PICHA: Tanzania yafikia 16% ujenzi wa reli ya kisasa

rail.jpg


kulitakiwa kuwe na two railways kama hivi ya kwenda na kurudi... yani kama mradi wa BRT ulivyo... ili kuleta ufanisi ktk usafirishaji.... hawa wanajenga njia moja hili lina pelekea niseme ni ushamba tena na tena....
 
juzi kati heche aliuliza wamuonyeshe hata mita moja ni wapi wamejenga hio sgr, mi nilidhani mawaziri wangeinuka na kuomba miongozo, ila mpaka mwisho wa hotuba yake sikusikia akijibiwa!
 
Mbona sioni nguzo za umeme. Hii standard gauge mbona kama ishaanza kuzeeka au ndo mmbeiba mataruma kwenye reli yetu ya zamani
 
1473509127391.jpg


tunapo amua kuboresha miundo mbinu tuwekeze kweli kweli... sio ubabaishaji kama tuna jaribu... tujenge tumalize katika sekta hii... tukiondoka kwenda sekta nyingine tuna hama jumla... kwakuwa uchumi wetu sio mzuri kukizi yote lakini sio kujenga ktk viwango hafifu

1 way hiyo hiyo kwenda hiyo hiyo kurudi... sikubaliani nalo hata kama ndio tuna anza... tunge wekeza kweli tujenge kweli sio kujenga mifano kama BRT ya kuchora ya ndugu zetu wakenya
 
lakini hii SGR mbona njia moja alafu ipo kama kishamba sana???
Mkuu na Mimi nilikua najiuliza hili swali..Labda kama Mleta Mada ameweka picha tofauti..Lakini Kama Mradi wenyewe ndiyo huu basi Wasitambe ni Mradi wa Kisasa..Hii ni ya Kishamba.
 
View attachment 811900

kulitakiwa kuwe na two railways kama hivi ya kwenda na kurudi... yani kama mradi wa BRT ulivyo... ili kuleta ufanisi ktk usafirishaji.... hawa wanajenga njia moja hili lina pelekea niseme ni ushamba tena na tena....

Unafananisha SGR na BRT hivi ni vitu viwili tofauti,halafu Rail track mbili zinakuwepo maeneo maalum tu mfano kwenye stesheni nk .Reli yoyote si kama bara bara ambayo kila mtu anatumia kuanzia mwenda kwa miguu mpaka mwenye Vitz.
Hata kuko kwa wenzetu walioendelea hawawezi kuweka reli mbili zilizo paralel kuanzia mwanzo wa reli hadi mwisho
 
Unafananisha SGR na BRT hivi ni vitu viwili tofauti,halafu Rail track mbili zinakuwepo maeneo maalum tu mfano kwenye stesheni nk .Reli yoyote si kama bara bara ambayo kila mtu anatumia kuanzia mwenda kwa miguu mpaka mwenye Vitz.
Hata kuko kwa wenzetu walioendelea hawawezi kuweka reli mbili zilizo paralel kuanzia mwanzo wa reli hadi mwisho
ni vitu viwili tofauti lakini vina endana... wapo walioweka reli mbili ya kwenda na kurudi... sasa sijui wewe una zungumzia wenzenu wa wapi??? labda wakenya...; kwenye stesheni kuna kuwa na idadi ya track mbili na kuendelea ina tegemea na ukubwa wa stesheni husika...
 
juzi kati heche aliuliza wamuonyeshe hata mita moja ni wapi wamejenga hio sgr, mi nilidhani mawaziri wangeinuka na kuomba miongozo, ila mpaka mwisho wa hotuba yake sikusikia akijibiwa!

Siyo kila mpayukaji unamjibu. Kumbuka ule usemi usemao kichaa akichukua nguo zako wakati unaoga mtoni.......
 
Ujenzi wa awamu ya kwanza wa reli ya kisasa (Standard Gorge) umefikia asilimia 16 na unatarajiwa kukamilika ndani ya miezi 30 ifikapo Novemba 2019.
Reli hiyo ya kisasa itakuwa ya treni yenye kasi ya kilomita 160 kwa saa na uendeshaji wake utatumia umeme au mafuta.



Akizungumza leo Julai 17 wakati wa ziara ya Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Mkuu wa Mipango (Planning Chief) wa kampuni ya Yapi Merkezi, Enis Eryilmaz amesema kipande cha Dar - Morogoro chenye kilomita 300 kitakuwa na vituo sita ambavyo ni Dar, Pugu, Soga, Ruvu, Ngerengere na Morogoro.
"Tumejipanga kumaliza mradi huu ndani ya wakati, tunatumaini tutasherehekea uzinduzi wake Novemba 2019," amesema mtaalamu huyo.



Eryilmaz amesema wamekuwa wanafanya kazi usiku na mchana lakini changamoto kubwa tuliyokabiliana nayo ni mvua nyingi zinaponyesha.
Amesisitiza kwamba kampuni ya Yapi Merkezi imeajiri watu 4000, kati yao Watanzania ni asilimia 90. Amesema ushiriki wao ni mzuri na wengi wanafanya kazi vizuri.



"Tunajitahidi kufanya kazi bega kwa bega na Watanzania ili tukiondoka waweze kuendesha mradi huu na kufanya matengenezo mengine," amesema.
Amebainisha kwamba ifikapo Agosti, mwaka huu wataanza kulaza mataluma ya reli kwenye baadhi ya maeneo wanayojenga.



Meneja mradi msaidizi kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Masanja amesema reli hiyo itakuwa na kituo cha kupoza umeme kila baada ya kilomita 50 na Shirika la Umeme (Tanesco) litaweka umeme maalumu kwa ajili ya reli hiyo.



Amesema Dar es Salaam itakuwa na treni maalumu kwa abiria na watajenga kituo kikubwa Pugu ambacho kitakuwa kinapakia abiria wa Dar es Salaam na waendao mikoani.



Awali akizungumza na wakandarasi hao, mwenyekiti wa ERB, Profesa Ninatubu Lema amewaomba kuchukua wakandarasi wanafunzi kwa ajili ya kujifunza kwa vitendo mbinu na teknolojia mbalimbali za uhandisi.



Amesema mradi wa SGR ni mkubwa na kwa nchi kama Tanzania, hutokea mara moja ndani ya miaka 100.
"Tumefurahi kuona kazi inafanyika kwa umakini mkubwa wa kihandisi na wana vifaa vya kisasa. Pia, tumefurahi kuona watanzania wanashirikishwa lakini kwa level ya wahandisi bado wako wachache," amesema Profesa Lem.


My take : Watapata taabu sana !View attachment 811891
Hii sio picha ya reli mpya, usidanganye
 
Ngoja tusubiri mradi ukamilike na uanze kufanya kazi, maana hii miradi inayoanzishwa kisiasa huwa ina matatizo yake. Maana hadi sasa sielewi tunajenga kwa fedha zetu kutoka hazina au kwa mkopo.
Mkopo wa uturuki, na Jana hela yao imedepreciate sana kwa asilimia 12, kwa hiyo Malipo ya interest yanatufilisi kishenzi
 
Back
Top Bottom