Maandamano ya CHADEMA: Aqulina Akwilini Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT apigwa risasi na kufariki; Polisi wakiri kuhusika

Azim Sokoine

JF-Expert Member
Aug 20, 2014
1,379
2,533
Wakati CHADEMA wanaelekea kwenye Ofisi ya Mkurugenzi kudai barua za viapo, polisi walivuruga na kuanza kupiga mabomu zikiambatana na risasi za moto kwa wapenzi na wanachama wa CDM eneo la Mkwajuni.

Kuna polisi alifyatua risasi ambayo ilimlenga mwanafunzi wa mwaka wa kwanza NIT, Aqulina Akwilini risasi iliyomlenga kifuani na kupoteza maisha

Pia soma
- Je, Polisi washitakiwe kusababisha vifo kizembe vya random shootout?. RIP Aqulina Akwilini, Baftaha, She is an Angel!.

- Mauaji ya Akwilina: DPP afunga jalada la kesi baada ya Jeshi la Polisi kushindwa kubaini mhusika wa mauaji

Akwilina.jpg


FB_IMG_1518810255853.jpg

======

Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(DARUSO) imelaani vikali mauaji ya mwanafunzi huyo ambaye mwanzoni alidhaniwa kuwa wa UDSM lakini ikabainika kuwa ni mwanafunzi wa Mwaka wa kwanza Chuo cha Usafirishaji cha Taifa(NIT) kozi ya Procurement and Logistics.


TAARIFA KWA UMMA

Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam(DARUSO) imepokea kwa mshituko taarifa za klfo cha mwanafunzi Aqulina Akwillni Baftaha anayesemekana amepigwa Risasi na Askari wa jeshi la polisi wakiwa wanakablliana na waandamanaji kwa kutumia risasi za moto.

Awali taarifa za Mwanafunzi huyo zilimuhusisha ni Mwanafunzl wa UDSM lakini baada ya uchunguzi wa kina imebainika ni mwanafunzi anayesoma Chuo cha Usafirishajl chaTaifa (NIT) 'course ya procurement and logistics' mwaka wa kwanza.

DARUSO inalaani vikali kitendo kllichotokea na kutumia nafasi hii kulishauri jeshi la polisi kujitafakari kama ni sahihi kupambana na Raia wa Tanzania kwa kutumia Silaha za moto. Ni kitendo cha kinyama na cha kulaaniwa na kukemewa na Kila Mtanzania yeyote bila kujali tofauti zetu kwa sababu hii siyo akisi na misingi ya siasa za nchi yetu.

Pamoja na tofauti zetu nyingi kama vyama dini ukabila na kadhalika, taifa letu limejengwa kwenye misingi ya undugu umoja, mshikamano na sio matumizi ya nguvu kupita kiasi au kukiuka sheria na taratibu za Nchi yetu.

Hivo basi, sisi kama Serikali ya Wanafunzl Chuo kikuu Dar es Salaam (DARUSO) kwa Umoja wetu tunalaani vikali vltendo vya unyanyasaji na ukiukwaji wa Sheria wa aina yeyote ile na tunaomba mamlaka husika ziweze kuwachukulia hatua wahusika na kukemea kwa nguvu zote vitendo vya aina hii.

Mwisho tunatangulita kwa huzuni kubwa salamu zetu za pole kwa Ndugu na jamaa waliofikwa na msiba huu, Pia Uongozi wa Chuo Klkuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

DARUSO-MLIMANI​
UPDATE:
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amekiri kuwa Jeshi la Polisi lilimpiga risasi mtu mmoja jana katika harakati za kutawanya wafuasi wa CHADEMA.

Zaidi, soma => Polisi yakiri kupiga mtu risasi maandamano ya CHADEMA

Viongozi na Wanasiasa wengine waliowahi kupigwa risasi
- Utata kifo cha hayati Abeid Karume

- DODOMA: Tundu Lissu ajeruhiwa kwa risasi, akimbizwa Hospitali

- Simulizi: Kisa na Mkasa wa Mauaji ya Jenerali Imran Kombe (Mkurugenzi Mstaafu wa Idara ya Usalama wa Taifa-TISS)

- Kifo chenye utata cha Waziri Nicas Mahinda

- Wakili mtetezi wa ICTR Prof. Jwani Mwaikusa auawa Tanzania

- TANZIA - Waziri Salome Mbatia afariki dunia, maswali yaibuka!

- Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka ashambuliwa kwa risasi na Watu wasiojulikana

- Askari polisi aliyepigwa risasi na majambazi Tanga afariki
 
Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na awape nguvu, subira na faraja Wazazi wake, ndugu jamaa na marafiki.

Serikali hii dhalimu imekatisha tena uhai wa Mtanzania mwingine asiyekuwa na hatia yoyote ile.
 
Imekua kawaida ya huyu mwenyekiti wa chadema kuanzisha fujo kwa kisingizio cha kudai haki bila kufuata sheria, fujo hizo akiziratibu nje ya mkoa anakozaliwa, kumbukumbu zinaonyesha, huziratibu mikoa ya Mbeya, Mwanza, Dar ,hili halikubaliki hata kidogo, serikali na vyombo vya dola waliangalie hili kwa jicho la tatu, huyu anaharibu shughuli za kiuchumi za maeneo mengine akiiacha Kilimanjaro salama.
Vurugu zake akazianzie Kilimanjaro Kama kweli kadhamilia.
hata MAKONDA NA MZEE BABA WANAIHARIBU DAR , nadhani tuwarudishe Mwanza siyo?
 
Imekua kawaida ya huyu mwenyekiti wa chadema kuanzisha fujo kwa kisingizio cha kudai haki bila kufuata sheria, fujo hizo akiziratibu nje ya mkoa anakozaliwa, kumbukumbu zinaonyesha, huziratibu mikoa ya Mbeya, Mwanza, Dar ,hili halikubaliki hata kidogo, serikali na vyombo vya dola waliangalie hili kwa jicho la tatu, huyu anaharibu shughuli za kiuchumi za maeneo mengine akiiacha Kilimanjaro salama.
Vurugu zake akazianzie Kilimanjaro Kama kweli kadhamilia.
Mkoa wa kilimanjaro ccm wenyewe wanauelewa ndio maana kule hawajisumbui wanajua hawatapata kitu
 
Back
Top Bottom