Elections 2015 Picha: Tulichokishuhudia katika mapokezi ya Magufuli Jijini Mwanza, upinzani unafutika

MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,536
2,264
Kwa kile ambacho tumekishuhudia Jijini Mwanza kinatoa ujumbe unaosema, Majimbo ambayo yako chini ya CHADEMA katika mikoa ya Kanda ya Ziwa yako mbioni kurudi CCM. Sina haja ya kuongelea Urais wa Tanzania kwa sababu Magufuli anasubiri kuapishwa tu.

SHUGHULI mbalimbali katika maeneo ya Barabara Kuu itokayo Uwanja wa Ndege wa Mwanza hadi mjini katikati, jana zilisimama kwa muda wa saa moja, huku wakazi wa jiji hilo wakishiriki kumpokea mgombea mteule wa urais wa CCM, Dk John Magufuli.

Mapokezi hayo ambayo yameacha historia ya pekee jijini hapa, yalianzia katika uwanja huo saa 8:00 mchana alipowasili akiongozana na mkewe Janeth Magufuli, Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Rajabu Luhavi.

Uwanjani, mgombea huyo alipokewa na mamia ya wana CCM, viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali kutoka mkoani hapa na mikoa ya jirani ya Kanda ya Ziwa, wakiwemo Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani na Naibu Waziri Nishati na Madini, Charles Kitwanga.

Msafara wa Dk Magufuli ukiongozwa na pikipiki zaidi ya 150 ulianza safari kwenda mjini kati ya saa nane mchana, ambapo maelfu ya wananchi waliojipanga katika maeneo mbalimbali katika barabara hiyo wakiwemo akina mama, watoto na vijana, wakijitokeza kumlaki na kumpungia kwa khanga za CCM na matawi ya miti.

Maeneo hayo ni pamoja na Ilemela, Butuja, Sabasaba, Iloganzala, Pasiansi, Nyamanoro, Ghana na Mission ambapo alilazimika kusimama kwa muda katika baadhi ya maeneo hayo na kusalimia wananchi baada ya kumzuia kwa nguvu wakimtaka awasalimie.

Kote huko wananchi walikuwa wakimshangilia kwa makofi, vigelegele na vifijo wakimuita ‘Jembe, Jembe' huku baadhi wakipaza sauti na kumwambia "Wewe ndiye Rais wetu, wengine wanajisumbua."

Kutokana na muda mwingi kutumia barabarani akitokea uwanja wa ndege, ilibidi mkutano wake kwenye viwanja vya Furahisha uahirishwe kutokana na kukosekana kwa muda wa kutosha.

Wananchi wengi wamesikika wakisema CCM kwa sasa inarudi kwa wenyewe ambao ni wakulima na wafanyakazi na kwa maana hii, wako tayari kumpa ushirikiano Magufuli kwa kuchagua wabunge wachapa kazi kama yeye ili wamsaidie kuunda serikali yenye kuwajika kwa wananchi.


























































Magufuli akisaini kitabu cha wageni katika ofisi za CCM Mkoa wa Mwanza.

 
Nilikuwa nasubiri huu umbea..nimeangalia ITV mpiga picture kajitahidi kuchukua usawa wa watu ila alikuwa napaotea km wewe hapa jamaa hakuwa hata na watu wa wenye ktk mkutano wa kawaida jimboni.Sidhani km kuna mbunge wa CHADEMA anaweza kuwa na watu kidogo km magufuli tena ktk ukanda wake.
 
Wala haujakosea hao ndo miongoni mwa wanachama 6mln wa ccm.Kumbuka wapiga kura nchi nzima ni 22mln, sasa Fanya hesabu mwenyewe kabla ya kushangilia.
 
Wala haujakosea hao ndo miongoni mwa wanachama 6mln wa ccm.Kumbuka wapiga kura nchi nzima ni 22mln, sasa Fanya hesabu mwenyewe kabla ya kushangilia.
jizo picture tafuta yenye watu wengi kabisa kadiria umbali wa camera km wewe ni mpiga picture halfu angalia mwisho wa hizo picture pande zote utaona zimeishia palipoishia watu,na jaribu ziunganisha kuna baadhi zinaweza kupapande zote za mpiga picture.Jiulize watu wa usalama ,waandishi na wapita njia ni wangapi?
 
Rais wetu mpendwa wa awamu ya 5 ndugu JM mungu amjalie afya njema, busara ili atuongoze vyema.
Busara hakujaliwa ,na pengine hakuwahi omba kwa Mungu wake kwani kafika hapo kwa kiherehere(Nyapara) ,Sasa Mungu yupi kigeugeu amjalie sasa hivi?
 
Mcheza kwao hutuzwa.. ! Magufuli asiende sana mwanza ataonekana ni mbaguzi,...bora angeanzia nyanda za juu kusini.
 
Nilikuwa nasubiri huu umbea..nimeangalia ITV mpiga picture kajitahidi kuchukua usawa wa watu ila alikuwa napaotea km wewe hapa jamaa hakuwa hata na watu wa wenye ktk mkutano wa kawaida jimboni.Sidhani km kuna mbunge wa CDM anaweza kuwa na watu kidogo km magufuli tena ktk ukanda wake.

Wapinzani ndiyo wanafiki, hizi picha hazichafanyiwa editing, ni natural na pure! Magufuli ndiyo rais. Sina habari na wabunge maana wengi wa ccm ni mbumbu, ila kwa rais ndiyo huyo
 
Umeshasema Wafuasi Wa Ccm Sasa Wewe Ulitalajia Wafuasi Wa Ccm Wampokee Slaa? Na Hao Wanaccm Wapo Myaka Yote Na Sasa Hivi Wanapungua Kwa Kasi Wengine Wanakufa Wengine Wanahama, Huku Vijana Wanaofikisha Miaka 18 Wote Wanaibukia Chadema, Je! Mwaka Huu Mtapona?
 
Wewe Ni FARAsi wa Sengerema. Hii ni aibu uloweka hapa. Mkajifanya kufunga barabara ili shughuri zikwame watu wakose pa kwenda. Hebu tafuta Picha ya lowasa siku ile kaenda pale Gandhi hall kisha linganisha na za huyu msagajiwe.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom