PICHA: Mbunge Kirufi (CCM, Mbarali) ataka kuvuruga mkutano wa CHADEMA Mbarali

Chadema Diaspora

JF-Expert Member
Oct 25, 2010
481
1,000
Mbunge Kirufi (CCM, Mbarali) ataka kuvuruga mkutano wa CHADEMA Mbarali

Mkutano wa CHADEMA ulio fanyika leo Mei 28, 2014, wilayani Mbarali ukiwa na agenda zifuatazo uliingia dosari pale Mbunge wa Mbarali Mh. Kirufi alipo itisha mkutano eneo hilo hilo ambalo CHADEMA ilibidi wafanye mkutano wao. Ikumbukwe kuwa CHADEMA ilitakiwa kufanye mkutano Mei 25, 2014, lakini polis walizui kwa madai kuwa intelejensia sio nzuri na wakasogeza mkutano siku ya leo Mei 28,2014

Agenda za mkutano zilikuwa kama zifuatazo
-Ushuru ulio pitishwa na madiwani wa CCM wa gunia la mpunga
-Katiba na UKAWA
-Taarifa ya CAG juu ya ubadhirifu wa Billion mbili na million mia nne (2 billion na million 400) fedha za halimashauri

Mkutano huu ulio kuwa ukiongozwa na mwenkiti wa CHADEMA wilaya, Ndg. Peter Mwashiti, na kuhudhuriwa na Madiwani wote wa CHADEMA wilayani Mbarali uliingia dosari na kuchelewa kuanza pale ambapo Mbunge wa Mbarali Mh. Kirufi alivyo itisha mkutano eneo moja karibu na mkutano wa CHADEMA.

Uongozi wa CHADEMA wilayani Mbarali ulipo ona Mbunge huyo kaitisha mkutano; ulienda polis na kuonana na OCD kuomba kibali cha uhalali wa Mbunge Kirufi kufanya mkutano siku moja na eneo moja la mkutano wa CHADEMA. OCD aliomba apewe muda na uongozi wa CHADEMA ili aongee na RPC. Baada ya maongezi ya muda mrefu na RPC, OCD alikili kuwa Mbunge kirufi alikuwa afanye mkutano wake siku nne zilizopita, Mei 24, 2014 na hana uhalali wa kufanya mkutano siku ya leo.

Baada ya majadiliano hayo, OCD alitoa amri kuwa Mbunge Kirufi asitishe mkutano wake. Mh. Kirufi alitii amri hii na CHADEMA iliendelea na mkutano wake kama kawaida. Mkutano wa CHADEMA ulimalizika kwa amani na wanaMbarali wakiwa wamepata muongozo juu ya UKAWA, ushuru wa gunia na ubadhirifu wa billion mbili na million 400.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Wilayani mbarali Ndg Peter Mwashiti anatoa shukrani za dhati kwa wote walio hudhuria mkutano huo.


SAM_2102.JPG
SAM_2097.JPG
SAM_2120.JPG
SAM_2096.JPG
2_SAM_2098.jpg
SAM_2094-2.JPG
SAM_2089.JPG
diwani.jpg
Source: CHADEMA DIASPORA : Mbunge Kirufi (CCM, Mbarali) ataka kuvuruga mkutano wa CHADEMA Mbarali
 

C Programming

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
2,957
2,000
daaa aisee nimeamini chadema ya sasa ni tofauti na ile ya 2010.....??

populations attendance tuu katika mikutano .....inaleta majibu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom