barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,726
- 32,818
Misa hiyo inaongozwa na Askofu Isaac Amani wa Jimbo la Moshi akiwa pamoja na Askofu Mkuu Josephat Louise Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha na Askofu Roghat Kimario wa Jimbo la Same pamoja na Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu Padri Amandus Kapele.
Wengine wanaishiriki Ibada hiyo ni Mapadri wa shirika hilo na Mapadri wa Jimbo la Arusha,Moshi, Same na Mbulu;wakiwa pamoja na Watawa wakike na wakiume na Walei mbalimbali.
Kwa heri Padre Babu...Ulikuwa na msemo wako maarufu sana,kila mtu alipokuwa anakuuliza,haya yote unajenga na kuyasimamia nani atayafaidi siku ukifa?Ulijibu " Life is more than just being alive",Kwako kufa sio mwisho wa maisha...Hakika leo umezikwa,lakini utaendelea kuishi.Miaka 99 sio mchezo.Sisi wanafunzi wako tutakukumbuka daima.
Padri Babu;Pumzika kwa Amani Mpendwa wetu.Ulivipiga vita vilivyo vigumu,na mwendo umeumaliza...Ulale Pema Peponi!!