Picha: Mtoto wa miaka saba aachiwa mtoto mchanga na mwanamke asiyejulikana mbeya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
SATURDAY, DECEMBER 8, 2012

MTOTO WA MIAKA SABA AACHIWA MTOTO MCHANGA NA MWANAMKE ASIYEJULIKANA MBEYA



Mtoto Sharifu huyoo wa darasa la pili shule ya msingi Mbata akiletwa na wenzake kuja kuzungumza na waandishi wa habari waliokwenda kumtembelea shuleni hapo ili kujua kisa kilichomtokea mpaka akaachiwa mtoto

Kazi kweli kweli watoto wakimwimbia wimbo wa kumtania sharifu kuwa kapakaziwa mtoto
Kwakweli tulikuta watoto wa shule ya msingi Mbata wamechangamka sana na kutupokea vizuri
Sharifu huyo katikati jamani sasa mwachieni tunashukuru kwa kutuletea tuongee nae
Rafiki yetu sharifu tayari wenzake wamemwachia na anaanza kutupa kisa cha kuachiwa mtoto mchanga

Sharifu 7 amesema yeye alipokua anatoka shule mida ya saa nne asubuhi kuna mama alimwita huyo mama alikuwa amebeba mtoto mchanga na ndipo mama huyo akamwambia sharifu naomba nisaidie kumbeba mtoto kwani nimesahau kuchukua kitu fulani nyumbani


sharifu bila kujua akamchukua mtoto huyo na mama wa mtoto akaondoka sharifu anasema ilipita muda mrefu sana bila ya kumuona tena mama huyo na mtoto huyo alianza kulia na sharifu kuona mtoto analia nayeye akaanza kulia
Ndipo akatokea mwanafunzi huyu na kumuuliza sharifu mbona unalia na mtoto analia? sharifu akamjibu mwanafuzi mwenzake kuwa kuna mama kaniachia mtoto toka saa nne mpaka sasa sijamwona mama huyo nae nami nimechoka kumbeba ndipo mwanafunzi huyo akamwambia twende tumpeleke kwa walimu
Upendo Mwakipunda mwalimu wa shule ya msingi mbata amekiri kutokea kwa tukio hilo kweli walimpokea mtoto huyo na kumpeleka kituo cha polisi
Tukiwa na mtoto sharifu baada ya kuongeanae habari kamili ya tukio hili tutawaletea jumatatu mara baada ya kufuatilia polisi na hospitali ya rufaa Mbeya
Kwa ujumla baada ya kumaliza maongezi tulianza kuona jinsi watoto wakiwa katika michezo mbalimbali shuleni hapo dogo katulia dirishani mwa darasa lake huku akipata embe kwa raha zake

Wengine madirishani wengine wanachora ukuta ni furaha tu shuleni hapo

Wa kuruka kamba haya wa kucheza mpira sawa
Wanafunzi wakifurahia chandarua walichobuni shuleni hapo

Wakifurahia kutembelewa shuleni kwao
Picha na mbeya yetu
 
Masikini SHARIFU sasa Miaka 7 ana MTOTO? Itabidi atafute kazi KUMLEA KITOTO HICHO.... LOL
 
At least huyo kafanya hivyo lkn mbaya ni wale wanaowatupa majalalani au vyooni na maeneo mengine ambayo hatujayajua bado! MUNGU ingilia kati hali!!!!!
 
huyo dogo ni Mwanamme.Bg up Dogo Sharif.Unafikiri ni raic kiivyo mtoto kukubali kubeba mtoto ambaye hamfahamu?Second,Why awe Sharifu na acwe Ali o Asha?Na huyo mtoto aliyeachiwa ni njisia gan?Itz lyk Magic.Huyo dogo atakuwa na uzao kama Mfalme Daudi.itz ma view.Hongera Dogo Sharifu.Na dogo aliyeachiwa akue cku moja mkutane.Na wewe Mama uliyefanya hivyo either kwa makusud o kujisahau,Usamehewe kwa sabb ni maajilio lakn Mungu azidi kukupa Uhai Zaidi huyo mtoto uliyetelekeza Cku moja awe msaada kwako.
 
picha ya huyo mtoto mdogo aliyeachiwa sharifu ipo wapi?
taarifa nyingine za huyo mama mtoto zipo wapi?
 
Back
Top Bottom