Picha: Mwenyekiti wa CHADEMA alivyochinjwa... [Extreme Images] | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Picha: Mwenyekiti wa CHADEMA alivyochinjwa... [Extreme Images]

Discussion in 'Jamii Photos' started by Crashwise, Apr 29, 2012.

 1. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #1
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Usa River, wilayani Arumeru, Msafiri Mbwambo (38) ameuawa kwa kukatwa shingoni na kitu chenye ncha kali.
   
 2. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Usa River, wilayani Arumeru, Msafiri Mbwambo (38) ameuawa kwa kukatwa shingoni na kitu chenye ncha kali.
  Kifo hicho kilitokea juzi majira ya saa mbili usiku eneo karibu na uwanja wa polisi Mji Mwema, ambapo wauaji hao walimkata shingo kwa kuanzia nyuma na kubakiza kidogo eneo la mbele ya shingo na kumwacha akiwa amelala chini kama aliyeanguka na pikipiki.
  "Atakuwa amekatwa na kitu kama shoka kwani wamekata shingo kwa nyuma, tulipotoka ndani baada ya kuitwa tulimkuta amelala pale unapoona kuna damu, kichwa chake walikiweka juu ya jiwe, kiwiliwili chake kilikuwa kwenye pikipiki, mguu mmoja ukiwa chini mwingine juu kama vile alikatwa akiwa kwenye pikipiki akaanguka nayo.
  "Unajua mimi nakaa nyumba ile lakini sikusikia tukio hili likitokea mpaka nilipokuja kugongewa na majirani na tulikuwa hatuna umeme ulikatika kama saa mbili zilizokuwa zimepita, ila ilikuwa majira ya saa tatu kasoro hivi," alisema mwananchi anayeishi karibu na eneo lililipotokea tukio hilo ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini.
  Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Thobias Andengenye, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo lililotokea takriban wiki moja baada ya watu wanne kuuawa kwa kunyongwa na miili yao kutupwa kwenye maeneo tofauti wilayani Arumeru, ambapo alisema kuwa jeshi hilo linaendelea na uchunguzi wa vifo hivyo.
  Naye mke wa marehemu, Eunice Mbwambo (30) alisema kuwa siku ya tukio marehemu alimchukua kwa pikipiki kutoka eneo la Kisambaro anakofanyia shughuli zake za kushona nguo majira ya saa mbili usiku akiwa na mtoto wao wa mwisho, Magreth (6) kati ya watatu walio nao na kuwapeleka nyumbani.
  Alisema kuwa kabla hawajashuka kwenye pikipiki marehemu alipokea simu akamweleza kuwa anakwenda kwenye kioski kinachofahamika kwa jina la mmiliki, Hashimu, kwa ajili ya kumuona rafiki yake anayeitwa Gurisha Msuya, maarufu kama ‘Kipara', ambapo baada ya muda ndipo akapata taarifa kuwa amekutwa amekufa.
  Mmiliki wa kioski hicho, Hashimu Bakari na rafiki wa marehemu Mwambo, ‘Kipara' walikiri marehemu kufika kwenye kioski hicho ambapo walisema kuwa aliondoka muda mfupi baada ya kupigiwa simu na kuondoka kwa ahadi ya kurudi baada ya muda mfupi kwa ajili ya kumpitia Kipara kwani wanaishi nyumba jirani lakini hakutokea mpaka majira ya saa nne usiku walipopata taarifa ya kifo chake.
  "Marehemu alikuwa na kawaida ya kuja hapa kuangalia mpira, hakuwa mtu mgomvi na jana (Ijumaa) alikuja kuangalia uamuzi wa kikao cha CCM juu ya sakata la kuwataka mawaziri wajiuzulu ndipo akiwa hapa akapigiwa simu akaondoka, hakuwa mgomvi wala hakuwa anakunywa pombe, alikuwa Msabato," alisema Hashimu.
  Wakizungumza kwa wakati tofauti wakazi wa eneo hilo walihusisha kifo hicho na tabia yake ya kupigania haki na kupambana na ufisadi kwenye miradi ya wananchi, ambapo walidai kuwa alikuwa amefuatilia mpaka kwa ofisa mtendaji wa kata kuhakikisha kikao cha mapato na matumizi cha kitongoji cha Magadini ambacho akijafanyika kwa zaidi ya miaka minne sasa kinafanyika Jumatatu.
  Wananchi hao, Jubileti Muro, Ruth Munisi, Eline Kisanga, Ibahimu Salum na wengine kadhaa ambao hawakuwa tayari majina yao kuandikwa gazetini walisema kuwa marehemu Mbwambo alipigania mkutano huo kwa kupeleka barua kwa Ofisa Mtendaji wa kata, Laizer John, ambaye aliagiza kikao hicho kifanyike Jumatatu.
  Walisema kuwa ufuatiliaji wake wa mambo ulimfanya marehemu kutofautiana na viongozi wa kitongoji akiwamo Mwenyekiti wake, Matia Nathan, ambaye ilifikia hatua ya kumtolea vitisho ambavyo aliwahi kuwaeleza wananchi kwenye moja ya mikutano yake ya hadhara.
  Walisema kuwa kwenye kikao hicho marehemu Mbwambo alikuwa amejiandaa kikamilifu kwa kukusanya nyaraka mbalimbali kuthibitisha tuhuma za ubadhirifu wa mali za umma zinazofanywa na viongozi kwenye miradi ya ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata ya Laki Tatu, mradi wa kusambaza maji safi na salama na mradi wa machimbo ya kokoto kitongojini hapo.
  Wananchi hao walisema kuwa marehemu alikuwa akisimamia jambo lake anakuwa na ushahidi wa kutosha, ambapo walitolea mfano kuwa aliweza kuwabana viongozi wakatoa fedha zilizokuwa zimekwisha kuliwa kwenye mradi wa maji, zilizotumika kutengeneza barabara kwa kiwango cha changarawe ambapo kwa sasa wanafikiria barabara hiyo waipe jina lake kwa ajili ya kumuenzi.
  Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kitongoji hicho, Nathan, alikanusha kutofautina na marehemu katika utendaji wake na kuwa hakuwahi kumtisha ambapo alisema kuwa yeye binafsi alikuwa akimpenda hasa kutokana na tabia yake ya kufuatilia mambo huku akiwa mkweli, kwani alikuwa akikosoa na kusifia panapostahili.
  "Binafsi sijawahi kumtishia marehemu kwa kufuatilia mapato na matumizi ya kitongoji, nilikuwa nachukulia ufuatiliaji wake kama changamoto ya kufanya kazi vizuri zaidi," alisema Nathan akiongea na Tanzania Daima kwa njia ya simu.
  Alisema kuwa ni kweli alipanga kuitisha kikao cha uongozi kati ya Jumatatu na Jumanne ili waweze kupanga tarehe ya kufanya mkutano mkuu wa kitongoji kwa ajili ya kusoma taarifa ya mapato na matumizi huku akisema kuwa hana taarifa kama marehemu aliwahi kuwasiliana na mtendaji wa kata kuhusiana na suala hilo.
  Naye Mbunge wa jimbo hilo, Joshua Nassari, aliwataka wananchi kuwa watulivu kwa kipindi hiki kigumu wakati Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi wake ili kuhakikisha waliohusika na tukio hilo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.
   
 3. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu weka worming ya huu uzi ...Dah! Hatari hii
   
 4. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #4
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, walidai kuwa kabla ya tukio Mbwamb
  alikuwa na wenzake wakistarehe kwa vinywaji, lakini yeye hakuwa anakunywa
  chochote lakini ghafla alipigiwa simu na watu hao, wakidai kuwapo wanachama
  wa CCM waliotaka kurudisha kadi na kujiunga na Chadema
  .
  Hata hivyo, chanzo
  cha tukio hilo hakijajulikana ila taarifa za awali zinahusisha masuala ya

  kisiasa, kwani baada ya uchaguzi mdogo wa ubunge Arumeru Mashariki kumalizika, malumbano ya kisiasa na kukamiana yaliendelea eneo hilo. SOURCE HABARI LEO
   
 5. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2012
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Mbona Arumeru mauaji yamekuwa kitu cha kawaida? Wale watano waliokutwa wadmekufa barabarani uchunguzi ulifikia wapi? CDM jamani mbona tunaisha?
   
 6. Mchaka Mchaka

  Mchaka Mchaka JF Bronze Member

  #6
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 20, 2010
  Messages: 4,530
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  Dah..wanadamu wamekuwa wabaya hivi..R.I.P kamanda!
   
 7. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Hivi duniani kuna watu wanyama namna hii
   
 8. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #8
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nimeweka kwenye title kabisa labda Mods wanisaidi namna ya kuiweka lakini yoyote kwa yote ni unyama ambao sikutegemea kama watanzania leo hii tumefikia unyama wa kiwango hiki...haivumiliki...
   
 9. Skp2ole

  Skp2ole Senior Member

  #9
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 13, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  inasikitisha sana kama sisi wenyewe kwa wenye tunafanyiana ukatili kiasi hiki bila hata kuogopa uwepo wa Mungu. Mungu aijalie familia yake Amani na upendo na awape Mwanganza Pia ailaze mahala pema mwili wa marehemu AMEN.
   
 10. TODO

  TODO JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2012
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 219
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  uuuh! sad story.anyway may he rest in peace.sijui twaenda wapi na tabia hii iliyoibuka.Mungu ampe mjane nguvu ya kuweza kustahimili hali hii.
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Huwezi amini........
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Wanazunguka mbuyu.......Ngoja tusubiri viongozi wa chama watasema nini lakini mambo haya haya vumiliki hata chembe....
   
 13. mnyanyaswaji

  mnyanyaswaji JF-Expert Member

  #13
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 469
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Dah very sad! Tumefikia hatua hii tena dah??
   
 14. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Mungu tusaidi amani isitoweke kwa sababu za kisiasa tu, poleni wafiwa , CDM na watanzania wote
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Duh hii hatari. Mbona tunaelekea pabaya. Kwa kuwa huyu alikuwa mwanasiasa inabidi polisi wafanye uchunguzi wa kina na kuutangazia umma juu ya kilichosababisha kuuawa kinyama namna hiyo. Yasije yakawa ni mauaji yanayohusishwa na siasa.
   
 16. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #16
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ni wanne na haijajulikana kama ni wana chadema moja kwamoja....lakini matukio ambayo unaweza kuya husisha moja kwamoja ni yule wakala alie uwawa kinyama kule Igunga na Kukatwa katwa kwa wabunge wa chadema kule mwanza pengine nia ya walikuwa wana wakataka ilikuwa ni kuwafanya kama walivyo mfanya mwenyekiti....
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Apr 29, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  sasa kama polisi wameshaanza kusema haihusianai na mambo ya kisiasa inaelekea walisha fanya uchunguzi wa kifo cha Mbwambo hata kabla hajafa......
   
 18. Mfatiliaji

  Mfatiliaji Senior Member

  #18
  Apr 29, 2012
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 101
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  This has gone too far...
   
 19. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #19
  Apr 29, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,524
  Likes Received: 10,441
  Trophy Points: 280
  sipati picha angekua mwenyekiti wa ccm.
   
 20. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #20
  Apr 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kuna haja ya kila mwanachama wa CDM kuwa makini sana.

  WanaJF kwa jinsi hali ilivyo haya sisi ambao tuko mstari wa mbele kupigania ukombozi wa kweli tungekuwa tunajuana wangeshatuua!!!!!

  Hali inatisha, hili suala siyo la kufumbia macho. Viongozi wa CDM taifa toeni tamko.
   
Loading...