PICHA; Wanaharakati wa CCM Elimu Ya Juu Wapinga Mgomo wa Madaktari

Kiganyi

JF-Expert Member
Apr 30, 2012
1,242
765
1.JPG

Kundi la wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya juu nchini, wakiwa na mabango jana katika hospitali ya taifa, Muhimbili, Dar es Salaam, kushinikiza madaktari waache mgomo.
2.JPG
Kiongozi wa wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya juu Abubakari Assenga (kushoto), akiwa na Katibu wa Jumuia ya Madaktari Tanzania, Edwin Chitange, baada ya maandamano ya wanaharakati hao kufika Muhimbili kushinikiza madaktari kusitisha mgomo
5.JPG
Kiongozi wa wanaharakati kutoka vyuo vya elimu ya Juu, Abubakar Assenga akizungumza na waandishi wa habari baada ya maandamano yao kufika Muhimbili kushinikiza madaktari kuacha mgomo.
3.JPG
Mwanamke aliyekuwa akisubiri kuona mgonjwa wake, Katika hospitali ya Muhimbuli, Dar es Salaam, Helen Thomas, akisoma bango lililoachwa na wanaharakati hao wa vyuo vya elimu ya juu.
4.JPG
Wanaharakati wa vyuo vya elimu ya juu, wakihanikiza baada ya kufika Muhimbili kutaka madaktari waache mgomo

MY TAKE; Hivi Wanaharakati wa MAgamba Vyuo vikuu ni hao tu?
 
Hao ni wafuasi wa ccm na ndio maana wameruhusiwa kuandamana.Jiulize wangekuwa wanaandamana kuunga mkono mgomo wa madaktari wangeruhusiwa?Ungesikia taarifa za kintelijinsia zinaonyesha uwezekanoi wa kutokea fujo na maandamano yangepigwa maarufuku.
Hili jeshi la polisi liko kisiasa zaidi.
 
  • Nani karuhusu haya maandamano??
  • wanakibali cha haya maandamano?????????
  • mama wa haki za binadamu akiomba kibali au kufanya maandamano atapewa kubali???
  • hawa ni wasomi au ni WAISLAMU WACHACHE WANAOCHOCHEWA KULETA MIGOGORO YA KIDINI?
  • yako wapi mabango yao yanayohusu hali za mahspotali na vitendea kazi??
  • nani kasema kiongozi yuko sahihi mudawote kwa kuwataka wawasikilize viongozi
WITO

KIKWETE ACHA USHABIKI TATUA MATATIZO YA HALI DUNI ZA HOSPTITALI NA VITENDEA KAZI< ACHA USHABIKI WA KUZUNGUMZIA MISHAHARA TUU..ACHA KULETA MACHAFUKO KWNY HII NCHI
 
Wangekuwa wapo against ungesikia wameandamana bila ya kibali. Ila kwa kuwa wanaeneza propaganda, basi wanakuwa ni wanaharakati toka Elimu ya juu. Hebu tufafanuleni, ni wana-elimu ya juu wapi hawa ambao wameshindwa ku-address ujumbe pande zote mbili, yani kwa madaktari na serikali pia. Je Madaktari wakirusi pasipo na vifaa muhimu wala madawa, ndiyo itakuwa suluhisho?
 
Ukijaribu kufuatilia kidogo tu utaundua kuwa wengi hapo si wasomi wa vyou vikuu, wengine wanatafuta publicity zaidi ya hapo unaweza kukuta wamepewa mwekudu tu waandamane.

Si unajua maisha yalivyo magumu chuo? Kwa waeelewa wanajua nini maana na kupigania maslahi na kuboreshwa kwa huduma ya afya. Unajua ilikuwa haijawahi kuniingia akilini kwamba wagonjwa wanalala chini tena kwenye hospitali kama mhimbili! Nilkuwepo mwaka jana ndo nilijua hilo na nilihuzunika sana kuona wagonjwa walivyorundikana.

Leo hii tunawalaumu madaktari lakini ukweli ni kwamba sisi wenyewe ndo tunatakiwa tujilaumu kwa kushindwa kujua haki zetu. kila kitu tunaona sawa tu. Kwa ulewewa wangu mdogo mgonjwa anapokwenda mhimbili nakuwa na risk zaidi ya kuambukizwa magonjwa mengine, achilia psychological effect wanazozipata wanapoona jirani yake amefariki akimshuhudia. Hata kama madaktari watarudi kutibu bado kuna tatizo kubwa la msingi ambalo ni vitendea kazi.

Just imagine hospitali kama mhimbili wanashindwa kuhudumia mtu aliyejeruhiwa tu kwa sababu ya ukosefu wa vifaa vya kufanyia kazi. Na hiyo ni hospitali kubwa kuliko zote Tanzania, Je hali ikoje huko mikoani, wilayani na vijijini? Baadhi ya hospitali na kama vyoo vya shule ya msingi!

Hebu tuache kiikingia kifua serikali tena inapofanywa na wasomi uchwara hapo ndo unajua kuwa ujinga umeishaingia hadi vyuoni wape kudesa tu!
 
Tanzania ni nchi ambayo haikosi vituko! Mtu huwezi kukaa tu na kuwa bored! Nasema hiki ni kituko kingine kama cha komedi maana mwenye akili ataona moja kwa moja kuwa hao (vijana?) wametoka upande gani.

Nasema hivi kwa sababu nimesoma mabango ambayo wameyashika, sijaona bango hata moja linalohimiza serikali nayo kutimiza wajibu wake wa kuboresha afya nchini! Hilo bango huyo mama alilolishikilia linaonyesha tu kuwa hoja kubwa ya madaktari ni kutaka nyongeza ya mishahara.

Jambo kubwa, na ambalo linawagusa wote la kuboresha huduma za afya, wao haliwahusu. Ndio maana nasema vioja haviishi Tanzania...ze Komedi wapo wengi!
 
kweli dhiki ukiiendekeza unaweza ukapandwa (waka kukameruni ) , nacheki wachumia tumbo wanavyo uza utu wao hapo
 
Njaa inapozidi mtajionea kila aina ya vibweka. Hawa kama wanajiita WANAHARAKATI basi ni Wanaharakati wa matumbo yao, hawana lolote vibaraka hawa.
 
  • Nani karuhusu haya maandamano??
  • wanakibali cha haya maandamano?????????
  • mama wa haki za binadamu akiomba kibali au kufanya maandamano atapewa kubali???
  • hawa ni wasomi au ni WAISLAMU WACHACHE WANAOCHOCHEWA KULETA MIGOGORO YA KIDINI?
  • yako wapi mabango yao yanayohusu hali za mahspotali na vitendea kazi??
  • nani kasema kiongozi yuko sahihi mudawote kwa kuwataka wawasikilize viongozi
WITO

KIKWETE ACHA USHABIKI TATUA MATATIZO YA HALI DUNI ZA HOSPTITALI NA VITENDEA KAZI< ACHA USHABIKI WA KUZUNGUMZIA MISHAHARA TUU..ACHA KULETA MACHAFUKO KWNY HII NCHI

Ulianza vizuri lakini sasa hapo UISLAM umeingiaje?
 
WAFU: Hawa ni maiti wako Hai ila ni mazoba, hata wakiambiwa na CCM walipie PUMZI na USINGIZI watalipia ingawa hawana kitu. Wanakubaliana na kila hali hawajui kupinga wala kukataa, hawana tofauti na mabehewa ya treni kinakokwenda kichwa ndiko wanakokwenda wao.

Mkuu Matola, nimeipenda sana hii ingawa inasikitisha na inatia huzuni. Iko haja ya kuwafufua hawa na kuwaambia wakate behewa linalowapeleka kuzimu kila kukicha!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom