Picha Matukio Ludewa - Filikunjombe apitiliza matarajio ya wengi

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
DSCF5292.JPG
DSCF5265.JPG

Paroko wa kanisa la Roman Katoriki (RC) parokia ya Lupingu Ludewa Thobias Mgani akionyesha fedha kiasi cha shilingi milioni 1.8 kilichotolewa na mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa ajili ya kuunga mkono jitihada za mkazi wa Lupingu Deo Ngalawa aliyejitolewa kujenga chuo cha ualimu katika kata mwambao wa Ziwa nyasa ili kupunguza tatizo la uhaba wa walimu

DSCF5084.JPG
DSCF5066.JPG


Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akimlisha chakula mtoto yatima wa kituo cha Lupingu jana kabla ya mkesha wa Krismas
DSCF5093.JPG
DSCF5094.JPG


Picha kushoto:

Mwanahabari wa ITV Vedasto Msungu akijumuika na mbunge na wanahabari wengine kula chakula na yatima kama njia ya kujenga upendo zaid

Picha Kulia:
Diwani wa kata ya Lupingu kupitia chama cha TLP na mbunge wa jimbo la Ludewa (kulia) wakila chakula na yatima


DSCF5031.JPG
DSCF5019.JPG


Mbunge wa jimbo la Ludewa akicheza ngoma ya kihoda na wasanii wa kundi la Kihoda Lupingu Ludewa

DSCF5036.JPG


Wasanii wa kundi la Mdanga katika kata ya Lupingu wakimzawadia zawadi ya ngoma mbunge wao.
DSCF5256.JPG

 
Afadhali yako Deo,umeamua kwenda kijijini na sio kijichi kwako,wananchi wanapenda viongozi wanao share nao mambo yanayowazunguka
 
Wanasiasa bana hapa ndo wanapokera sana, hana nia ya dhati uyu sharobalo wa kihehe, sasa mpaka apigwe picha na azisambaze uyu ni nyamisifa pia nyamiujiko..
 
Wanasiasa bana hapa ndo wanapokera sana, hana nia ya dhati uyu sharobalo wa kihehe, sasa mpaka apigwe picha na azisambaze uyu ni nyamisifa pia nyamiujiko..

Sawa huyu sifa na kama ulivyosema hapo juu.Je,wa kwako (m-bunge) hata kama hataki sifa (siamini) na hayo mengine amefanya nini hasa kwa watoto yatima?
 
Afadhali yako Deo,umeamua kwenda kijijini na sio kijichi kwako,wananchi wanapenda viongozi wanao share nao mambo yanayowazunguka

Wachache wanaweza kufahamu hili, Filikunjombe X-mass ameenda kijijini kusikofikika kirahis ambako hata mawasiliano ya simu shida, na si kijijini alikozaliwa bali kule karibu alikotoka hayati Kolimba. Kolimba katika maisha yake licha ya kuzaliwa huko hakufanya chochote hadi Deo ndio ameamua kuwaona watu wale. Na kabisa kuamua kula na yatima badala ya kwenda starehe Dar kama wabunge wengine wanavyotumbua kwenye mahoteli ya kitalii.
 
Sawa huyu sifa na kama ulivyosema hapo juu.Je,wa kwako (m-bunge) hata kama hataki sifa (siamini) na hayo mengine amefanya nini hasa kwa watoto yatima?


Joseph Mungai naye afaya aliyofanya Doe Filikunjombe
Huyu naye tunampongeza kwa moyo wa kuwajali watoto hawa ambao kwao leo imekuwa faraja kubwa ambayo ni kumbukumbu tosha kwao.

100_4682.JPG
100_4679.JPG
100_4684.JPG


FAMILIA ya mkandarasi maarufu mkoani Iringa Geofrey Mungai wametoa zawadi ya Krismass na mwaka mpya kwa watoto yatima 35 wa kituo cha Daily Bread life childreans home (DBL)cha mkimbizi katika Manispaa ya Iringa kama njia ya kuhamasisha jamii kuendelea kusaidia watoto yatima mkoani Iringa.
 
DSCF5036.JPG


Ngoma ya mganda ni ngoma ambayo inahitaji si mradi kucheza, mafunzo na mazoezi maalumu na wenye wepesi ndio wanaoweza. Niliona mara kadhaa nikaishiwa uwezo wa kuigiza maana wakipeleka mguu kushoto mie napeleka mbele, na wakipeperusha mkia wa mnyama mie napepezursha basi basi nikakoma ubishi, maana bila zoezi vigumu kuwafuatilia stp zao.
 
sijui mbunge ilkuaje Pale Sokoine Jmosi ktk tamasha wa kupata pesa za kusaidia walio athilika na mafuriko DSM
 
endelea na moyo huo huo mpaka 2015 lazima uwe mtu mashahuli kijijini kwako..
 
Jamani Deo tumpongeze wengine hata kuongea na wananchi hawawezi muda wote wapo Dar hasa kipindi hiki cha sikukuu big up DEO.
 
Jamani Deo tumpongeze wengine hata kuongea na wananchi hawawezi muda wote wapo Dar hasa kipindi hiki cha sikukuu big up DEO.

Wabunge wengi wanajikokota kuwa karibu na wananchi wakati uchaguzi unakaribia, kwa sasa wanakula bada tu mijini. Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
 
Wabarikiwe sana Deo na huyo Godfrey Mungai

Amen na tunatakiwa kuiga mifano yao, kwani enzi za kutegemea misaada kutoka ulaya imeshapitwa na wakati na wenyewe wameshashoshwa wanapoona waliobahatika kuwa na uwezo hapa kwatu wanawatia kisogoni maskini hawa na kile kidogo wanachotoa kinaishia mifukoni mwa wenye uwezo.
 
Back
Top Bottom