Picha niliyopiga na shemeji yangu ilisababisha mke wangu kunihisi namsaliti

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,820
Ilikuwa siku nzuriiiiiiiii ya kuvutia, nikaamkia machinjioni, nikanununua figo na maini kama kilo Saba, nikapitia sokoni, nikanunua kuku watatu wa kienyeji, nikawachinja na kuwanyonyoa.

Nikanunua mboga za majani, matunda na viungo mbalimbali. Nikarudi nyumbani, nikashusha mzigo, kisha nikamchukua mdogo wangu tukatoka kidogo, ilikuwa siku ya Jumamosi.

Mdogo wangu akaniambia twende tukampitie shemeji yako nikutambulishe, Basi tukaenda hadi kwenye nyumba ya huyo binti, akatupokea na kutukirimu kwa vinwaji.

Baada ya muda kidogo, tikahamia sehemu kwenye kitimoto, huko Sasa ndio kimbembe kilipoenda kuanza.
Mdogo wangu kwa kutumia camera yangu akanipiga picha nikiwa nimepozi na shemeji yangu, tukakaa huko hadi saa mbili kasoro tukawa home.
Tukala chakula vizuri, nyumba nzima tukiwa na furaha.
Mida ya saa sita na kitu, nikajikuta napigwa,

Napigwa na mikanda, napigwa vibao, narushiwa viatu, waifu kakasirika, nikamuuliza shida ni Nini? Akasema hujui ehh, hujijui kuwa wewe Ni Malaya na huyu ni changudoa wako, akimtaja jina la yule binti. Matusi na kashfa vikaendelea na mimi hasira zikapanda kwelikweli, nikasema leo ntamvunja mtu.

Nikatoka usiku huo, nikaenda sehemu, nikapiga chicha la hatari, nikarudi home saaa kumi na moja kasoro, niko mafuta vibaya sana.
Nikalala kama mzigo.

Nikashtuka mida ya saa tano na nusu, mwili una rangi mbalimbali, kijani, njano, pink, maroon, nyekundu, yaani zile rangi za kupaka kwenye kucha nimechorwa nazo mwili mzima, Mimi Ni Malaya, Mimi Ni Malaya.

Rangi zimekaukia mwilini sijui hata namna ya kuzitoa.
Mke wangu kaja huku analia, nisamehe, nisamehe, kumbe Yule mwanamke ni wa mdogo wako.

Kumbe alienda kunishtaki kwa dogo, dogo akamthibishia kuwa Yule mwanamke ni wake, akamuonyesha picha na mawasiliano yao mbalimbali.
Nukamwambia nimekusamehe, ila haya maandishi yako yameingia hadi ndani ya akili yangu, Mimi Ni Malaya, Mimi Ni Malaya ,Mimi Ni Malaya.
 
Situmii chai siku hizi!
Hebu lete chapati 2?
934fbf841f07ad353d57ad0c382dd5f7.jpg
 
Kwann uende kula ktmoto bila mkeo...??

Wewe si malaya tu na uchoyo unaooo...!!
 
Mwanaume mwenye kujiselfia na wanawake mda mwingi kila tukio huwaga namfananisha na Le mutuZ.
 
Duuuu............pole sana, kichapo cha pili utahama hiyo nyumba. Wewe endelea kulea yaya yayaa utaisoma namba
 
Ilikuwa siku nzuriiiiiiiii ya kuvutia, nikaamkia machinjioni, nikanununua figo na maini kama kilo Saba, nikapitia sokoni, nikanunua kuku watatu wa kienyeji, nikawachinja na kuwanyonyoa.

Nikanunua mboga za majani, matunda na viungo mbalimbali. Nikarudi nyumbani, nikashusha mzigo, kisha nikamchukua mdogo wangu tukatoka kidogo, ilikuwa siku ya Jumamosi.

Mdogo wangu akaniambia twende tukampitie shemeji yako nikutambulishe, Basi tukaenda hadi kwenye nyumba ya huyo binti, akatupokea na kutukirimu kwa vinwaji.

Baada ya muda kidogo, tikahamia sehemu kwenye kitimoto, huko Sasa ndio kimbembe kilipoenda kuanza.
Mdogo wangu kwa kutumia camera yangu akanipiga picha nikiwa nimepozi na shemeji yangu, tukakaa huko hadi saa mbili kasoro tukawa home.
Tukala chakula vizuri, nyumba nzima tukiwa na furaha.
Mida ya saa sita na kitu, nikajikuta napigwa,

Napigwa na mikanda, napigwa vibao, narushiwa viatu, waifu kakasirika, nikamuuliza shida ni Nini? Akasema hujui ehh, hujijui kuwa wewe Ni Malaya na huyu ni changudoa wako, akimtaja jina la yule binti. Matusi na kashfa vikaendelea na mimi hasira zikapanda kwelikweli, nikasema leo ntamvunja mtu.

Nikatoka usiku huo, nikaenda sehemu, nikapiga chicha la hatari, nikarudi home saaa kumi na moja kasoro, niko mafuta vibaya sana.
Nikalala kama mzigo.

Nikashtuka mida ya saa tano na nusu, mwili una rangi mbalimbali, kijani, njano, pink, maroon, nyekundu, yaani zile rangi za kupaka kwenye kucha nimechorwa nazo mwili mzima, Mimi Ni Malaya, Mimi Ni Malaya.

Rangi zimekaukia mwilini sijui hata namna ya kuzitoa.
Mke wangu kaja huku analia, nisamehe, nisamehe, kumbe Yule mwanamke ni wa mdogo wako.

Kumbe alienda kunishtaki kwa dogo, dogo akamthibishia kuwa Yule mwanamke ni wake, akamuonyesha picha na mawasiliano yao mbalimbali.
Nukamwambia nimekusamehe, ila haya maandishi yako yameingia hadi ndani ya akili yangu, Mimi Ni Malaya, Mimi Ni Malaya ,Mimi Ni Malaya.
Kama hayo maandishi yameingia ndani ya akili yako uamuzi ni mmoja tu, anza umalaya rasmi ili ufurahishe moyo wako. Tabia zingine mbaya tunafunzwa na wake zetu kutuhisi vibaya, wao wanatuimbia nyimbo kuwa wewe uko hivi au huko vile kumbe zile kauli zao ndizo zinatupa ujasiri wa kucheat au kubadilika. Hongereni kina Mama kwa kutubadili tabia.
 
Ila umalaya gharama kichizi
 
Halafu juzi si ndio ilikuwa siku ya mavuno ya umalaya? Umepona?
 
Back
Top Bottom