PICHA:rais kikwete akielekea dodoma kuhutubia bunge maalumu

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,277
8,836
ImageUploadedByJamiiForums1395323897.860265.jpg rais jk akiweka maandalizi ya hotuba yake kesho akiwa safarini kwenda dodoma leo!
 
Mungu ampe ujasiri wa kutetea lawama zote anazoelekezwa na akina Sendeka badala ya kumjibu/shambulia mzee Warioba na kwa kufanya hivo ataungwa mkono na wananchi wengi.
 
Naomba kwa niaba ya WAFANYAKAZI wote nchi hii, Jakaya wetu atangaze KESHO siku ya MAPUMZIKO ili tupate muda mzuri wa kumwona na KUMSIKILIZA. Mbona tulipumzika siku ile baada ya sherehe za Mapinduzi ambazo kumbe zilikuwa za NCHI nyingine?

Ikishindikana basi ahutubie BUNGE hili maalum saa mbili usiku kesho ili wengi wetu tuwe tumefika majumbani.
 
Mkuu nimesoma post ya Kennedy hapo chini kwamba unatudanganya. Hivi unapata faida gani mtu mzima kudanganya wenzio? Kwani ni lazima ulazimishe post??

Pumbaf nikudanganye ili iweje nyuzi zangu zote humu sio za utunzi ni vitu halisi na hii ni kweli tupu!
 
Hakuna chochote hapa picha ya zamani sana hii na hapa jukwaani ipo sana.

Unaona raha kupotosha eeh siku nyingi lini wewe jf una muda gani?uliona jukwaa gani watu waitafute?usiwe ka olesendeka wewe picha hii imepigwa leo
 
Mbona ndege ndani haifanani na ya Obama nilicha ya kulishwa nyasi ikanunuliwa?
 
Mkuu nimesoma post ya Kennedy hapo chini kwamba unatudanganya. Hivi unapata faida gani mtu mzima kudanganya wenzio? Kwani ni lazima ulazimishe post??

Kweli Urais hauna ubia wala muda ama sehemu ya kuchapa kazi. Wakati wowote na mahali popote ni sehemu ya kazi, kama inavyoonekana hapa ambako Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametulia ndani ya ndege akisafiri kutoka Dar es salaam kuelekea Dodoma huku akiifanyia kazi hotuba yake ambayo ataitoa katika Kikao cha Bunge Maalum la Katiba, Ijumaa, Machi 21, 2014.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amealikwa kuwa mgeni rasmi na kuhutubia Bunge Maalum la Katiba kwa mujibu wa Kanuni 7(1)g na Kanuni 75(1) la ya Kanuni za Bunge Maalum.PICHA NA IKULU.
 
Mbona ndege ndani haifanani na ya Obama nilicha ya kulishwa nyasi ikanunuliwa?

Seat ya rais kwenye jet yetu haina hadhi kabisa unless kuna chumba kingine....

Kama ndo hapo huwa anakaa hadi ulaya....mimi niko tayari kula nyasi tena tununue jet ya kisasa...
 
Naomba kwa niaba ya WAFANYAKAZI wote nchi hii, Jakaya wetu atangaze KESHO siku ya MAPUMZIKO ili tupate muda mzuri wa kumwona na KUMSIKILIZA. Mbona tulipumzika siku ile baada ya sherehe za Mapinduzi ambazo kumbe zilikuwa za NCHI nyingine?

Ikishindikana basi ahutubie BUNGE hili maalum saa mbili usiku kesho ili wengi wetu tuwe tumefika majumbani.
Mkuu fanya kazi kama hotuba ya raisi utaipata kwenye Website ya serikali, sometimes tujizoeshe kutafuta habari kwa kuperuzi mitandaoni kama ulivyojitutumua kuingia humu maana tangu runinga zije tumepoteza kabisa utamaduni wa kujisomea
 
Seat ya rais kwenye jet yetu haina hadhi kabisa unless kuna chumba kingine....

Kama ndo hapo huwa anakaa hadi ulaya....mimi niko tayari kula nyasi tena tununue jet ya kisasa...

Nakuunga mkono kiongozi, maana hapo pembeni alipokaa hiyo ni meza au kabati ama kitu gani sijui naona kama uchafu fulani hivi.........
 
Mbona ndege ndani haifanani na ya Obama nilicha ya kulishwa nyasi ikanunuliwa?

Hizo ndio 10% alizochukua Basil Mramba mwishowe akaishia Keko kunyea pipa!!! Siku hizi ukimuona hana hadhi tena na maradhi yamemtinga !!!
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom