PICHA - Njaa Mbaya Sana, Wanakijiji Zimbabwe Wamla Tembo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA - Njaa Mbaya Sana, Wanakijiji Zimbabwe Wamla Tembo

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Mar 13, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 13, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  <table style="width: 491px; height: 277px;" border="0" cellpadding="0" cellspacing="0"><tbody><tr><td colspan="3" style="padding-left: 10px; padding-top: 5px; width: 491px;">
  </td> </tr> <tr style="background-color: rgb(225, 225, 225); padding-top: 10px;"> <td style="width: 250px; padding-left: 5px; padding-bottom: 5px; padding-top: 5px;" valign="top">
  [​IMG]
  Wanakijiji wakijisevia nyama ya tembo</td> <td style="padding-left: 10px; width: 316px;" valign="top"> Saturday, March 13, 2010 3:02 AM
  Kweli njaa si mchezo, wanakijiji wa kijiji kimoja nchini Zimbabwe ambacho kimekumbwa na janga la njaa na umaskini, wanakijiji wake walitumia dakika 105 tu kumchuna ngozi tembo aliyekutwa amefariki na kisha kujisevia nyama zake na mwishoe hakuna hata </td> </tr> <tr> <td colspan="3" style="vertical-align: top; width: 491px;"> Ndani ya lisaa limoja na dakika 45 tembo aliyekutwa msituni amefariki, alichunwa ngozi na kisha wanakijiji walianza kujisevia nyama zake na kubakisha mifupa tu ikiwa imezagaa kwenye eneo ambalo tembo huyo alifariki.

  Mifupa ya tembo huyo nayo ilipitiwa na wanakijiji wengine siku iliyofuatia na hivyo kufanya eneo alilofariki tembo huyo liwe jeupee bila dalili ya kufariki kwa mnyama yoyote yule.

  Tukio hilo lilitokea katika kijiji kimoja nchini Zimbabwe ambapo inasemekana mifupa ya tembo hutumika kutengenezea sabuni.

  Tukio la wananchi kujisevia nyama ya mzoga wa tembo huyo halikufanyika kwa utulivu na hali ya vurugu na ngumi zilizuka wakati wanakijiji wakipigania kupata chochote cha kuganga njaa.

  Picha za tukio hilo zinaonyesha jinsi hali ngumu ya maisha na njaa inavyowafanya watu wale mpaka mizoga.

  Gonga linki chini kujionea picha za tukio hilo. http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=742511

  http://www.nifahamishe.com/album_preview.aspx?AlbumId=742511
  </td></tr></tbody></table>
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  sijuii kama ni njaa bwana.. juzi miye nimejaribu kula miguu ya chura (frog legs)..
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Mar 13, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Yuuuuck...them things are nasty man. I have never eaten and I will never eat frog legs...
   
 4. Companero

  Companero Platinum Member

  #4
  Mar 13, 2010
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Mbona watu, wazungu kwa waafrika, wanakula wanyamapori kila siku huku kwenye mbuga zetu za wanyama!

  Hivi hizi pembe za ndovu ambazo Serikali imeamu kuziuza unadhani hao tembo waliokuwa nazo waliuliwa na kuzikwa tu bila kuchunwa, kuliwa na kutengenezea mafuta ya tembo?
   
 5. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #5
  Mar 13, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,037
  Trophy Points: 280
  mbona tembo analiwa tu kama kawaida, kuna watu wanatushangaa sana tunavyokula ng'ombe, twiga pia ni mtamu , crocodile as well
   
 6. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,367
  Likes Received: 7,008
  Trophy Points: 280
  hat Tanzania hivyo vitu hutokea, tusiwe wepesi wa kukubali propaganda za media za west
   
 7. mbarikiwa

  mbarikiwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 13, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 507
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hii sio Njaa, ni sawa tu na wana wa Ishmail wanavyokula Ngamia
   
 8. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,407
  Likes Received: 685
  Trophy Points: 280
  Nyama ni nyama,nyama ni nyama!!!!!!!!!!!!!
   
 9. Omuregi Wasu

  Omuregi Wasu JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 753
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mwandishi wa habari hiyo namkaribisha China. Hakuna njaa na vyakula ni vingi lakini tunakula panya, nyoka, ng'e, mbwa, ruba wa mitoni, mbu, vyura, paka n.k Tusemeje kwa hao waliokula tembo ambaye analiwa na jamii nyingi za watu?
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280

  Kumbukumbu la Torati/ Chapter 14

  3. Usile kitu cho chote kichukizacho.
  4. Wanyama mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi,
  5. kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima;
  6. na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla.
  7. Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;
  8. na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
  9. Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula;
  10. na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu.
  11. Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.
  12. Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu;
  13. na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake;
  14. na kila kunguru kwa aina zake;
  15. na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake;
  16. na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa;
  17. na mwari, na nderi, na mnandi;
  18. na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo.
  19. Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale.
  20. Mna ruhusa kula katika nyuni wote walio safi.
  21. Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.
  22. Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka.
  23. Nawe utakula mbele za Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua apakalishe jina lake, zaka ya nafaka zako, na divai yako, na mafuta yako, na wazaliwa wa kwanza wa makundi yako ya ng'ombe na ya kondoo; ili upate kujifunza kumcha Bwana, Mungu wako, daima.
   
 11. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,821
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  yuk,congo hapo gorilla ndio kitoweo chao kikubwa
   
 12. L

  Lunanilo JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2010
  Joined: Feb 15, 2008
  Messages: 370
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kuna mahali hapo hapo Tanzania tembo wanaliwa kama kawaida, tena wawindaji huipitisha mitaani kuuza. Sijui kama siku hizi wameacha lakini kwenye miaka ya sabini nilikuwa katika huo mji ilikuwa kawaida watu kuja kuuza nyama ya tembo ( smoked) wanakuuliza kabla hawajafungua kama unatumia hiyo kitu.
   
 13. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,821
  Likes Received: 1,167
  Trophy Points: 280
  nimeshakula sana,hata mwaka fulani tulikua na project ya uwindaji hapo ifakara tembo wote waliouliwa wanakijiji waliitwa kuja kuchukua nyama na walikua hawabakishi hata ugoko,nyama yake poa tu ukizingatia vegetarian
   
Loading...