Picha: Misa ya mazishi ya Padre Babu Arusha leo hii

barafu

JF-Expert Member
Apr 28, 2013
6,726
32,818
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
image.jpeg
Hali ilivyokuwa katika viwanja vya Seminari ndogo ya Usariver Jimbo Kuu Katoliki la Arusha, palipofanyika Ibada ya Misa Takatifu ya Kumsindikiza Fr JOSEPH BABU maarufu kama Fr Babu, katika Safari yake ya Mwisho hapa duniani.

Misa hiyo inaongozwa na Askofu Isaac Amani wa Jimbo la Moshi akiwa pamoja na Askofu Mkuu Josephat Louise Lebulu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha na Askofu Roghat Kimario wa Jimbo la Same pamoja na Mkuu wa Shirika la Roho Mtakatifu Padri Amandus Kapele.

Wengine wanaishiriki Ibada hiyo ni Mapadri wa shirika hilo na Mapadri wa Jimbo la Arusha,Moshi, Same na Mbulu;wakiwa pamoja na Watawa wakike na wakiume na Walei mbalimbali.

Kwa heri Padre Babu...Ulikuwa na msemo wako maarufu sana,kila mtu alipokuwa anakuuliza,haya yote unajenga na kuyasimamia nani atayafaidi siku ukifa?Ulijibu " Life is more than just being alive",Kwako kufa sio mwisho wa maisha...Hakika leo umezikwa,lakini utaendelea kuishi.Miaka 99 sio mchezo.Sisi wanafunzi wako tutakukumbuka daima.

Padri Babu;Pumzika kwa Amani Mpendwa wetu.Ulivipiga vita vilivyo vigumu,na mwendo umeumaliza...Ulale Pema Peponi!!
 
Utamaduni wa kikanisa wa kuzika ndani ya Kanisa ni kwa ngazi ya Maaskofu,Kardinali na Papa
Mapadre huzikwa ktk eneo maalumu ambalo jimbo huwa wamejiwekea
Mkuu ninaelewa hili lakini wale watoto watatu wa Fatima wote wamezikwa ndani ya kanisa.
 
Back
Top Bottom