Picha na habari ya Dk Slaa, Lissu kupandishwa kizimbani Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha na habari ya Dk Slaa, Lissu kupandishwa kizimbani Arusha

Discussion in 'Jamii Photos' started by Chenge, Nov 9, 2011.

 1. Chenge

  Chenge JF-Expert Member

  #1
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 1,077
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa, akishuka kutoka kwenye Karandinga la Polisi, kusomewa mashitaka yanayomkabili na washitakiwa wengine 26 waliofikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kwa kosa la kufanya mkusanyiko kinyume na sheria. (Picha na Filbert Rweyemamu)


  Dk Slaa, Lissu mbaroni

  Dk Slaa, Lissu na wafuasi wengine 25 wa Chadema walifikishwa mahakamani jana kujibu mashtaka matatu tofauti likiwamo la uchochezi ambalo linamkabili Dk Slaa pekee.
  Viongozi hao wa Chadema na wafuasi wao, walifikishwa mahakamani wakiwa chini ya ulinzi mkali wa maofisa wa polisi majira ya saa nane mchana na kesi hiyo ilianza kutajwa mahakamani saa 9:00 alasiri.

  Wakili wa Serikali, Haruna Matagane alisema watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa makosa mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali usiku wa Novemba 7, mwaka huu na saa 12 asubuhi Novemba 8, mwaka huu licha ya kutakiwa kutawanyika na Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP), Peter Mvulla.
  Akisoma mashtaka hayo mbele ya Hakimu Mkazi, Devota Kamuzora, mwendesha mashtaka huyo alisema watuhumiwa hao kwa pamoja walikaidi amri halali ya Mvulla kinyume cha sheria walipotakiwa kutawanyika.

  Alisema Dk Slaa anashitakiwa kwa kosa moja pekee la kutoa maneno ya uchochezi kinyume na sheria mnamo Novemba 7, mwaka huu saa 11:30 jioni.

  “Tunatoa muda ifikapo saa kumi na moja jioni wanataka kumpeleka kwa ndege Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Arusha, Zuberi Mwombeji kwa IGP Said Mwema ili wampangie wilaya nyingine ya kuhamia,” Matagane alisema akinukuu kauli inayodaiwa kutolewa na Dk Slaa.
  Wakili huyo wa Serikali alisema Dk Slaa pia anatuhumiwa kutoa maneno ya uchochezi kutaka Lema atolewe Kisongo ifikapo saa kumi na jioni la sivyo kutakuwa na maandamano ya kumtoa Rais Jakaya Kikwete madarakani.

  Baada ya kusomewa mashtaka hayo, Mawakili wa utetezi, Method Kimomogoro na Arbert Msando waliomba watuhumiwa hao wapatiwe dhamana kwa kuwa yanaruhusu kufanya hivyo ombi ambalo lilikubaliwa na Hakimu Kamuzora akiwataka washtakiwa wote kuwa na wadhamini wawili na kila mmoja kuweka ahadi ya kiasi cha Sh5 milioni.Watuhumiwa 20 wakiwamo viongozi walipata dhamana na kesi yao imeahirishwa hadi Novemba 22, mwaka huu.

  Source : Mwananchi Newspaper 09/11/2011   
 2. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #2
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Lazima kieleweke tu! hatuwezi kuendelea kunyanyaswa kana kwamba tuko utumwani, eti tulazimishwe kuwapenda wahujumu uchumi! CDM HADI KIELEWEKE! HATA TUVUNJWE MATAYA NAMNA HII!!!!

  Vurugu noma.jpg
   
 3. RasJah

  RasJah JF-Expert Member

  #3
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 697
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  ni ccm wenyewe wanapata chati hao jamaa maana muda mpaka leo arusha ni migogoro hakuna utendaji shughuli za maendeleo zinakaba na ujue kabisa washindwa kukaa sawa ina maana baadae watu wataanza kukaba ao watalii na tutakosa hela ya kuchangia pato la taifa na itawakuwa shida.

  Huyo anaetoa order kwa ajili ya kusimamisha vitu vya msingi na viko wazi kisheria na haki itakuwa shida baadae maana watu watashindwa kuvumilia wataona bora wafe sasa atuwezi fika uko wakati kila mwananchi ana amani sasa naomba sana jamani tuwe makini na maamuzi na ina maana gani mgeni watu kaja kashindwa kufika hapo sio picha nzuri tunaaribu sifa za Tanzania.

  Mungu ibariki Tanzania
   
 4. z

  zamlock JF-Expert Member

  #4
  Nov 9, 2011
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 3,849
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  yangu macho ila niko tayari kwa lolote lile hapa kuandamana nitajitokeza
   
 5. LEGE

  LEGE JF-Expert Member

  #5
  Nov 9, 2011
  Joined: Oct 14, 2011
  Messages: 4,914
  Likes Received: 5,351
  Trophy Points: 280
  Mbona hayo maneno yaliyo andikwa hapo kwamba yalisemwa na dr slaa kama yameongezwa chumvi vile.
  Kama kuhusu kuandamana kwenda kumtoa LEMA kwa maandamano.Na hilo kuhusu jk.
  Duuu kweli hawa magamba ni noma .
   
 6. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #6
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Nadhani busara ikitumika itasaidia sana. Hiyo ni kwa wote, serikali na wapinzani. Wengi mnasema eti niko tayari kwa lolote. sidhani kama inasaidia, utakufa na wanaobaki maisha yataendelea bila wewe. Then utasahaulika siku mbili tu.
   
 7. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #7
  Nov 9, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Una fikra zax kitoto ndo maana unaogopa kufa, kwani ulichagua kuzaliwa au uliletwa tu kupitia starehe za unaowaita wazazi wako.
  Kama ulisoma enzi za Mwl. tulikiwa tukiimba nyimbo za kuwapa moyo wazalendo wenye moyo wa ushujaa, sio waoga kama wewe!
  Unaukumbuka wimbo huu "AFADHALI KUWA NA TAIFA AMBALO, HALINA SIRAHA ZA KISASA LAKINI, LINA MOYO WA USHUJAA, KULIKO KUWA NA TAIFA, LENYE SIRAHA ZA KISASA LAKINI VIJANA WAKE NI WAOGA"
   
 8. d

  dotto JF-Expert Member

  #8
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  MAisha mabaya tuliyonayo ni kama tumeshakufa tayari.
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Nov 9, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Hii imezidi Mkuu
  [​IMG]
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Nov 9, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,559
  Likes Received: 1,916
  Trophy Points: 280
  Hii ya wapi hii?
   
 11. katabu

  katabu JF-Expert Member

  #11
  Nov 9, 2011
  Joined: Apr 19, 2011
  Messages: 307
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kifua kipo kaka kama Misri na Tunisia?
   
 12. Malipesa

  Malipesa JF-Expert Member

  #12
  Nov 9, 2011
  Joined: Aug 23, 2011
  Messages: 310
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama haki ipo kisheria na mtu ananyimwa sababu ya mtu mwingine tu et sababu ameamua basi nami naunga mkono haki hiyo itafutwe kwa nguvu. Nimesoma hapa JF etu Rombo wamepandisha bandera ya Kenya kwa sababu ya hujuma.

  Mungu atusaidie tusiichukie nchi yetu
   
Loading...