PICHA: STARS ILIVYOIPA KIPIGO KITAKATIFU SOMALIA yaenda ROBO FAINALI NGASSA AVUNJA REKODI

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,780

Saturday, December 1, 2012

STARS YAIPA KIPIGO KITAKATIFU SOMALI, YAENDA ROBO FAINALI, NGASSA AVUNJA REKODI YA MABAO, BOCCO MOTO
Kikosi cha Bara, Kilimanjaro Stars kilichofuzu kuingia Robo Fainali ya michuano ya CECAFA Tusker Challenge, baada ya kuilaza Burundi mabao 7-0 katika mchezo uliofanyika kwenye Uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda leo.

Ngassa baada ya kufunga la kwanza

Salum Abubakar akimiliki mpira mbele ya kiungo wa Somalia

Bocco akipiga kichwa mpira kwenye lango la Somalia

Kapombe akifanya kazi yake

Ngassa akimiliki mpira mbele ya beki wa Somalia

Kipa wa Somalia akiokoa moja ya hatari langoni mwake

Kocha Poulsen

Wachezaji wa aStars Mwinyi Kazimoto kulia na Amir Maftah wakiwa na rafiki yao jukwaani

Amri Kiemba akimpongeza Ngassa kufunga
Kwa picha zaidi bofya read more

John Bocco akimburuza Msomali

Bocco akifanya vitu, angalia miguu

Bocco anapongezwa na wenzake baada ya kufunga

Bocco anamuacha mtu

Amri Kiemba kulia

Bocco mawindoni

Yondan anaokoa
Mrisho na mpira wake baada ya kufunga mabao matano

Na Mahmoud Zubeiry, Kampala

TANZANIA Bara, Kilimanjaro Stars imefuzu kuingia Robo Fainali ya michuano ya CECAFA Challenge, baada ya kuilaza Burundi mabao 7-0 katika mchezo uliofanyikakwenye Uwanja wa Lugogo mjini hapa.

Matokeo hayo yanaifanya Bara itimize pointi sita baada ya kucheza mechi tatu na sasa, wakishinda mbili na kufungwa moja.

Stars, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager leo ilionyesha kandanda safi na kusisimua mashabiki wa Tanzania waliokuja kuoiunga mkono hapa, akiwemo Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Alhaj Juma Nkamia.

Iliwachukua sekunde 48 tu Stars kupata bao la kwanza, kupitia kwa mshambuliaji wa Simba SC, inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premum Lager pia, Mrisho Khlfan Ngassa aliyewazidi ujanja mabeki wa Somalia.

Kabla hawajakaa vizuri, Somalia walipachikwa bao la pili, dakika ya 23 lililofungwa na Ngassa tena, aliyeunganisha kona nzuri ya Issa na Rashid.

John Bocco ‘Adebayor' alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo na la tatu kwake katika mashindano haya dakika ya 26 akiunganisha kwa kichwa krosi ya Issa Rashid kutoka wingi ya kushoto.

Bocco tena aliwainua vitini mashabiki wa Tanzania kwa kufunga bao la nne kwa kichwa, akiunganisha krosi ya Ngassa dakika ya 41.

Ngassa alifunga bao la tatu katika mchezo wa leo dakika ya 44 na la tano kwa Stars baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa Hussein Abdallah kufuatia shuti kali la Salum Abubakar ‘Sure Boy Jr.'

Somalia ilipata pigo dakika ya 30, baada ya kipa wake namba moja, Mohamed Abdullah kuumia baada ya kugongana na Bocco na kutoka, nafasi yake ikichukuliwa na Hussein Abdallah.

Kipindi cha pili Stars walirejea na moto wao na tena na kufanikiwa kupata mabao mawili zaidi yaliyotiwa kimiani na Ngassa yote dakika za 73 pasi ya Erasto Nyoni na 74 pasi ya Ramadhani Sinago ‘Messi'.

Kwa kufunga mabao matano, Ngassa sasa ameingia kwenye mbio za kaiti cha dhahabu akikwa anaongoza, akifuatiwa na Bocco ambaye ana manne hivi sasa.

Kocha wa Stars, Mdenmark Kim Pouslen baada ya mchezo huo, alisema aliwapongeza vijana wake kwamba wamejitahidi kucheza vizuri na akasifu pia hali nzuri ya Uwanja wa Lugogo kuwa ilichangia ushindi huo.

Mbunge Nkamia alisema kwamba amevutiwa na soka ya vijana leo na anaamini wana uwezo wa kurejea na Kombe nyumbani. Nkamia aliwapongeza wadhamini wa Stars kwa kuchangia mafanikio ya timu hiyo tangu waanze kuidhamini na akaomba Watanzania zaidi wajitokeze mjini hapa kuisapiti timu hiyo.

Waandishi wa Habari waliopo mjini hapa pia wamevutiwa mno na kiwango cha timu hiyo na kusema wana wana imani itafika mbali.

Wallace Karia, Mjume wa Kamati ya Utendaji ya TFF aliye hapa Uganda amesema amefurahishwa na kiwango cha timu na anaamini itafika mbali.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, wadhamini wa Kilimanjaro Stars, George Kavishe ametuma salamu za pongezi kwa ushindi wa leo na mafanikio ya kutinga Robo Fainali na kusema anatakia mafanikio zaidi timu hiyo.

Katika mchezo wa leo, kikosi cha Stars kilikuwa; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Kevin Yondan/Ramadhani Singano, Shaaban Nditi, Mrisho Ngassa, Salum Abubakar, John Bocco/Christopher Edrwad, Frank Domayo/Athumani Iddi na Amri Kiemba.

Somalia; Mohalim Abdullahi/Hussein Abdallah dk30, Ali Mohamed, Said Mahamud, Ali Dadir, Sadaq Abdikadir, Mohamed Salah, Abdikarim Abubakar, Abdallah Mohamed/Hamza Mukhtar, Ahmed Abdikadir Dahir/Muhad Hajji na Ali Ahmed Ali.

Katika mchezo mwingine uliopigwa kwenye Uwanja wa Nankurunkuru, Burundi ilishinda 1-0 bao hivyo kuongoza Kundi B baada ya kufikisha pointi tisa.


Habari na picha kwa hisani ya Bin Zubery Blog


 

mzabzab

JF-Expert Member
Aug 18, 2011
21,172
27,944
tumewafumania wachovu hao....ni sawa na mtu mwenye afya akajipime nguvu na mgonjwa kitandani....mbona burundi walitutoa kamasi...na rwanda wanatutoa.
 

Mentor

JF-Expert Member
Oct 14, 2008
20,343
23,814
Kimbembe ni Burundi na Uganda bana...hao tukiwafunga kombe letu.
 

gwino

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
335
47
hata kama somalia ni kibonde wanastahili pongezi goli 7 si mchezo.
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,780
Tanzania kila sekta nimbovu hawako makini sasa tazama hii habari nngu007 fafanua au nawewe umekopi bila yakusoma ukaleta tambuu na tumbaku hapa?

Bwana Kana-Ka-Nsungu Mimi Sio Mhariri wa Gazeti Hilo au HABARI; Sasa Unasema nisingeiweka Sababu ya MAKOSA ya Mwandishi wa HABARI HII?

Jamii Forums ni MAHALI pa kutoa HOJA either UNAZOZIPENDA au USIZOZIPENDA; Au HOJA unapenda kuona USHAURI wa Wana JAMII...

Ndio hii ni haki yako KUCHUNGUZA hiyo habari na KUONA KOSA; Lakini hiyo isiwe sababu ya MIMI kuipost; PENZI LANGU la HII HABARI haikuwa MWANDISHI na MAKOSA yake; PENZI LANGU la hii HOJA ilikuwa ni JINSI TIMU ya TANGANYIKA ilivyopendeza na MAVAZI yake; Sikujali HABARI sababu nilishajua ILICHEZA na TIMU gani na IMEPANGWA kucheza na TIMU GANI ROBO FAINALI...

Kwahiyo SIKULETA TAMBUU na TUMBAKU; Nimeweka KILICHONIFURAHISHA na KUTAKA KUSHARE na Wana Jamii

I'm FREE to EXPRESS MY FEELINGS and MY THOUGTHS and I BELIEVE you are FREE as well but PLEASE don't CRITIZISE ME for the ARTICLE...
 
Oct 10, 2012
32
1
Kwani kuna la kujipongeza kufungwa na BURUNDI MOJA BILA THEN kuwafunga SOMALI 7 _ O , Inaonyesha sisi bado sana na ngojeni muone wananyotufanya WARWANDA KWVILE SIE MBUMBU.
 

gutierez

JF-Expert Member
May 14, 2010
1,246
158
Uwanja kama wa shule ya sekondari vile!
tatizo la bara letu afrika mechi inachezwa leo uwanja huo na kesho pia uwanja huo,ulaya kamwe hauoni hivyo,angalia mfano ac milan na inter milan zinatumia uwanja 1 san siro giusseppe meazza,mfano tuchukulie ktk uefa zimeshika nafasi ya 2 au ya kwanza ktk makundi yote wote,kwahiyo ina maana ktk mtoano kama wameshika nafasi ya 2 wataanzia nyumbani ya kwanza ugenini,sasa kwa kuwa zinashare uwanja,hata 1 akicheza j4 san siro mwingine pale san siro ni next wiki sio j5,ndio maana hata community charity cup man city vs chelsea ilichezwa villa park jijini birmingham 7bu jana yake kulikuwa na final soka olimpiki mexico vs brazil pale wembley,uwanja unapewa muda uwekwe sawa sio jana na leo mfululizo,hongera Mrisho Ngasa kaza buti huenda si ajabu taratibu unavunja na wewe rekodi ya Messi japo kwe2 bado soka watu hawatufuatilii kwa sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

1 Reactions
Reply
Top Bottom