Picha - Uamsho Zanzibar ngangari hadi kieleweke | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha - Uamsho Zanzibar ngangari hadi kieleweke

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Candid Scope, May 27, 2012.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]

  [​IMG]
  Picha hisani ya Michuzi blog

  Licha ya mabomu na vitisho vya serikali, waandamaji Zanzibar wangali ngangari kudai maoni yao kuhusu serikali ya Muungano. Haki ya wananchi si kitu cha kuporwa kirahisi siku hizi. Bora tu kusikiliza madi yao na kuyafanyia kazi, lakini nguvu si lo lote na si chochote kwani ni kuchochea zaidi vurugu. Madai yao hayajasikilizwa muda mrefu na kudharaulika kila walipotaka kutoa maoni yao, matokeo leo ndiyo haya.
   
 2. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #2
  May 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Binafsi sijui kwanini hawa watu anaachwa waendelee kutupa tabu. ukiskiliza kwa makini ni like wamechoka kuugana, sasa kama ndoa ikiwaboa wawili nyie na ikafikia mmoja akawaanadai talaka kwa mtutu ni bora nn? Nafkir ni bora apewe haki yao sisi tuendelee na bara yetu.kwao kuua ni jihad
   
 3. bampami

  bampami JF-Expert Member

  #3
  May 27, 2012
  Joined: Nov 5, 2011
  Messages: 4,847
  Likes Received: 1,286
  Trophy Points: 280
  BABA WA TAIFA JULIUS KAMBARAGE NYERERE, Upo wapi Mwalimu wa nchi hii,Baba yetu ungekuwepo leo hii NENO LAKO MOJA TU LINGEBADILISHA NCHI HII.
  Haya uliyasema na kuyatabiri mda mrefu sana. NAKUMBUKA WAKATI WA UCHAGUZI 1995 ULIONGEA MAMBO MENGI KUHUSU MUUNGANO. Leo hii yanatokea hakuna anayeweza kukumbuka uliyosema. NARUDIA....SEMA NENO MOJA TU HUKO ULIKO LIBADILISHE NCHI YETU.
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana nawe, kwani picha hizi ni maandamano yanayoendelea baada ya mabomu usiku kucha asubuhi wameamkia maandamano. Wapeni haki yao wanayodai, kuendelea kuwanyima haki yao ni kuchochea machafuko kama haya tunayoshuhudia sasa.

  Somo la urahia kuhusu sheria na haki ya kuhoji muungano lililotolewa na Tundu Lisu linafanya kazi yake, na hapa wameshaamua hadi kieleweka, hakuna kurudi nyuma.
   
 5. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #5
  May 27, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,943
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikir hata kama ni kuuenzi Muungano but now patnaz wetu ameuchoka kiasi kwamba wanatishia amani ya nchi.

  Huwa najiuliza swali hili hivi muungano usiokuwa na amani na utengano wenye amani ni kipi bora? Pia kama muungano utagharimu amani yetu kwanini tuwe nao? dhana ya kwamba tukitengna tz itakuwa hatarini kiusalama imeshapitwa na wakati wanunue rada iwe inasoma usalama a taifa kwenye mipaka yetu.
   
 6. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #6
  May 27, 2012
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hatari
   
 7. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #7
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ndio kitu ninachojiuliza, kwa nini inatumika nguvu kubwa kuzima hoja ya kujadili Muungano? Inawezekanaje kufanya mabadiliko ya Katiba ya nchi ambayo ndani kuna vifungu vya Muungano huku vifungu hivyo visijadiliwe inatoa taswira gani? Je muungani unafaida kwa wananchi wa nchi hizi mbili au kwa viongozi tu wa juu wa serikali?
   
 8. Mfarisayomtata

  Mfarisayomtata JF-Expert Member

  #8
  May 27, 2012
  Joined: Feb 2, 2012
  Messages: 417
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Wawape uhuru jamani inatosha basi, wanatia huruma! Hasa huyo mwenye ndevu ka beberu.
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  May 27, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  lakini ni kwanini serikali ya ccm haioni ulazima wa kurudisha tanganyika then tuwe na serikali tatu!
   
 10. asrams

  asrams JF-Expert Member

  #10
  May 27, 2012
  Joined: Sep 4, 2011
  Messages: 4,000
  Likes Received: 1,364
  Trophy Points: 280
  Yupo kafukiwa Musoma,


  Sent from my NOKIA 3310 using Tapatalk HD
   
 11. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #11
  May 27, 2012
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Waishie huko huko na vurugu zao wasizivushe huku ng`ambo.

  Hawa watu wa majambia wagumu sana kuelewa!
   
 12. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #12
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Lakini kumbuka wanachodai ni haki yao ya msingi, na wanawajibika kwa uhuru wao kuamua kuukubali Muungano au kuukataa kama wanavyoukana sasa. Kuna faida gani kung'ang'ania Muungano, unatufaidia nini Watanganyika kama si kutuongezea mzigo tu?

  Bajeti kubwa, wanaongeza ukubwa wa Bunge, wanatuchukulia ajira zetu wabara wakati sisi Wabara hatutii pua huko Kwao Zenj.
   
 13. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #13
  May 27, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Tatizo si Wao Tatizo ni Viongozi wa Dini zao wanawalisha Matope.
   
 14. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #14
  May 27, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Mkuu sema kwamba tatizo ni viongozi wa Dini zao wanaowafungua macho na wala siyo kuwapaka matope.
   
 15. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #15
  May 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160

  Tusiwasingizie viongozi wa dini yao kwa kila ajenda, hili la Muungano ni kitendawili kilichotegwa, kufumba na kufumbua ipo siku wanaotetea kwa nguvu zote wataumbuka.

  Ndoa za kushinikizwa zina matatizo mengi sana tofauti na ndoa za hiari ya wanandoa kwani kwa maamuzi yao sahihi wamekubaliana kwa ridhaa yao kufunga ndo, lakini hizi za mkeka matokeo ndo hayo.
   
 16. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #16
  May 27, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  hawana lolote,washajazwa ujinga huko madrasatul....
   
 17. Shakazulu

  Shakazulu JF-Expert Member

  #17
  May 27, 2012
  Joined: Feb 23, 2007
  Messages: 940
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  I admire the people from Zanzibar as they know their rights.
   
 18. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #18
  May 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  mshaolewa nyinyi na aliyekula mahari ashakufa..so no separation here...

  ndoa ngumu vumilieni mtafika tuu
   
 19. leroy

  leroy JF-Expert Member

  #19
  May 27, 2012
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 834
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 60
  Ningepeleka majeshi na kudhibiti waandamanaji kwa namna yoyote ilimradi amani na utulivu vipatikane. Ningehakikisha jeuri yao naikomesha na chokovhoko za vikundi vya kidini nazimaliza kwa kuwabana viongozi.

  Ningeongeza magari ya washawasha na kuongeza idadi ya wanajeshi kutoka bara.
   
 20. Bakari Maligwa

  Bakari Maligwa Member

  #20
  May 27, 2012
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...Katiba ya Zanzibar Toleo la 2010 inatambua kwamba, "Zanzibar ni nchi ndani ya Jamhuri ya Muungano." Na huu ndi ukweli wa kihistoria, siyo?! Tatizo lisilotatuliwa ni kwa nini Tanganyika haitaki kuwa na katiba yake na kuitambulisha Tanganyika kwenye muungano (?)! Huu ni mshangao unawafanya baadhi ya Wazanzibari kudahi kwamba Tanganyika ina "agenda" ya siri nyuma ya muungano wa kulazimisha!

  Cha ajabu na cha kusikitisha; CCM ilipowaruhusu Wazanzibari kuanzisha mchakato wa kuanzisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUKI) ndani ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) walidhani itaishia hapo...; walijidanganya hata pale walipokubali kuanzisha mchakato "ghushi" wa katiba kwamba watawabana wananchi wa Zanzibar wasiujadili muungano, hasha; wameshindwa! Nadhani wameweza kuwatia "uzezeta" wananchi wa bara kwa kuwa watu wa Tanganyika wamezowea kuburuzwa na kwao muungano hawaujui kwa jinsi wanavyoujua wananchi wa Zanzibar. Zanzibar wanajitambua na wanajijua; Watanganyika wamejishahau kama "misukule" au "mandondocha" waliyechukuliwa na wachawi na kufanywa "mazemule."

  Nadhani hakuna asiyeona harakati za utambuzi na utambulisho wa Wazanzibari; na mara zote kunapotokea hamkani ya kisiasa visiwani wanaotafuta sababu ya kutuliza gafugafu la joto la kisiasa huwa ni Watanganyika kwa kutumia nafasi yao kama ilivyokuwa mwaka 1964 na kama alivyofanya Mwalimu Nyerere...wanafunika "kawa" mwanaharamu apite ilhali wanalikuza tatizo la sintofahamu ya muungano badala ya kutafuta ufumbuzi wa kudfumu wa muungano!

  Hivi; kama Wazanzibari wanataka kupiga kura ya maoini juu ya muungano kuna kosa gani? Na hata wakiukataa muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwani ni dhambi? Tuache uwendawazimu wa kudhani vile tunavyodhani kla siku itakuwa kama ilivyokuwa mwaka 1964 au 1984 au 1995 au 2000 au 2005; siku hazigandi, na wananchi wa Zanzibar kama watu huru wanawafundisha "jambo" wananchi wa Tanganyika kwa kuwa Tanganyika iliingizwa kwenye muungano ili kuimeza Zanzibar kwa vile Tanganyika haikuwekwa kwenye ramani isipokuwa Zanzibar ndiyo iliyowekwa.

  Nadhani umefika wakati sasa wa kutumia akili yenye satwa ya maamuzi makini na ya kimkakati; wapo waliyehusika kwa namna moja na au nyingine kuhakikisha kwamba Sudan Kusini inajitoa kwenye SUDAN KUBWA; na leo wote ni mashahidi kwamba kuna nchi mpya mbili zilizokuwa moja zinaitwa Sudan Kusini na Sudan Kaskazini - nchi moja ya Wakristo (wengi) na nchi nyingine ya Waislam (wengi). Je, hamuoni kwamba Zanzibar wana haki ya kuamua hatma yao? Na je, hamuoni kwamba Tanganyika ina haki ya kuamua hatma yao? Kwani ni nani aliyewaambia kwamba waliyeasisi muungano ni "miungu" na au "malaika" wenye asili ya watu na walichokifanya kilikuwa maagizo ya Mungu?! Tusijitoe fahamu na au akili ya kudhani kwamba watu wanaweza kudanganywa kwa muda wote na au nguvu zinaweza kutumika muda wote kuwatisha na kuwaogopesha watu wasidai uhuru na haki yao ya kujiamulia mambo yao!

  Tuache uzezeta wa akili; turuhusu uhuru na haki ya watu kujiamulia mambo yao wenyewe hata kama kwa upande mmoja ni uchungu na au fedheha. Uhuru, haki na wajibu wa wananchi ni kuamua kwa jinsi wanavyoona wao inafaa! Na hakuna katika historia ya binadamu kwamba aina ya utawala na au uongozi wa kisiasa ulilazimisha jinsi ya kutawala na ukabaki milele - kila utawala ni wenye kwisha na kunapotokea "mapinduzi ya fikra" hapo ndipo panapokuwa chemchemi ya harakati za ujenzi mpya wa nchi mpya na watu wenye mtazamo mpya wa kiakili na kifalsafa. Uhuru kwanza; ubabe na vita vya kuua haki ya kuwa huru baadaye! Huwezi kuwalazimisha binadamu wenye akili timamu ya utambuzi kama unavyoweza kuwalazimisha punda kubeba mizigo huku wakitandikwa bakora na kusukumwa alimuradi mzigo ufike! Punda; hata kama ni mnyama (hayawani) asiyejitambua, akichoka hugoma na lazima abwage mizigo na mateke ayarushe hewani kuonyesha hasira zake....inasemekana kwamba hata wakati mwingine, punda akichoka kuburuzwa na kutandikwa baokora huku amemebeshwa mizigo mizito hurusha mateke na hata kumjeruhi mmiliki. Huyu si binadamu mwenye akili ya utambuzi; nadhani serikali ya JMT na ile ya SUK (ndani ya SMZ) wasiwafanye Wazanzibari na Watanganyika kama "punda" wa kuwalazimisha vile wao (SJMT na SMZ na CCM) wanavyotaka...wafuate utashi wa wananchi unavyotaka; nadhani muafaka ni: KURA YA MAONI JUU YA MUUNGANO! Hili ndio suluhisho la kidemorasia; kama CCM imeamua twende kwa njia ya demokrasia haina budi kukubali "matokeo" ya demokrasia hata kama ni machungu kwa chama hicho!
   
Loading...