rumplelstiltskin
JF-Expert Member
- Jul 27, 2020
- 214
- 307
Hii picha hapa inaelezea mifumo yetu ya elimu watakao ielewa comment hapo
Wapo we subir utaonakama kuna mtu hatoielewa ana shida
Uko sawa hili swala inabid liangaliweMfumo wetu wa elimu unasikitisha
Mwalimu anafundisha wanafunzi 60 katika darasa moja.
Kwa njia moja tu ya ufundishaji.
Kila mwanafunzi katika lile darasa ana mahitaji yake,uwezo wake,ndoto zake,strength yake na weakness yake.
Na kila mwanafunzi anaelewa kwa nija tofauti wengine kupitia nyimbo wengine simulizi wengine kupitia meditation.
Lakini mwisho wa siku uelewa wao unapimwa kwa mtihani mmoja. mmoja
Mfumo wetu wa elimu unaua ubunifu kwa watoto.
Watoto wanakariri na kumeza material kwa ajili ya kufaulu mtihani na baada ya mtihani wanasahau.
Utaonekana una akili shuleni endapo tu utafanya vizuri darasani.
Lazima tujiulize Why C students are more successful than A students in the real world today...
😂😂😂Hapo maskini karunguyeye, ameonewa sana, sijui itakuwaje? Nyani anashangilia mtihani ulivo rahisi, Kipepeo daa! kamependelewa sana, kwake kama kumsukuma mlevi huo mtihani atapita kirahisi mno, Nyoka anamsanifu mwlm kimoyoymoyo, kitu ubua tu huo.
Ngoma iko kwa Simba anatamani but mpaka roho inamuuma, atafanyaje?, Mamba wa watu ndo kabisaaa msindikizaji atajirudia zake majini. tembo anajiuliza kwa ukubwa wake huo atazarauliwa sana akishindwa hapo kuna mawili auvuruge mti, na kukatakatamajani au ajiue.
Kuna makundi ya watu wa aina hizi Duniani wengine ni kina karunguyeye na wenzake, wengine kipepeo na wenzake mwalimu ametoa kitu (Mtihani) bila kujali hali zao. wazi nyani na wenzake wamependelewa! nauliza sasa Elimu yetu kwani ni ya upendeleo?