Picha: Mtangazaji wa TBC1 uso kwa uso na KUB

KIJOME

JF-Expert Member
Jun 7, 2012
3,084
732
attachment.php

Baada ya uwasilishaji wa bajeti ya sirikali jioni hii mtangaji wa TBC alikuwa akiwahoji wabunge mbalimbali kuhusu maoni yao juu ya bajeti hii.

Katika pita pita yake kakutana uso kwa uso na Kamanda wa anga Mh.Freeman Mbowe na mahojiano yalikuwa kama ifuatavyo:

Mtangazaji: Mheshimiwa unaonaje kuhusu bajeti hii ya sirikali ya magamba na nini maoni yako?

Kamanda Mbowe: Bajeti hii haina jipya kama ilivyo kawaida na wabunge wa chama cha mapinduzi wamekuwa wakishangilia sana bajeti bajeti hii ambayo haina chanzo kipya cha mapato zaidi ya ya vile walivyozoea kama sigara,bia,mvinyo,mafuta na ushuru wa magari wakati sekta kama madini, utalii na vinginevyo vikiachwa au kuonekana vinachangaia kidogo sana pato la taifa.

Kwa mfumo huu hali ni ngumu sana na haiwezi kumkomboa mwananchi wa kawaida.....

Wadau angalieni vizuri hiyo picha na nimemuona kama mtangazaji anataka kukimbia kwa nondo zile alizoshusha kamanda na alichanganyikiwa ghafla magamba yakiambiwa ukweli...huu utumwa mpaka lini tibisisiem?

Nawasilisha kwa maoni zaidi.....
 
Attachments

  • cap00012.jpg
    cap00012.jpg
    28.2 KB · Views: 4,565
Nimecheka sana, maana yule mtangazaji hakuyategemea hayo na baada ya Mbowe kuanza kutiririka uso wa mtangazaji ulionyesha kabisa hofu na kujilaumu kwa nini kamhoji. Kwa jinsi hali ilivyo TBCCM lolote laweza kumpata yule mama kwenye ajira yake. Ndio asili ya hofu yake.
 
ushabiki usiokuwa na maana. simuoni kama anataka kukimbia.
Huwezi kumuona kwa sababu na wewe ni wale wale!!!!Pole sana dada kibarua kitaota nyasi shauri ya kunyenyekea magamba....
 
Hajataka kukimbia ila alikuwa anamsaidia mh mbowe atizame camera vzr maana macho ya mh yote ni ya kushoto ni taabu sana kwa digital camera kupata picha nzuri
 
Hajataka kukimbia ila alikuwa anamsaidia mh mbowe atizame camera vzr maana macho ya mh yote ni ya kushoto ni taabu sana kwa digital camera kupata picha nzuri
Una ugonjwa unaoitwa UKIKI....ukitaka kirefu chake niulize baadae...
 
Hajataka kukimbia ila alikuwa anamsaidia mh mbowe atizame camera vzr maana macho ya mh yote ni ya kushoto ni taabu sana kwa digital camera kupata picha nzuri

acha kejeli bwana mtangazi alikua anataka kusepa hadi anamkatisha bwana.
 
Kuna mambo ya siasa na kiutaalamu,mwenye kufahamu taaluma ya Mbowe kwenye masuala ya uchumi atujuze.Usikute bajeti inasomwa yeye haoni kitu.
 
Yani huyu madam, alikuwa anataka kuondoka lakini anakumbuka makombora ya CHADEMA dhidi ya TBC1 akawa anashindwa anafanye nini, maana kamanda Mbowe alishusha nondo za ukweli sana juu ya hii bajeti. Alitegemea wabunge wote wataifagilia kinafiki.
 
Nimeshangaa kumbe hata wabunge wanapenda kuhojiwa kama watoto wa shule. Yaani wanasimama pembeni ya mwandishi kusubiri kuhojiwa
 
Zisome sms zao.............
Mshana ''kwa kumuhoji Mbowe umeivua nguo bajeti,unatakiwa ufike ofisi za TBC Dodoma kwa ajili ya mahojiano ya kina''
Mdada- ''sawa bosi ila sikujua kama ni Mbowe, nimekuja kushtuka tayari keshafunguka''
 
Kuna mambo ya siasa na kiutaalamu,mwenye kufahamu taaluma ya Mbowe kwenye masuala ya uchumi atujuze.Usikute bajeti inasomwa yeye haoni kitu.
Mkuu Mingoi Mbowe anauwezo mkubwa kuliko mawaziri wengi wa serikali hii ingawa hana uzoefu wa kuongoza wizara. Najua huwezi/hamuwezi kukubali ila huo ndio ukweli. Angalia alivyo weza kuongoza kambi ya upinzani mpaka Bunge sasa linaonekana kama bunge la wananchi licha ya mizengwe wanayofanyiwa.
 
Last edited by a moderator:
Ushauri kwa TBC pesa walizoongezewa wawajengee uwezo watanganzi wao ili kumudu kazi yao katika mfumo wa mawazo kinzani. Yule mama alionyesha mshituko wa wazi wachangiaji waliposema kinyume cha matarajio yake. Attachment ya muda mfupi BBC itasaidia kuwajengea ujasiri.
 
Mkuu Mingoi Mbowe anauwezo mkubwa kuliko mawaziri wengi wa serikali hii ingawa hana uzoefu wa kuongoza wizara. Najua huwezi/hamuwezi kukubali ila huo ndio ukweli. Angalia alivyo weza kuongoza kambi ya upinzani mpaka Bunge sasa linaonekana kama bunge la wananchi licha ya mizengwe wanayofanyiwa.
Unasumbuliwa na ugonjwa wa mahaba binafsi na hauna tiba.

Back
Top Bottom