PICHA: Mzee MWINYI akiwakabidhi KWALEGO tangi la Maji na Kitanda;... MZEE STILL STRONG and KICKING!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

PICHA: Mzee MWINYI akiwakabidhi KWALEGO tangi la Maji na Kitanda;... MZEE STILL STRONG and KICKING!!

Discussion in 'Jamii Photos' started by nngu007, Oct 1, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  MZEE MWINYI AWAKABIDHI KWADELO TANGI LA MAJI, KITANDA CHA KUJIFUNGULIA

  [​IMG]
  Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Ali Hassani Mwinyi leo
  [​IMG]
  Diwani wa Kata ya Kwadelo, Kondoa mkoani Dodoma, Omari Kariati akimsalimia Mama Sitti Mwinyi nyumbani kwa Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi (kushoto), Mikocheni jijini Dar es Salaam. kabla ya hafla ya wananchi wa Kata hiyo kukabidhiwa tangi la maji na kidanda cha kujifungulia kina mama, iliyofanyika nyumbani hapo, leo.
  [​IMG]
  Diwani Kariati akiongozana na Mzee Mwinyi na Mama Sitti Mwinyi kwenda eneo la tukio
  [​IMG]
  UNAONA MAMBO YA KILIMO KWANZA? Akasema Omari Kariati wakati akitazama maembe yaliyopo kwenye mwembe wa kisasa uliopo nyumbani kwa Mzee Mwinyi.
  [​IMG]
  Kina mama wa Kwadelo wakiwa kwenye viwanja vya shughuli ya makabidhiano ya vifaa hivyo
  [​IMG]
  "Kwanza tunamshukuru Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Mzee wetu Ali Hassan Mwinyi kwa kutukaribisha nyumbani kwake kukamilisha hafla hii. Shughuli iliyotuleta hapa ni Mzee wetu kuwakabidhi wana-Kwadelo tangi kubwa la maji la sh. 650,000 na kitanda cha kujifungulia kina mama, kisha atamapatia sh. 200,000 kijana wetu aliyemuahidi kwa ajili ya kukamilisha masomo yake ya ualimu pale Ununio" akasema Diwani wa Kwadelo Omari Kariari kufungua shughuli. pembeni ni Mzee Mwinyi na Mkewe Mama Sitti, wakimsikiliza.
  [​IMG]
  Kisha mzee Mwinyi na mkewe wakasongea pamoja na waalikwa pahala vilipokuwa vitu vya kukabidhi. Hapa anakabidhi kitanda
  [​IMG]
  Kwa furaha baada ya kukabidhiwa, mama mmoja wa Kwadelo akakifanyia majaribio kidogo kitanda hicho.
  [​IMG]
  Kisha Mzee Mwinyi akakabidhi tangi la lita 5000 kwa Mwadham Msami (kushoto) ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji cha Kerereng'ombe, palepale Kwadelo. Naye Omari Kariati akishuhudia
  [​IMG]
  Baada ya kurejea meza kuu, Mzee Mwinyi akakabidhi sh. 200,000 kwa kijana, Kassim Omar kwa ajili ya kumalizia masomo yake ya ualimu Chuo cha Ununio, Bagamoyo.
  [​IMG]
  Kisha Mzee Mwinyi akaeleza yake ya moyoni kuwahusia wana Kwadelo na Watanzania kwa jumla akisema "wanaodhani maandamano yanaleta maendeleo wanapotea, maendeleo yanaletwa na kujituma na kutumia fursa zilizopo kufanya kazi kwa bidiii". Kushoto ni Mama Sitti Mwinyi.
  [​IMG]
  Picha za pamoja na Mzee mwinyi zikapigwa kwa makundi ya wananchi wa Kwadelo waliohudhuria hafla hiyo
  [​IMG]
  Hawa ni kina mama wa Kwadelo wakiwa na Mzee Mwinyi
  [​IMG]
  Na kina Baba wakachangamkia
  [​IMG]
  Vijana wa Kwadelo wakiwa nyumna ya Mzee Mwinyi katika picha ya pamoja
  [​IMG]
  Hawa pia ni vijana wa Kwadelo kati ya 50 wanaofanya shughuli zao jijini Dar, waliojitolea kwenda kulima katika kata hiyo
  [​IMG]
  Waandishi nao wakatumia fursa hiyoo adhimu kupigapicha na Mzee Mwinyi. Kulia kabisa ni Mimi
  [​IMG]
  Hapa pia ni waandishi wakichangamkia fursa hiyo.
  [​IMG]
  "Karibuni Chai" akasema Mama Sitti kuwakawakabisha wageni mwishoni mwa shughuli
  [​IMG]
  Wageni wakachangamkia chai kama hivi:


  POSTED BY: BASHIR NKOROMO AT SUNDAY, SEPTEMBER 30, 2012 0 COMMENTS
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Wakati akiwa RAIS... kabla hajaanza kazi, alikuwa anaamka asubuhi kama saa kumi na moja hivi...

  Wanamwendesha MPAKA MASAKI wakati huo hakuna hiyo hotel iliyopata kuungua

  Mzee Mwinyi ataanza kutembea toka pale... Anapita NYUMBA ya ZAMANI ya KAWAWA anendelea

  kutembea MPAKA Maeneo ya OYSTERBAY HOTEL ndipo analipanda GARI kurudi IKULU; alikuwa

  anafanya hivyo kila SIKU - ISIPOKUWA IJUMAA... kwa Miaka 10 kiwa Madarakani...

  Sasa Mwangalie ana Miaka 86 lakini strong na hekima zake zipo... NDIO TUNGEPENDA MARAIS WETU

  WAWE HIVYO na ana WAKE WAWILI... Hajachoka!!!
   
 3. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  inachekesha. miaka 10 ya uongozi wake wananchi wa kwadelo walitakiwa wawe na maji. lakini wapi. eti leo anawaitia chai.
   
 4. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #4
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,843
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  [​IMG]
  Rais Mstaafu wa awamu ya Nne, Ali Hassani Mwinyi leo


  Katu sikubaliani na wewe kwenye red!
  mwandishi wa daraja gani ww??
  hakika nina wasiwasi na ww kama hata hili una kosea
  kwenye issue nyeti unaweza angamiza taifa.......................period!!


   
Loading...