PICHA: Mbunge Steven Ngonyani akipiga magoti kumuombea kura mgombea wa CCM, Maulid Mtulia

Kweli tuko mbali. CCM, jaribuni basi kuwaaminisha wananchi kuwa hayo myasemayo mtayafanya. Nilimsikiliza Kibajaji, nikajiuliza; Hili ndilo tutakalo wafanyia wana Kinondoni kweli?? Kuwadharau wazee kwa sababu ati wamezeeka na hawajui hata kutembea?? Kilichoniumiza zaidi; Nikasikia vigelegele na sauti za kike. Nkajua; Weshakula pilao hao.
Haya, Mtulia anasimama anasema; Mkinichagua, ntawajengeeni magorofa pale Magomeni mkakae humo!!! Shit! Tutakaa humo wangapi?? Je, tusipokuchagua inamaana serekali haijali hata huo mtaji waliowekeza humo hata sasa??
Mkuu wa mkoa naye anasema msipoichagua ccm hampati maendeleo. Najiuliza, ccm imeanza leo hii au miaka 50+ iliyopita?? Sasa wamekuja hawa majuha, Waziri mzima unaenda kupiga magoti kuwaomba ccm wenzako kura kwa ajili ya aliyeukataa ugali mnamshurutisha kuula tena. Shame on yuuuu.
Mngeleta mwingine hata mngelimrudisha Iddi mkamsafisha skendo ya Ngada nadhani mngelikuwa na kitako (Base) sio huyu. Mmeshapotea msiendelee kujidhalilisha. Japo twajua LAZIMA apite. Lakini, hamna uwezo wa kumnadi
 
Lazaro Nyalandu alipojiuzulu ubunge japokuwa alijiunga na team Ufipa lakini hakutaka kuwapa adhabu akina Msigwa na Mdee kwenda kupiga magoti na kugalagala majukwaani kumuombea kura. Mwanaume anapopiga magoti kuomba kitu ni ishara ya majuto na kujiona " usiyestahili". Hivyo pamoja na mapungufu yote ya Nyalandu lakini katika hili la kutogombea tena Mungu alimpa macho ya rohoni, nampongeza. Ni hayo machache, ahsante!
Unajuaje km asingegombea kama wasingesusia?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom