kaskazini Kim Jong Un walikuwa pamoja katika barabara za mji wa Hong Kong, wakipiga picha na kula pamoja chakula cha jioni katika mgahawa mmoja.
Lakini uchunguzi wa kina ulibaini kwamba wawili hao walikuwa watu waliowaiga viongozi hao wawili.
Kutana na jamaa anayejiita Cresencio Extreme anayefanana na Durtete na Howard X anayefanana na Kim Jong un.
Wawili hao waliobeba bunduki bandia walisalimiwa na wafanyikazi na raia walipowasili katika mgahawa huo wa kuku karanga au Fried Chicken Restaurant.
Walihudhuria ibada ya Jumapili katika kanisa la St Joseph's huku Cresencio Extreme (kushoto)akiwa amevalia shati jeupe ambalo hupendwa sana na rais Durtete
Mtu huyo anayefanana na rais Durtete alizua kihoja na mkanganyiko katika kanisa hilo katikati ya mji wa Hong Kong baada ya kuzungukwa na waumini
"Je huyu ni Durtete?'' Wengine hawakukubaliana naye huku raia huyo akionekana kuwa mdogo kwa umri kuwa rais wa Ufilipino pamoja na mwenzake anayemuiga rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
Wawili hao walizidi kuwakanganya raia waliopoonekana wakila chakula cha jioni katika mgahawa wa Hong Kong siku ya Jumapili.
Mr Duterte {kushoto) na muigaji wake
Bwana Kim (kushoto) na muigaji wake kulia