Picha: Spika Makinda awasili mjini Quebec, Canada kuhudhuria mkutano wa 127 wa chama cha mabunge

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
SUNDAY, OCTOBER 21, 2012


Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika uwanja wa ndege mjini Quebec, Canada tayari kwa kuhudhuria mkutano wa 127 wa chama cha Mabunge Duniani (IPU) unaotarajia kufunguliwa rasmi kesho tarehe 21 Oktoba, 2012 na kumalizika 26 Oktoba . Makinda ameongoja ujumbe wa wabunge wanne kutoka Tanzania, ambapo zaidi ya maspika wa nchi 150 duniani wakiongoza ujumbe wa wabunge kutoka Nchi zao watashiriki mkutano huo.


Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiteta jambo kuhusu maandalizi ya awali ya mkutano na afisa kutoka Bunge la Canada mara alipopokelewa baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege mjini Canada kuhudhuria mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani. Kulia ni Mhe. David Kafulila na Mhe. Hamad Rashid waliongozana na Mhe. Spika katika Mkutano huo nchini Canada.

Afisa wa Ubalozi wa Tanzania nchini Canada Joseph Sokoine akimkabidhi Mhe. Spika taarifa ya maandalizi ya mkutano huo pamoja na hali ya kisiasa ilivyo nchini Canada baada ya kuwasili kuhudhuria Mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU).Picha na Owen Mwandumbya



SUNDAY, OCTOBER 21, 2012 ~ COPYRIGHT: MICHUZI BLOG









 
Huyu MAMA yetu hataki kurudi BONGO? Kuna Maandamana na pia UCHAGUZI wa UWT? Au alipapenda INDIA na kusingizia UGONJWA? Sasa huyooo CANADA

NI SPEAKER MTEMBEZI KULIKO WOTE TULIONAO...

Angalia Maspeaker wa Marekani au UINGEREZA au KENYA sioni Wakisafiri kama WA BONGO ni hizo PESA za GAS zinatuwasha????
 
Joseph Sokoine ni MWINGINE; Anagoma kurudi NYUMBANI... Muda wake uliisha zamani akiwa US kwa miaka 6; lakini alipoambiwa ARUDI NYUMBANI wakati huo hawajateua BALOZI CANADA baada ya wa CANADA kwenda UK; Yeye akasema kuna nafasi CANADA akaenda... Akahamisha na FAMILIA... hiyo ni MIAKA 3 au 4 iliyopita...

ANA NGUVU haswa Mmmm na anapenda toto's huyooooooo
 

Kwenye KUNDI; HAMAD RASHID - Hakosekani; KAFULILA ina MAANA na ZITTO KABWE yumo kwenye hilo KUNDI...
 
mama anakula bata duh, visa ya canada kaipata akiwa india, pesa za walipa kodi hizo
 
badala arudi kwenye swala la mifuko ya jamii, ye anazurura. Mbururaaa! Mbururaah!
 
Huyo ni serengeti boy au ni nani jamani? n auliza tu sina ugomvi na mtu
 
Reporter hajui hata anachoandika ..

... baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege mjini Canada kuhudhuria mkutano wa 127 wa Chama cha Mabunge Duniani.

Huo mji siuelewi!

... Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika uwanja wa ndege mjini Quebec, Canada tayari

Montreal? Maana Quebec ni mji mdogo ktk jimbo la Quebec ambao hauna uwanja wa ndege wa kimataifa.
 
Back
Top Bottom