Picha:Mwanaharakati wa kutetea Haki za Wanawake na Watoto akutwa amekufa Hotelini

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225

MBUNGE wa Musoma mjini Vicent Nyerere(Chadema) amemtaka mkuu wa jeshi la polisi nchini (IGP)Said Mwema kuchukua hatua sasa kuhusu mauaji ya kikatili ambavyo yameibuka katika Manispaa ya Musoma na wilaya ya Butiama.


Akizungumza tukio hilo amesema katika kipindi cha mwezi mmoja tu zaidi ya watu kumi na saba wameuawa huku wengine wakichinjwa vichwa na wauaji kuondoka navyo pamoja na viungo vyao vingine vya miili yao.


Alisema pamoja na hali hiyo ambayo imechangia hofu kubwa kwa wananchi lakini hakuna jitihada zozote zinazochukuwa kwaajili ya kukabiliana na vitendo hivyo vya kinyama.

Aidha mbunge huyo alimtaka pia Rais Jakaya Kikwete kuchukua hatua kwa wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama wa wilaya hizo ambao amedai baadhi yao wameshindwa kusimamia majukumu yao na kubaki kuendesha siasa wakati wananchi wakizidi kuawa kinyama na wengine kuachwa na vilema vya maisha.

"Ni tatizo kubwa ndani ya mwezi mmoja tu watu kumi na saba wameuawa kinyama na wengine kuchinjwa lakini mbali na vyombo vya dola kukaa kimya hata nyinyi waandishi mmeshindwa kujulisha umma kuhusu ukatili huu"alisema Nyerere na kuongeza.


"Rais mtoe mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya(DC) hapo Musoma amekalia siasa na kuacha majukumui ya serikali katika kulinda raia na mali zao hii ni hatari kubwa"aliongeza.

Hata hivyo wakati mbunge huyo akitoa kauli hiyo,mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Butiama Angelina Mabula,ameliagiza jeshi la polisi kufanya kazi usiku na mchana katika kuhakikisha linawatia mbaloni watu wote ambao wanahusika na mauji ya kikatili ya raia.

Mabula ambaye ni mkuu wa wilaya ya Butiama,alitoa agizo hilo juzi jioni baada ya kuokotwa kwa mama mmoja Sabina Mkereri (46)ambaye alichinjwa na wauji kuondoka na kichwa chake katika kijiji cha Kabegi kata kata ya Nyakatende.

"Nawaomba wananchi mtoe ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha wahusika wote wanasakwa na kuanzia sasa naagiza kuanza kwa vikundi vya ulinzi shirikishi kwaajili ya kufanya kazi ya kuwasaka watu hawa usiku na mchana…jamani tunaipeleka wapi Tanzania yetu yenye amani kwa kufanya matendo haya ya kinyama"alisema DC Mabula.

Kwa upande wake mwenyekiti wa CCM wilaya ya Butima Yohana Mirumbe na mwenyekiti wa halmashauri ya Musoma vijijini Magina Magesa,walisema ni wajibu wa polisi kuhakikisha inapambana na unyama huo unaendelea katika wilaya hizo hatua ambayo imejenga hofu kubwa kwa wananchi.

Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mara SSP Japhet Lusingu,amekiri kutokea kwa matukio hayo huku akisema jeshi la polisi limejipanga kikamilifu katika kukabiliana na mauji hayo ambayo yameibuka katika siku za hivi karibuni.

Wakati huo huo kaimu kamanda wa polisi mkoani Mara, SSP Japhet Lusingu,amethibitisha kutokea kwa kifo cha Eustace Nyarugenda ambapo amesema tukio hilo limetokea usiku wa Desemba nne katika nyumba ya wageni ya Savana Bar and Guest house mjini Bunda.

Amesema wahudumu wa nyumba hiyo walisikia mtu huyo ambaye ni mwanaharakati wa ABC Foundation la kutetea haki za wanawake na watoto walisikia akikoroma na baada ya kutoa taarifa polisi walivunja mlango na kukuta akiwa katika hali mbaya na baada ya kufikishwa hospitali ya DDH alifariki dunia muda mfupi wakati akipatiwa matibabu.

Chanzo: Mwanaafrika blog
 

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
1,225
Oh GOD.... Save US... Sasa wakibeba KICHWA CHANGU wanakitaka cha NINI??
 

King'asti

JF-Expert Member
Nov 26, 2009
27,813
2,000
17 pple in a month?! Kuuwawa kinyama? Na polisi wanajishangalisha na kufyatulia risasi watoto na waandishi wa habari? Seriously!
 

Naibili

JF-Expert Member
Jan 24, 2011
1,688
1,500
hii nchi ya kipekee sana, watu 17 na hakuna aliyewajibika ni aibu
 

wikolo

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
801
195
Kila kukicha utasikia jeshi limejipanga baada ya matukio kwani huwa limekaa tu bila kujipanga hadi kutokee matukio?

Hapo sasa ndo inashangaza, wao polisi wamejipanga lakini watu 17 wamekufa ndani ya mwezi mmoja. isije ikawa neno kujipanga lina maana nyingine kwao hao polisi!
 

Relief

JF-Expert Member
Aug 6, 2010
255
0
Tulikosea sana pale ambapo form four failures na standard seven leavers walipokuwa wanaingia chuo cha polisi, ndo imechangia tumekuwa na jeshi la polisi la kipumbavu unakuta mkuu wa kituo elimu yake ni la saba, unadhani atakuwa na maamuzi ya msingi au kukaa tuu na kupokea rushwa badala ya kutekeleza na kusimamia sheria na ulinzi wa raia. Jeshi la polisi linahitaji re-structuring, matukio haya ni hatari sana na ya kukatisha tamaa, ....its like been in a house but not a home. JK upo? au unasafiri tuu?:angry:
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,497
2,000
kamanda Barlow aliuliwa akiwa katika shuhuli zake za uzinzi tukaona viongozi wakubwa wa polisi walikimbilia mwanza kuwatafuta wahalifu ila huko Butiama kwa mwezi mmoja wamekufa watu 17 ila tunaskia matamko ya kipuuzi kutoka kwa jeshi la kipuuzi.
Huyu said mwema aliapaswa kujiuzulu na anastahili kupandishwa kizimbani.
Polisi wanafanya kazi kisiasa.
 

Eng. Kayombo

Member
Mar 6, 2012
21
0
Jaman sasa tumefika mwisho inatupasa tufumbuke macho tanzania imeuzwa hivyo tupige chin ccm na kuchagua chadema.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom