Picha-Polisi wapiga mabomu ya machozi Arusha

mkongo

Member
Nov 21, 2009
19
9
IMG00933-20130618-1353.jpg IMG00935-20130618-1359.jpg IMG00937-20130618-1705.jpg IMG00938-20130618-1705.jpg IMG00939-20130618-1706.jpg IMG00941-20130618-1709.jpg IMG00942-20130618-1709.jpg IMG-20130618-WA0004.jpg IMG-20130618-WA0005.jpg
 
Tangu vita vya Kagera watu hawajaona vita kwa hiuo wamesahau ndiyo maana wanaitafuta vita kwa udi na uvumba. Waulizeni watu walokuwa Kagera ndipo mtajua madhara ya vita. Tena vita ya wenyewe kwa wenyewe ni mbaya zaidi iwa kuwa huwa haiishi. Jamani. Tusifike huko.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Wadau,
Nimekaa, nikatafakari juu ya taarifa inayohusu mlipuko huko Arusha na kujiuliza maswali haya bila jibu:
  1. Ni kwa nini Polisi waende kwenye mkutano wa hadhara (kama huo wa huko Arusha) huku wakiwa na silaha za moto?
  2. Je? Sheria za ulinzi na usalama hasa zile zinazowasimamia Polisi zinasemaje kuhusu ubebaji na utumiaji wao wa silaha za moto?
  3. Hata kama ni kwa kujihami na fujo za raia, yale maji ya kuwasha, risasi za plastic, virungu, n.k viko wapi mpaka watangulize silaha za moto?
  4. Hao viongozi wetu (Pinda, Kikwete, Lukuvi, n.k) ambao mara kwa mara wamekuwa wakiwakingia kifua hawa Polisi wanaoua raia mara kwa mara nao hawajui hizo sheria? Au wao ndio wanaowatuma? Mbona watu kama Pinda na Kikwete hawafananii kuwa na roho kama hizo? (Labda Lukuvi).
  5. .........? :shock:

Naomba mnisaidie kupata majibu ili roho yangu itulie kwenye msimamo mmoja! Ahsanteni.
 
Maswali yako ni mazuri ila ninadhani Mwigulu anaweza akawa na majibu sahihi.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Natamani maandamano ya nchi Zima kwa sasa sijui kwa nini viongozi wangu hawayaitishi maana tunayahitaji wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule
 
Nimekoswa risasi hapo karibu na kwenye maduka ya kwenda stand ndogo!!
Nilikuwa natokea ofcn kwangu mitaa ya stadium. Difender ikaja kwa kasi pasipo mimi kujua wakati navuka barabara kuelekea stand ndogo. Jamaa walikimbia na nilikuwa wa mwisho kukimbia.
Nilisikia sauti piga risasi huyo wa mwisho?! Kugeuka akawa anajiandaa kwa kushusha kioo na kuninyooshea bunduki.
Nikalala chini! Nikasikia sauti tena mfuate palepale?! Kunyanyua kichwa akawa anafungua mlango ashuke!
Nikanyanyuka na kuingia duka jirani na kujifungia!!
Wakaondoka??!
 
Tangu vita vya Kagera watu hawajaona vita kwa hiuo wamesahau ndiyo maana wanaitafuta vita kwa udi na uvumba. Waulizeni watu walokuwa Kagera ndipo mtajua madhara ya vita. Tena vita ya wenyewe kwa wenyewe ni mbaya zaidi iwa kuwa huwa haiishi. Jamani. Tusifike huko.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

CCM ndio ma-architect wa vita na vurugu hapa nchini, nenda Lumumba ukawaambie usilete unafiki JF
 
Polisi ni kama mbwa tu wanaoamrishwa kuuma!!! Mwenye mbwa ndiye anayefahamu kisa na mkasa wa mbwa wake kuuma! Mwenye mbwa yupo... Kikwete ndiye mratibu wa shughuli zote za mabomu makanisani na katika mikutano ya kisiasa pamoja na mauaji na utesaji unaoendelea sasa katika Tanzania!!!
 
Tangu vita vya Kagera watu hawajaona vita kwa hiuo wamesahau ndiyo maana wanaitafuta vita kwa udi na uvumba. Waulizeni watu walokuwa Kagera ndipo mtajua madhara ya vita. Tena vita ya wenyewe kwa wenyewe ni mbaya zaidi iwa kuwa huwa haiishi. Jamani. Tusifike huko.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums

ushauri wako nini sasa make naona kama unatetea kofia za yanga funguka alafu waambie magamba siyo kuchangia kama ujui kinachojadiliwa
 
Sisi tuloko mbali kazi yetu kushabikia tuu,, ngoja nasi tuje tupoteze ndugu zetu wa karibu ndo tutajua uchungu wake ukoje.. tusishabikie vita kwa sababu hayajatukuta ndugu zangu.. hizi naona sio siasa tenaa.

Watu wanatafuta maslahi tuu,, wanotaka kuingia ikulu kwa namna hii ni balaa,,,,kesho wataondoka wanaenda kwenye kikao makao makuu DSM mtaachwa nyie na polisi wenu.. AKILI ZA MBAYUWAYU......
 
Polisi ni kama mbwa tu wanaoamrishwa kuuma!!! Mwenye mbwa ndiye anayefahamu kisa na mkasa wa mbwa wake kuuma! Mwenye mbwa yupo... Kikwete ndiye mratibu wa shughuli zote za mabomu makanisani na katika mikutano ya kisiasa pamoja na mauaji na utesaji unaoendelea sasa katika Tanzania!!!
Umenena kweli kabisa,JK ndiye mratibu mkuu,wa matukio yote ya unyama yanayotokea hspa nchini.

Lakini JK anapaswa kutafakari mfano mmoja mkubwa,Hosni Mubarak wa Misti,naye miaka michache tu iliyopita,naye alikuwa Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote nchini Misri,naye kama JK,alikuwa akitumia kofia yake ya uamiri jeshi mkuu,kuviamrisha vikosi vyake vya ulinzi na usalama,kuwaua waandamanaji wowote,ambao watakataa amri ya kutoandamana,kutokana na hali hiyo,waMisri kwa maelfu waliuawa.

Kwa sasa kila mtu anajua kuwa Hosni Mubarak,anaozea jela,na kwa kuwa mzee Fast Jet,ni bingwa wa kufanya ziara nchi mbali mbali,ni vyema wanaoratibu safari zake,wakampangia safari ijayo,atembelee Misri,ili azuru gereza alilofungwa Hosni Mubarak na amuulize,ilikuwaje pamoja na kuwa na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo amekubali kulundikwa "Segerea" ya huko?!!

Jibu ambalo naamini atampa ni kuwa,hakuna binadamu yeyote anayeweza kuibadilisha historia,ambayo inasema,tokea dunia iumbwe hakujawahi kutokea mtawala yeyote,hata kama ana vyombo vya ulinzi na usalama mahiri kiasi gani,ambavyo vimewahi kushinda people"s power!!

Vyombo vya ulinzi na usalama navyo vinapaswa kutumia akili za mbayumbayu,wachanganye zao wenyewe na za kuambiwa na Amiri jeshi wao mkuu.

Hebu wajiulize tu kitu kimoja,hata kama taratibu za kijeshi zinawataka kutii amri bila shuruti,watafakari kuwa amri hizo za maboss wao wanazozitii,zinaweza kuleta maangamizi makubwa sana kwa Taifa hili,na watambue pia kuwa miongoni ya wahanga hao wataksokufa kutokana na machafuko hayo watakuwemo,watoto wao,wake zao,baba zao,mama zao,shangazi zao,wajomba zao na shemeji zao.

Sasa wanachopaswa kwa sasa ni kuweka kwenye mizani,hivi ni kweli maisha ya JK yana thamani zaidi ya watanzania wengine milioni 45?!!

Nawaomba makamanda wetu wa vikosi vya ulinzi na usalama,mlitafakari kwa makini sana suala hili,na naamini jawabu muafaka mtalipata.
 
Si uyaanzishe ww?? Watu wanalilia amani wee unawaza vita??shame kwako
Hujasikia hapo juu jamaa alikua anatoka zake kazini wakataka kumlenga kama mnyama-pori. Haijalishi unaandamana au huandamani you will fall victim of policcm. Hawa jamaa ni kama wehu and someone has to stop them and put them down to their knees. Kama unachagua kufa bila kelele waache wanaotaka kufanya kitu/
 
Umenena kweli kabisa,JK ndiye mratibu mkuu,wa matukio yote ya unyama yanayotokea hspa nchini.

Lakini JK anapaswa kutafakari mfano mmoja mkubwa,Hosni Mubarak wa Misti,naye miaka michache tu iliyopita,naye alikuwa Amiri jeshi mkuu wa majeshi yote nchini Misri,naye kama JK,alikuwa akitumia kofia yake ya uamiri jeshi mkuu,kuviamrisha vikosi vyake vya ulinzi na usalama,kuwaua waandamanaji wowote,ambao watakataa amri ya kutoandamana,kutokana na hali hiyo,waMisri kwa maelfu waliuawa.

Kwa sasa kila mtu anajua kuwa Hosni Mubarak,anaozea jela,na kwa kuwa mzee Fast Jet,ni bingwa wa kufanya ziara nchi mbali mbali,ni vyema wanaoratibu safari zake,wakampangia safari ijayo,atembelee Misri,ili azuru gereza alilofungwa Hosni Mubarak na amuulize,ilikuwaje pamoja na kuwa na vikosi vyote vya ulinzi na usalama vya nchi hiyo amekubali kulundikwa "Segerea" ya huko?!!

Jibu ambalo naamini atampa ni kuwa,hakuna binadamu yeyote anayeweza kuibadilisha historia,ambayo inasema,tokea dunia iumbwe hakujawahi kutokea mtawala yeyote,hata kama ana vyombo vya ulinzi na usalama mahiri kiasi gani,ambavyo vimewahi kushinda people"s power!!

Vyombo vya ulinzi na usalama navyo vinapaswa kutumia akili za mbayumbayu,wachanganye zao wenyewe na za kuambiwa na Amiri jeshi wao mkuu.

Hebu wajiulize tu kitu kimoja,hata kama taratibu za kijeshi zinawataka kutii amri bila shuruti,watafakari kuwa amri hizo za maboss wao wanazozitii,zinaweza kuleta maangamizi makubwa sana kwa Taifa hili,na watambue pia kuwa miongoni ya wahanga hao wataksokufa kutokana na machafuko hayo watakuwemo,watoto wao,wake zao,baba zao,mama zao,shangazi zao,wajomba zao na shemeji zao.

Sasa wanachopaswa kwa sasa ni kuweka kwenye mizani,hivi ni kweli maisha ya JK yana thamani zaidi ya watanzania wengine milioni 45?!!

Nawaomba makamanda wetu wa vikosi vya ulinzi na usalama,mlitafakari kwa makini sana suala hili,na naamini jawabu muafaka mtalipata.

Wapuuzi kabisa mnashindwa kuheshimu mamlaka zilizo kisheria mkishughulikiwa mnaanza kulialia pambaneni tu nyie sini makamanda?
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom