KIJOME
JF-Expert Member
- Jun 7, 2012
- 3,084
- 732
Baada ya uwasilishaji wa bajeti ya sirikali jioni hii mtangaji wa TBC alikuwa akiwahoji wabunge mbalimbali kuhusu maoni yao juu ya bajeti hii.
Katika pita pita yake kakutana uso kwa uso na Kamanda wa anga Mh.Freeman Mbowe na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:
Mtangazaji: Mheshimiwa unaonaje kuhusu bajeti hii ya sirikali ya magamba na nini maoni yako?
Kamanda Mbowe: Bajeti hii haina jipya kama ilivyo kawaida na wabunge wa chama cha mapinduzi wamekuwa wakishangilia sana bajeti bajeti hii ambayo haina chanzo kipya cha mapato zaidi ya ya vile walivyozoea kama sigara,bia,mvinyo,mafuta na ushuru wa magari wakati sekta kama madini, utalii na vinginevyo vikiachwa au kuonekana vinachangaia kidogo sana pato la taifa.
Kwa mfumo huu hali ni ngumu sana na haiwezi kumkomboa mwananchi wa kawaida.....
Wadau angalieni vizuri hiyo picha na nimemuona kama mtangazaji anataka kukimbia kwa nondo zile alizoshusha kamanda na alichanganyikiwa ghafla magamba yakiambiwa ukweli...huu utumwa mpaka lini tibisisiem?
Nawasilisha kwa maoni zaidi.....