Picha, miongoni mwa scene za bongo muvi kuwahi kutokea

Kajolijo

JF-Expert Member
May 30, 2016
3,364
4,612
Hapa ni jambazi akimvamia mtu nyumbani kwwake ila kabla ya kuingia alivua kwanza viatu na kuviacha mlangoni halafu akaingia kufanya mashambulizi.
3ac931ea8675b61045e0f725e73fdd91.jpg
Mimi ata bure hizi muvi sitizami wallah.
 
Hahhaaaaa hii ndio bongo bana nchi yenye maajabu mengi mungu tupe maarifa tu wanao tunaangamia
 
Ni kama vile kuangalia TBC kile kipindi cha watoto Bongo Kids.
Balaa kabisa,
Yaani Mfungua geti lazima awe mtambo au chizichizi hivi
Jambazi lazima avae nyeusi
Lazima kuwe na scene ya kitandani au supermarket au Saloon
Wanawake lazima wavae vinguo vifupi
Scene inakwambia miaka mitano nyuma, lakini rangi ya kucha, wig ni lile lile la miaka ya sasa
 
Bashite ameamuru lazima tununue hizo tuu,hakuna cha Jumong au Prison Break wala Legend of the seeker
 
Bashite ameamuru lazima tununue hizo tuu,hakuna cha Jumong au Prison Break wala Legend of the seeker
Labda afunge internet maana zinadownloadika kirahisi. Bongomovie siwezi kununua wala kukodi.
Lakini mi najiuliza hawa actors wa bongo hawaangalii actors wa nje kama America?
Mbona hawaigi??
Maana mi hata nikijitia kiburi kuangalia bongo movie ndani ya dakika ya pili nakuwa nshaikinai wanavyoongea.
 
Kuigiza katika maisha hali ya juu kwelikweli, wakati hata milo mitatu tu wengine inawasumbua.
Yaani mtu unaangalia kitu na unabaini wazi kabisa hiki kitu ni cha uongo, hakina uhalisia kabisa
 
Usanii Bongo ukijua kuongea na kuwa mtu maarufu kidogo basi we ni actor.

Mwanaume uwe na Sura nzuri sana, Pia uwe na Sura mbaya sana ukae getini.

Mwanamke uwe umenyea ushuzi haswa hata kama mjuso wa kubabia babia ndio ujiulize kunyea ushuzi {{Kund..}} na usanii wapi na wapi.

Msanii zoezi lake kubwa ni kujipiga self tu.
 
Hapa ni jambazi akimvamia mtu nyumbani kwwake ila kabla ya kuingia alivua kwanza viatu na kuviacha mlangoni halafu akaingia kufanya mashambulizi.
3ac931ea8675b61045e0f725e73fdd91.jpg
Mimi ata bure hizi muvi sitizami wallah.

Unakuta kuna scene pengine inaonesha miaka 20 iliyopita labda character alipokuwa mdogo cha ajabu magari hayo yanayopita katika hiyo scene ya miaka 20 iliyopita yana namba TXXX 123 ambazo ni namba za sasa sisi tulitegemea TZA,TZB,TZC halafu gari zenyewe zinazopita ni passo,raum na nyinginezo ambazo zimetoka miaka ya karibuni.



Kingine sote tunaelewa bunduki inapotoa wakati huo na risasi imeshafika kwenye target wenzetu bongo movie inaanza risasi kisha mlio.Halafu damu za majeruhi utafikiri rangi ya vodacom
 
Hawa bongo movie kwanini wasitafute mashamba walime nyanya na pilipili hoho kama Bushman2 the great. Wanahangaika na maandamano wakati kuigiza hawawezi.
 
Back
Top Bottom