Picha: Mrembo wa Kitanzania aliyekamatwa na heroin China

EMT

Platinum Member
Jan 13, 2010
14,483
15,308
Mwanamke wa Kitanzania mwenye umri wa miaka 28 amekamatwa na kilo 1.1 za dawa za kulevya aina ya heroin huko Macao. Dawa hizo zilikutwa tumboni mwake baada ya kushtukiwa na kufanyiwa X-ray ambapo alikutwa na jumla ya vidonge 66 vyenye thamani ya dola za Kimarekani 137,720.

Mwanamke huyo alikuwa akisafiri kutoka Thailand akielekea Macao Jumanne iliyopita. Aliwaambia polisi kuwa alikuwa anaelekea Guangzhou ambao ni mji wa jimbo la Guangdong huko Chima.

Pichani ni mwanamke huyo wa Kitanzania (akiwa amefunikwa uso) aliyekamatwa na kilo 1.1 za heroin huko Macau. Hapo amepigwa picha na vidonge vyake kwenye press conference huko Macau, Disemba 19, 2013.

Ok kwa wale walokuwa wakilalamika 'habari nusu nusu' huyo binti anaitwa Jackie Cliff. ..appeared in Diamondz Nataka Kulewa. Was a runners up or something kwenye Miss Tz huko nyuma.




a3853fb3862d450baca5a4282c0c0d81.jpg


Polisi wakichunguza vidonge ambavyo huyu mrembo alikuwa amevimeza.

fe5c726676e94e5fadbe9356a9ec599f.jpg



Waandishi wa habari wakipiga picha vidonge vya heroin alivyokamatwa navyo mremboi huyu wa Kitanzania.

0f5d40554df94bcb9c99d45b4ef29b6a.jpg


Kila pipi unayoiona hapo katika picha ina gross weight ya10 grams!

Heroine iliyofungwa ndani ya kila pipi huwa na ugumu kama chaki au udongo ule wanao kula kina mama hasa wakiwa wajawazito, nikiwa na maana kuwa haiwi katika mfumo wa unga! Baadae ndio husagwa na kuwa kama unga!

Hapo unapo iona kwa ndani hiyo pipi moja, unga (unga) wake umezungushiwa nylon gumu kabisa, kisha inazungushiwa soltepu nyingi ya kutosha....na mwsho (kwa nje) wanafunga kwa kutumia vidole vya kwenye gloves kwa umahiri mkubwa sana! Kwahiyo, hiyo cover ya nje tunayoiona ni gloves!

Kama mzigo ni mkubwa, huwa (haupigiliwi)...kuingiza kutumia tundu la haja kubwa bali humezwa taratibu na kwa siku mbili tatu! Punda anameza pisi kadhaa, anatoka nje kutembea tembea nadhani ili mzigo ushuke, kisha akijisikia poa, anarudi tena ndani anameza tena kidgo kidgo...hivyo hivyo, kwa kadri ya uwezo wake! Kwa hali hii, watu hutofautiana kwa uwezo wa kubeba mzigo.......na mara nyingi watu wembamba humeza kiasi kikubwa sana!

Hali kadhalika wakati wa kushusha mzigo, nayo huchukua hata siku tano kama ilivyo wakati wa ubebaji! Leo ana k.nya 10, badae tena kidgo, kesho tena hivyo hivyo....na kuna wakati mtu anakaa siku kadhaa ndani, kisa ni kuwa pipi mbili au tatu zimegoma kutoka! Katika zoezi hili, punda....hushushia huu mzigo ndani ya nyumba chumbani na sio chooni....tena juu ya gazeti au karatasi....halafu watu wanapembua kutoka kwenye m.vi na kuosha kisha kumenya ili kuondoa vifungashio tayari kwenda sokoni!

Zoezi hili huwa halifanyiki katika makazi ya Punda! Linatafutwa chimbo hasa la maana, na punda anakata mawasiliano karibu na watu wote, lakini hubakia na namba fulani au ya mtu kwa ajili ya kuwasiliana na watu wake maalumu!

Moja ya tabia kuu ya Punda hawa ni kupoteza hati ya kusafiria (passport) mara kwa mara! Hii ni kwa sababu ya kuficha nchi alizotembelea na hasa zile zenye sifa ya kuzalisha haya madawa!

Mimi sio afisa uhamiaji na wala sijasomea hiyo mambo, lakini natambua kuwa visa ya nchi zenye mfumo wa kubandika i.e (stika).....huwa zinabandikwa upande wa kulia wa Ppt than wa kushoto! Kwa mfano hii passport yetu ya Tanzania...visa huwa zinabadikwa zaidi kuanzia page namba 3, 5, 7 hadi 45 (kwa uelewa wangu endapo nafasi zipo wazi!) Lakini Passport za Punda huwa unaweza kukuta viza za nchi fulani TOFAUTI imebandikwa page namb 2 na nchi nyingine page namb 3, wakati ppt ina page kadhaa zilizo wazi!.........Hapa nataka kufafanua kuwa, kisa cha kufanya hivi ni ili kufunika mihuri ya entry na exit ya nchi fulani....ili maafisa katika any point of entry wasitilie shaka wapi Punda alishwahi kupita! Hizi viza fake za nchi zingine huwa ni ama viza (washed) iliofutwa na kuchapwa upya ama zilizo tokana na scan ya viza.....na ambapo Punda hatowahi kwenda hizo nchi kwa kutumia hiyo ppt!

Sifa ya elimu ya Punda 90% ya idadi yao hakuna aliyevuka A level, na kama alishawahi kufika chuo, basi alifukuzwa kabla ya kumaliza! Na popote Punda atakapo kuwa anaishi, lakini ni lazima awe na marafiki wa Magomeni, Kinondoni, Kariakoo na baadhi ya maeneo ya Ilala na Tandika....mara moja moja nyakati za usiku lazima aende huko!
 
Ni bahati mbaya tu hiyo ,ajali kazini msivunjike moyo .


[h=1]Tanzanian woman nabbed for body-smuggling 1.1kg of heroin[/h] 2013-12-20 01:41:28 GMT2013-12-20 09:41:28(Beijing Time) SINA English



(1/3)(Photo: ecns.cn)


  • U158P5029DT20131220094104_h60.jpg
  • U158P5029DT20131220094106_h60.jpg
  • U158P5029DT20131220094108_h60.jpg




A 28-year-old woman from Tanzania was arrested at Macau airport as the security found over 1.1kg of heroin (valued at over 1.1 million pataca) in her body, which would be smuggled to S China's Guangzhou city. This is the third case this year involving drug traffickers of Tanzania nationality.
 
Tunapeleka watoto wetu shule ili wapate elimu,si tu iwasaidie waweze kupata kazi nzuri na kuwapa maisha mazuri, bali pia kuwaongezea ufahamu na kuwaondolea balaa la kuwa gizani. Waache kushawishiwa na vitu vya kupita kama hivi.

Siwalaumu hawa mabinti, lakini kikwazo kikubwa kwao kwenye hizi biashara zao ni ukosefu wa elimu,ukosefu wa ufahamu,kuona kuwa wale wanaowashauri ni majuha kwa kuwa tu wamewazidi kipato.

wengi kwa nyakati tofauti wanajaribu sana kuwatahadharisha hawa waache huu upuuzi wao,lakini kutokana na ujinga wa hawa mabinti huwa hawaelewi wanachoelezwa.hakuna kitu kibaya kama mjinga asiyetaka kujifunza.kuna kibabu kimoja kiliwaita wajinga wa aina hii w**umbavu.
 
Back
Top Bottom