PICHA: Sababu Hamis Kigwangalla anatetea chanjo ya Corona Virus. Akutana Na Bill Gates Na Jasusi Kutoka Israeli

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
Habari Wana Jamvi,

Ni kawaida kwa viongozi wa taifa letu kuwa vigeugeu katika misimamo yao na ukakasi katika matamko yao. Kiburi na majivuni yamekua kama nguo juu ya tabia zao. Pengine ni udhaifu waliokua nao na unaotokana na kutokua na elimu katika ya uongozi wa umma.

Kwa upande wetu raia, hali hio imepelekea kukosa imani kwa viongozi wetu wa umma. Lakini mara kadhaa, viongozi wa juu wameonesha wazi wazi kutokujali kabisa mitazamo na malalamiko yetu raia kuhusiana na viongozi tunaoteuliwa kuja kutuongoza (Serikalini). Jambo ambalo limepelekea mgawanyiko kwetu raia, na kuzaa makundi mawili - Waungaji Mkono (Die Hard Fans) & Wapingaji (Die Hard Opponents).

Nirudi kwenye mada husika,

Hivi karibuni tumeshuhudia viongozi wengi (Karibu Wote Kuanzia Bungeni Na Serikali Kuu) wakigeuka na kukanyaga mitazamo na kauli zao. Si jambo geni nchi yetu kuwa na viongozi vigeugeu.

Mfano, Dr. Hamis Kigwangalla, ambae awali alivyokua Waziri alikua ni muungaji mkono wa kila kitu, ila mara baada ya kuwekwa pembeni amekua akigeuka mitazamo na kauli zake. Kauli juu ya mitazamo yake ambayo alipaswa kusema kipindi yeye ni Waziri, hakuzisema.

Swala la Corona,

Kipindi yeye Waziri ambae alikua karibu sana na kiongozi wa nchi, hakuwahi kusema kuhusu serikali kuangalia upande wa pili (Kufanya Utafiti) kukubali chanjo. Ila sasa baada ya kuwekwa pembeni katika jopo la mawaziri ndio ameanza kuonesha katika mitandao (Uwanja Wake Wa Mapambano) kugeuka mitazamo aliokua nayo awali, kupelekea kuishauri serikali kuangalia uwezekano wa kuchukua chanjo za Corona.

Kuna taarifa na picha sasa zinaenea mitandaoni (Social Media & Online News Platforms) zikimuonesha Dr. Hamis Kigwangalla akikutana kisiri siri na Bill Gates (Mmiliki Wa Baadhi Ya Chanjo Za Corona) na Jasusi kutoka Israel Shlomo Carmel.

Bill Gates ni tajiri mkubwa duniani ambae anatambulika kwa kutumia taasisi yake ya Bill & Melinda Gates kwa nguvu zote alizokua nazo kushawishi dunia kukubali chanjo dhidi ya Corona. Kwa mantiki, yeye ni miongoni mwa watu wanaomiliki Haki Miliki Ya Chanjo Ya Corona.

Jasusi Shlomo Carmel ni miongoni mwa majasusi hatari Israel (Elite Israel Paratroopers & MOSAD) ambae ana historia ya kutukuka katika utendaji wake kazi - Moja ya kazi aliowahi kufanya ni Kuokoa WaIsraeli 100 waliokua wametekwa nyara katika Uwanja Wa Ndege Wa Kimataifa Entebe, nchini Uganda mwaka 1976.

Hamis Kigwangalla ni mbunge wa Nzega, ambae hivi karibuni alianza kutetea matumizi ya chanjo za Corona, licha ya baadhi ya nchi jirani kutaka kuziteketeza baada ya kuona kasoro zake, mfano Malawi, DRC n.k.

Maamuzi yake ya kutetea matumizi hayo ya chanjo, yanatia ukakasi kwamba anapata ushawishi kutokana na hao watu wawili wakubwa aliokutana na kuwasiliana nao (Pengine anaendelea kukutana nao kisirisiri).

Licha ya CAG Kachere kutoa report yake ya ukaguzi wa serikali kubainisha Wizara Ya Maliasili (Kipindi Cha Yeye Kuwa Waziri) kuwa na matumizi mabaya na upotevu wa mabilioni ya hela za wananchi walipa kodi, serikali siku ya leo imeenda mbele zaidi na kutamka kwamba alikanyaga na kusigina sheria kipindi yeye ni Waziri (Kwa kufungia lesseni za vitalu halali kwa wawekezaji) na kuamua kurudisha lesseni hizo kwa wamiliki wa vitalu kwa wamiliki hao.

Sio mara ya kwanza kwa Hamis Kigwangalla kuingia matatani kwa kashfa wakati yupo katika Wizara Ya Maliasili Na Utalii. Aliwahi kuingia matatani kutokana na ugomvi aliokua nao baina yake na Katibu Wake Prof Mkenda kwa matumizi mabaya wizarani.


Swala la yeye kushawishi Tanzania kukubali Chanjo za Corona wakati baadhi ya nchi kutamka kwamba hazifai na wanataka kuziteketeza, ni muendelezo wake wa kutaka kuitia hasara ya mabilioni (Kununua Chanjo hizo) kwa Taifa letu pendwa, Tanzania Mama.

Wito wangu,

Raia tusimame imara na Rais Mama Samia kwa Maadui Wa Taifa Letu. Kama taifa tusiwabeze wapinzani na kuwaona ni maadui walio nje ya serikali na bunge, kwani maadui hata ndani ya chama tawala, serikalini na bungeni bado wapo.

Adui wa nje ya familia si hatari kama adui wa ndani ya familia, tena ni hatari kweli kweli kwani anaweza akateketeza familia nzima kwa muda mfupi.

Picha husika.



Kigwa%20Secret%20Meetings.jpg
JamiiForums36193241.jpg
[/b]
 
Hii nchi hii, watu kuendekeza matumbo yao wametufikisha pabaya, ila sasa huko tunapoelekea watatufikisha kuzimu kabisa.

Nawasubiri waliobeza na kukashifu kwenye thread hii kuona watakacho sema na huku. Waliomba video Magufuli akitamka Tanzania tutapewa asilimia nyingi zaidi ya Uganda (Museven amekubali na ametupa 60%) kwenye bomba la mafuta, ila mwisho tumepewa 5%, tumewapa hio video alipokua na Rais Museven kuthibitisha, wakakimbia na kukaa kimya.

Mimi na watapia tumbo (Watembea Upesi Ili Kinyesi Kisigande) wa taifa letu mpaka kielewe JF, tutazaa pamoja, labda nipigwe BAN la maisha na mods.
 
Said Nassor bagaile ni mpiga dili.
Adui namba moja wa taifa. Alikua anaomba rushwa kwa wafanyabiashara wa vitalu, wakimnyima anaanzisha bifu na kuwafutia vibali bila kufuata sheria. Huyu wa kufungwa jela.

Sasa acha serikali iendelee kumfumbia macho, halafu aanze kutoa siri za ndani za serikali kwa Majasusi ndio labda serikali itapata akili.

Kuliko wanaowabeza na kuwatukana kina Tundu Lissu/Shangazi/Mange/Kigogo kwa kuwaita maadui wa taifa.
 
Back
Top Bottom