PICHA: SPIKA aongoza Viongozi Nchini kuomboleza Msiba wa Mzee RAJANI, UPANGA - VIONGOZI wengi WA CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
Monday, November 26, 2012

SPIKA ANNE MAKINDA AONGOZA WAOMBOLEZAJI MSIBA WA MZEE RAJANI, UPANGA JIJINI DAR




1.JPG

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwasili nyumbani kwa marehemu mzee Shree Jayantilal Pragji Rajani, maarufu kama Mzee Rajani kuhani Msiba. Mzee Rajani alifariki Jumatano Novemba 21, 2012 mjini London alikokuwa amelazwa.
2.JPG



Spika Anne Makinda akisaini kitabu cha waombolezaji.
3..JPG



Mzee Pius Msekwa na Anne Abdallah wakisaini kitabu cha waombolezaji.
Kwa picha zaidi bofya read more
10.JPG

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiongoza waombolezaji kuweka maua katika mwili wa Mzee Rajani ikiwa ni ishara ya kutoa heshma za mwisho kwa marehemu wakati wa kuaga mwili wa marehemu MzeeRajani nyumbani kwake Upanga.
11.JPG

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM bara Mzee Philip Mangula wakitoa heshima
zao za mwisho kwa mwili wa mzee Rajani.
9.JPG

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mzee Salim Ahmed Salim.
5.JPG

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mmoja wa Waombolezaji, katikati ni Rostam Azizi.

8.JPG

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mzee Kingunge.
6.JPG



Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda Akisalimiana na Mama Anna Mkapa.
7.JPG

Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akisalimiana na Mzee Pius Msekwa.(Picha zote na Owen Mwandumbya, Bunge)




 
Raha haswa... VIONGOZI kibao wa CCM; Hapo UNAJUA kweli MZEE RAJANI aliisaidia sana CCM
 
R.i.p mzee rajani lakini pamoja ni msiba ngoja niseme nilichokiona kwa spika kila msiba naona uwa anakanga iyo iyo tu kulikoni mnaomchagulia kuvaa spika wetu,lingine kumbe lostam yupo "njii" hii nimemnukuu mzee wa kilalacha.
 
Mbona makada wa CCM wamejaa hapo?

Marehemu Rajani alikuwa nani hasa kisiasa?

Huenda ukakuta alikuwa official sponser wa magamba, maana hawa ndugu zetu japo ni watanzania lakini huwa hawajiamini kabisa katika kuishi kwao hapa Tz.
 
R.i.p mzee rajani lakini pamoja ni msiba ngoja niseme nilichokiona kwa spika kila msiba naona uwa anakanga iyo iyo tu kulikoni mnaomchagulia kuvaa spika wetu,lingine kumbe lostam yupo "njii" hii nimemnukuu mzee wa kilalacha.
Mkuu kuna mambo ya kamati za ufundi.
Kwa tunaomjua huyu mama hatushangai sana.

Inasemekana huwa ni mtu asiyejiamini sana na hivyo yuko defensive katika angle zote.
 
Mkuu kuna mambo ya kamati za ufundi.
Kwa tunaomjua huyu mama hatushangai sana.

Inasemekana huwa ni mtu asiyejiamini sana na hivyo yuko defensive katika angle zote.

apo sasa nimeelewa mkuu
 
Msibani kidogo kajihuzuni ni muhimu. mbona Naona watu wanafuraha sana?!
Wanakunja uso mbele ya mwili wa marehem tu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom