PICHA: Nyumba ya Mwalimu Shule ya Msingi Ipyana, Kyela

Hivi mbunge wa Jimbo hilo ni nani? Sio yule mzee wa misifa Mhe. Dkt Harrison Mwakyembe? Ana mikakati gani hasa kutumia tu zile fedha za mfuko wa jimbo? Wananchi wa Kyela mnachagua mtu kwa kuangalia fedha anazotoa wakati wa kampeni hamuangalii maisha yenu na watoto wenu baada ya uchaguzi yatakuwaje. Hiyo ni moja tu lkn karibuni nyumba zote za walimu hasa wa shule za Msingi ni majanga.

Amukeni na mfanye maamuzi sahihi la sivyo mtaendelea kulialia maisha yenu yote.
 
SAM_2238.JPG

Moja ya nyumba za walimu katika shule ya msingi Ipyana wilayani Kyela mkoani MbeyaHali ya nyumba za walimu katika shule hiyo ni mbaya kama inavyoonekana hapa

SAM_2239.JPG

Hili ni dirisha lenye kioo cha bati

Picha kwa hisani ya Gordon Kalulunga
Cc lizaboni
 
Kipaumbele chao ni kuwashughulikia akina Lowassa na CHADEMA si kuhangaika na walimu.
 
Hebu pita Lupembe ,Ibungu, Kilasilo ,Mbako , nenda hadi Isaki kajionee uozo wa nyumba za walimu utashangaa ! Au njoo mbele kidogo ya Ipyana , hapa utakuta ile iliyokuwa shule nzuri zamani ya Mpanda, imechoka hadi upepo kidogo tu inayumba , Aibu !
Mkuu asiishie hapo arudi nyuma kidogo hapo ikolo shule ya siku nyingi majengo ya waalimu kichefuchefu lugombo na katumba songwe ni vibanda vya nyasi tu.
 
Back
Top Bottom