PICHA: Vurugu Zanzibar: Mabaki Ya Kanisa Lililochomwa Moto kama ingekuwa Msikiti ingekuwaje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA: Vurugu Zanzibar: Mabaki Ya Kanisa Lililochomwa Moto kama ingekuwa Msikiti ingekuwaje?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, May 29, 2012.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Monday, May 28, 2012  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]


  [​IMG]
  Kanisa la Mpendae. Picha zote na mjumbe wa jukwaa la Mjengwablog aliye Unguja.
  Picha kwa hisani ya Mjengwa Blog   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hivi kwa fikra za kiundani kama ingekuwa ni Msikiti ndio umefanyiwa hivyo ingekuwaje??? Kungekuwa na Usalama?
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,949
  Trophy Points: 280
  hakuna tofauti na Nigeria
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,527
  Likes Received: 19,949
  Trophy Points: 280
  protests dunia nzima
   
 5. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mbona kawaida tu. Aaaagh napita tu.
   
 6. z

  zanzibar huru Senior Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 184
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Askofu pengo yuko wapi?

  mbona hatoi tamko juu ya hili?
   
 7. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Hii inasikitisha sana na sijui taifa letu linaelekea wapi ambao wale wenye wajibu wa kuliongoza ili kuwa na mwelekeo unaoeleweka hawajui nini cha kufanya, au wanajua lakini wanaacha hali hii kuendelea kwa manufaa yao binafsi.

  Hata kama madai ya waandamanaji siyo sahihi au ni sahihi nadhani ingekuwa busara kwa serikali kuruhusu huo mjadala wa masuala ya Muungano na baadaye kuwaachia wananchi waliowengi kuamua kwa njia ya kura. Hivi ilivyo na ikiachwa kuendelea hivi hali inaweza kuwa mbaya zaidi hasa endapo pia hao ambao wanachomewa mali zao nao imani zao zikiwatuma vinginevyo japokuwa hatuombei hilo.

  Serikali iwasikilize na kuruhusu mjadala wa aina ya Muungano wanaoutaka wanachi waamuwe wenyewe.
   
 8. DGMCHILO

  DGMCHILO Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuvua hijabu vs kuchoma kanisa
  nani mkorofi zaidi
   
 9. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  My brother seems that you missed the dot. Hakuna kingozi wa Kanisa ametuhumiwa mahali popote kumvua mtu hijabu katika nchi yetu if you know one you may remind me
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,928
  Likes Received: 83,495
  Trophy Points: 280
  Rais wa nchi hadi hii leo yuko kimyaaaaa
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,618
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]
  Kiongozi wa Jumuiya ya kikundi cha uamsho, Sheikh Farid Hadi Ahmed
  [​IMG]
  Baada ya jeshi la polisi kulazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya baadhi ya wafuasi wa kikundi cha uamsho kufuatia kukamatwa kwa mmoja wa kiongozi wao, hali inaendelea kuwa tete na hivi sasa baadhi ya wafuasi hao wameingia mtaani wakishinikiza kuachiwa kwa kiongozi huyo huku jeshi la polisi likilazimika kutumia mabomu kuwatawanya wafuasi hao …..

  [​IMG]
  Maelfu wa wazanzibari wakiongozwa na Taasisi za Kiislamu na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) wakifanya matembezi ya amani katika barabara za Zanzibar na kupeleka ujumbe wao kwa viongozi wa serikali za Zanzibar na ile ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Umoja wa Mataifa wakitaka Zanzibar huru ambapo baadhi ya watembeaji hao wakiongoza na Kiongozi wa Jumuiya hizo, Sheikh Farid Hadi Ahmed na viongozi wengine
  [​IMG] [​IMG]

  Maelfu ya wazanzibari leo wamefanya maandamano amani kuishindikiza Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuitisha kura ya maoni juu ya Muungano na kupeleka ujumbe kwa Umoja wa Mataifa wa kutaka Zanzibar kujitenga kama ilivyofanya Sudan ya Kusini.
  [​IMG]
  Waanamanaji hao wakiongozwa na Sheikh Farid Hadi Ahmed walitembea kutoka viwanja vya Lumumba na kupitia barabara ya Kinazini, Mpigaduri, Michenzani Maskani ya CCM Kisonge, kwa Biziredi na kurudi tena viwanja vya Lumumba.
  Maandamano hayo walioyaita matembezi ya amani yalifanyika na kuhudhuriwa na maelfu ya wazanzibari ambapo awali kuliandaliwa kongamano kubwa lililoandaliwa na Taasisi za Kiislamu kwa kushirikiana na Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa lengo la kuzungumzia mfumo wa elimu Zanzibar.

  Akizungumza na maelfu ya wazanzibari kabla ya kuanza maandamano hayo yaliitwa ni matembezi ya amani, Sheikh Farid alisema wazanzibari wana haki kama walivyokuwa na haki wananchi wengine ulimwenguni kote kudai haki yao ndani ya nchi yao....................

  [​IMG]
  “Sisi wazanzibari kama wananchi wengine wowote duniani tuna haki ya kikatiba kudai nchi yetu kama walivyodai Sudan ya Kusini,

  mbona Sudan ya wameweza kujitenda na kupata nchi yao kwa nini sisi kama wazanzibari tusikubaliwe kudai nchi yetu sasa sisi tunampelekea salam katibu mkuu wa umoja wa mataifa kumwambia kuwa wazanzibari sasa wanataka nchi yao” alisisitiza Sheikh Farid huku akiungwa mkono kwa mamia hao kuinua mikono na kusema ndiooooo.

  Awali Sheikh Farid alisema salamu hizo anataka zimfikie Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin moon ambaye kwamba wazanzibari wamechoshwa na kuwepo ndani ya Muungano ambao umedumu kwa miaka 48 lakini bado ukiwa na kero nyingi na malalamiko ambayo yanaonekana utatuzi wake ni mdogo na usiowezekana ambapo alisema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar

  hauna manufaa yena na wazanzibari.
  Katika kuonesha kwamba hawataki tume ya katiba ije kuchukua ya maoni ya katiba mpya Sheikh Farid alisema wanataka kwanza kuamuliwe suala la Muungano kabla ya jambo lolote na kuahidi kwamba wataendelea kufanya

  makongamano, mihadhara na maandamano kwa kadiri wawezavyo hadi hapo serikali itakaposikia kilio hicho.


  “Ujumbe huu tunautoa kwa Ban Kin moon, na kwa ulimwengu mzima lakini pia tunataka rais wetu Dk Shein asikie kilio hiki na Rais Kikwete ambaye yeye ni mtetezi wa haki za binaadamu na pia ni mfuatiliaji wa nchi zinazovunja haki za binaadamu tunataka asikie kilio cha wazanzibari kuwa wanataka nchi yao” alisema.


  Alisema juzi wamefanya maombi maalumu ya kumuombea Rais wa Zanzibar lengo likiwa ni kumjaaliwa kheri na awe na maamuzi sahihi juu ya wananchi wa Zanzibar sambamba na kuwaomba Makamu wa Kwanza na makamu wa Pili wa Zanzibar kusikia kilio cha wazanzibari wasiotaka Muungano.


  “Tunamuomba Rais wetu Dk Shein, Makamu wa Kwanza Maalim Seif na Makamu wa Pili Balozi Seif kwamba sisi wazanzibari tunahitaji Zanzibar huru, tunahitaji heshima ya nchi yetu na tupo tayari kwa lolote kwa hivyo tunataka salamu hizi na ujumbe huu ukufikieni” alisema Sheikh Farid huku akiungwa mkono na maelfu waliohudhuria katika kongamano hilo ambalo awali liliandaliwa kwa lengo la kuzungumzia masuala la elimu na mfumo wake.


  Akiendelea kutoa salamu hizo mara Sheikh Farid alisoma kifungu cha 16 cha katiba na kuwaleza wananchi kwamba haki ya kutembea ni haki ya kila mwananchi ambayo imeainishwa katika katiba na sheria za haki za binaadamu hivyo aliwageukiwa na kuwataka wasimame na kisha kumfuata yeye.


  “Haki ya kutembea ni haki ya msingi kwa mujibu wa sheria na kifungu cha 16 kinatupa haki ya kutembea sasa mimi nataka kutembea jeee mpo tayari kutembea na mimi? Alihoji Sheikh huyo huku akijibiwa na umma mkubwa kwamba ndioooo”


  Aliongeza kwamba “Tunaanza kutembea na tuone mtu atukamate tunakwenda njia ya kinazini, tunapita michenzani, tunapita barabara ya kwa biziredi na kisha tunarejea hapa hapa kuendelea na kongamano letu kwa amani kabisa mmesikia….akajibiwa ndiooooo”


  baada ya kusema hivyo Sheikh Farid alitoa takbir na kuanza kukamatana mikono na viongozi wenzake na huku ummati mkubwa ukiwa umekamatana mikono nyuma na kuanza safari kwa pamoja na kutembea katika barabara ambazo walizitaja awali.


  Waandamani hao walikamata mabango yenye maandishi mbali mbali ikiwemo hatutaki muungano, tunataka nchi yetu, zanzibar bila ya muungano inawezekana na wengine kadhalika huku wakitembea njiani na kupiga takbir ambapo walikuwa wakisema Mwenyeenzi

  Mungu Mkubwa, Mwenyeenzi Mungu Mkubwa sisi hatuna uwezo isipokuwa tunakutegemea wewe Mwenyeenzi Mungu.

  Waandamanaji hao walianza kutembea kwa utaratibu maalumu huku magari yakisimama na kuwapisha bila ya kuwepo jeshi la polisi ambapo viongozi wa jumuiya hiyo na wananchi wengine waliongoza utaratibu huo na kutembea katika barabara kwa utaratibu mzuri hadi

  kumaliza maandamano yao waliyoyaita matembezi ya amani.

  Baadae jeshi la polisi lilifika katika eneo ambalo kumefanyika maandamano hayo na kufungua mabango yao ya kuwataka watu

  kuondoka lakini wakati magari hayo ya polisi matatu yanafika eneo hilo la Kariakoo tayari ummati mkubwa ulikuwa umeshapita katika eneo hilo na hivyo kuingia ndani ya magari yao na kuondoka kwa salama.


  Awali akitoa mada katika kongamano hilo, Maalim Abdulhafidh Malelemba alisema sekta ya elimu imekuw aikidorora Zanzibar kutokana na kukandamizwa na mambo ya Muungano ambapo kila mwaka wanafunzi wanapofanya mitihani kufelishwa kwa makusudi huku idadi

  ya wanafunzi wanaokwenda katika vyuo vikuu wakiwa kidogo kutokana na kufelishwa katika mitihani ambapo husainiwa na baraza la mithani Tanzania (NECTA).


  Wakizungumza katika nyakati tofauti katika kongamano hilo, baadhi ya walimu walisema kukosekana kwa baraza la mitihani Zanzibar kusimamia mitihani ya elimu ya juu ndio sababu ya wazanzibari kufelishwa kwa wingi na kushindwa kuingia katika vyuo vikuu kwa kuwa wanafunzi wengi wa Zanzibar hufelishwa.


  Walimu hao walitoa ushahidi wa hivi karibuni wa kufelishwa wanafunzi wa kidatu cha nne ambapo walisema lile ni tukio la makusudia lililofanywa na baraza la mitihani ikiwa ni kuwadhoofishwa wanafunzi wa Zanzibar ili wasiendelee katika masomo kwa kuwafelisha.

  Hali ilivyokuwa Zanzibar

  Kasheshe kweli ndugu zetu wa Ki Zanzibar.

   
 12. Brightman Jr

  Brightman Jr JF-Expert Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: Mar 22, 2009
  Messages: 1,233
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni UPEPO tu wa kidini utapita. Huenda makanisa ni chanzo cha kuwanyima waznz kuvunja union.
   
 13. DGMCHILO

  DGMCHILO Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: Aug 6, 2011
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Kuvua hijabu vs kuchoma kanisa
  nani mkorofi zaidi
   
 14. Maarko

  Maarko JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,030
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Wanadai haki ni sawa ni bora wajitenge kuliko kukaa kwenye Serikali ya Muungano iliyo ya kifisadi namna hii.
   
 15. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  je anafurahi?; maybe someone is doing the dirty work for him
   
 16. t

  thatha JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Mkuu msikiti nyumba ya mungu. Mkichoma hata mji mnaokaa itabidi muukimbie wenyewe
   
 17. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Tamko litasaidia nini wakati kanisa limeshaungua?
   
 18. M

  Mujwahuzia Senior Member

  #18
  May 29, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 137
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yalifanyika maandamano ya nguvu kupinga kwa mkuu wa wilaya ya Igunga kuvuliwa mtandio ambao yeye aliuita ni Hijab viongozi wakuu wa dini ya kiislamu waliacha shughuli zao za kulihubili neno la Mungu wakaanza maelezo marefu juu ya huyo mkuu wa wilaya na Hijab yake. Kama sio Busara za msamalia mwema anayeifahamu vizuri dini ya kiisilamu kutoa maelezo na ufafanuzi juu ya vazi hilo la mkuu wa wilaya basi ingekuwa taabu kidogo ufafanuzi ulikuwa huyo mama kwanza kabila lake ni Mchagga yeye alijiegesha kimaisha kwa bwana mmoja ambaye ni Mwisilamu hawakufunga ndoa hivyo hata maana ya hijabu huyo mkuu wa wilaya hijui ndio maana hata kelele za kesi hiyo zimepungua. leo hii Makanisa ya waumini wenzetu yanachomwa moto viongozi wa kiislamu wanatoa maelezo mepesi tu juu ya tukio hilo kama ni swala muungano linatatuliwa kwa uchomaji makanisa basi hata Misikiti, majengo ya Serikali zingechomwa moto hapo tungejua kweli watu hawataki huo Muungano kuna jambo lipo nyuma ya Pazia.Mujwahuzia.
   
 19. m

  mob JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,028
  Likes Received: 511
  Trophy Points: 280
  MUNGU utujalie tuishi kwa Amani na upendo pasipo kuwepo na ubaguzi wa dini,rangi ,kipato wala ukabila,utujalia uvumilivu na hekima wakati wa kujadili masuala yenye Manufaa kwa taifa letu.
   
 20. L

  Laurano Senior Member

  #20
  May 29, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 103
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni kweli Yupo Mungu na miungu, Mungu wa kweli hapendi fujo, Mungu wa kweli ni wa upendo, Mungu wa kweli ni amani. Amani ya Kristo na iwafunike watu wa Mungu Zanzibar tunawaombea.
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...