Dr. Stephen Ulimboka alivyopokelewa Dar akitokea Afrika Kusini

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
00.jpg


003.JPG


007.JPG
 
wasiwasi kama sio hofu ndo zinazidi kuwajaa huko waliko..hivi anaweza akaitisha press akatupa walau mawili matatu ya kilichojiri? au pia itakuwa ni kuingilia mhimili ule mwingine.
 
DK. ULIMBOKA AREJEA, ATOA NENO ZITO

-Wanahabari wakimsubiri kwa hamu Dk. Ulimboka.…


Dk Ulimboka akiwa amezungukwa na wananchi waliofika kumpokea leo.
MWENYEKITI wa Jumuiya ya Madaktari, Dk. Stephen Ulimboka, ametua nchini leo mchana kisha kutoa neno zito.

Dk. Ulimboka, aliwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, saa 8:00 mchana, akitokea nchini Afrika Kusini, alipokwenda kwa matibabu.
Madaktari wenzake na wananchi wengine, walimlaki kwa mabango yaliyosomeka:
“Dk. Ulimboka karibu nyumbani.”
“Dk. Ulimboka, damu yako iliyomwagika inaamsha ari ya wananchi kudai haki ya afya.”
“Dk. Ulimboka wewe ni mpigania haki ya afya bora kwa wananchi wote. Mungu na Watanzania wote tuko nawe.”

Kwa upande mwingine, Dk. Ulimboka baada ya kukuta umati mkubwa uwanjani, alishindwa kujizuia, hivyo akatoa machozi kisha akasema: “Nawashukuru sana Watanzania kwa kuwa pamoja na mimi kwa maombi, sasa nimerejea nikiwa na afya njema, mapambano yanaendelea.”

Huku uwanja wa ndege ukiwa umepambwa na mabango mengi ya kumpamba na kumuunga mkono, Dk. Ulimboka aliongeza: “Watu wacheze na watu lakini wasicheze na Mungu, hasa Mungu wangu mimi.”

Juni 26, mwaka huu, Dk. Ulimboka alitekwa na watu wasiojulikana, kupigwa na kujeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili, kisha kutupwa katika Msitu wa Mabwepande, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.

Ulimboka, alitekwa wakati akiwa anaratibu mgomo wa madaktari na katika utekaji huo, alidaiwa kuvunjwa mbavu, miguu yote miwili, kung’olewa meno yote ya mbele na kuumizwa vibaya katika sehemu mbalimbali za mwili wake.
Global Publishers

 
[h=3]MAMIA WAMPOKEA DK. ULIMBOKA KISHUJAA AIRPORT[/h]


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akipata mapokezi makubwa wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, akitokea nchini Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana. Picha ya chini ikimuonesha Dk. Ulimboka akiwa katika hali mbaya baada ya kuokotwa katika msitu wa Mabwepande, Juni 27. (Picha na Habari Mseto Blog)<o:p></o:p>


Dk. Ulimboka akiwasili leo kutoka nchini Afrika ya Kusini alikokwenda kwa matibabu.

Wanaharakati wakipaza sauti wakati wa mapokezi ya Ulimboka.

Dk. Ulimboka akiwapungia mkono baadhi ya madaktari wenzake waliofika kumpokea

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akiwa ameshika ua mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, akitokea nchini Afrika Kusini kwa matibabu

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madakatari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka akiwa ameshika ua mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam jana, akitokea nchini Afrika Kusini kwa matibabu baada ya kutekwa na kuteswa na watu wasiojulikana. Picha ya kulia ikimuonesha Dk. Ulimboka akiwa katika hali mbaya baada ya kuokotwa katika msitu wa Mabwepande, Juni 27.
Baadhi ya Wanaharakati pamoja na Madaktari wakilisukuma gari alilokuwa amepanda Dk Ulimboka mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
 
Wingi huu wa watu una ujumbe pia,kwetu wananchi na kwa serikali

Inatia moyo sana kuona wingi wa watu waliokuja kumpokea. Hii itawapa imani madaktari na wapigania haki wengine nchini kwamba hawako pekee yao katika vita dhidi ya Serikali dhalimu.
 
MAMIA WAMPOKEA DK. ULIMBOKA KISHUJAA AIRPORT












Juni 27.
Baadhi ya Wanaharakati pamoja na Madaktari wakilisukuma gari alilokuwa amepanda Dk Ulimboka mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.


Huyu mama Ananileya Nkya mie ninamzimia sana kwa juhudi zake za kuwa mstari wa mbele kupambana na Serikali hii dhalimu. Ningependa kuona 2015 anagombea Ubunge katika jimbo lolote lile ambalo atalichagua mwenyewe.
 
ni kweli Dr. anagusa mioyo ya Watanzania maana sidhani kama katika hawa waliojitokeza kumpokea kuna hata mmoja aliyealikwa au kugawiwa nauli kufanya hivyo kama tulivyozoea.

...naendelea kumkubali mama Ananielia Nkya kama mtu mwenye nia ya dhati na kuguswa na matatizo yaliyopo nchini hivi sasa!
 
Dr. Ulimboka anatakiwa kusema ekweli juu kile kilichotokea ili umma wa Tanzania tujue.

Ukweli alisha usema kabla hata hajaondoka anatakiwa kuwafungulia mashitaka wale walio mteka na kumtesa...!
 
Mungu ambariki Dr. Ulimboka, na kurudi kwake salama kuwa chanzo cha mabadiliko ya kweli katika mfumo wa afya na mahusiano kati ya serikali na wadai haki.
 
Back
Top Bottom