Makamu wa Rais azuru Kaburi la Magufuli akiwa njiani kuelekea Kibondo

Uzalendo wa Kitanzania

JF-Expert Member
Mar 8, 2020
2,191
4,656
IMG-20210514-WA0013.jpg


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Philip Mpango ametembeleaa kaburi la aliyekuwa Rais wa Tanzania Hayati Dkt John Magufuli.

Dkt Mpango alizuru kaburi hilo akiwa njiani kuelekea Wilayani Kibondo Mkoani Kigoma ili kufunga kampeni za Uchaguzi za CCM jimboni Muhambwe.

Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Muhambwe utakaofanyika Mei 26, 2021 unafuatia kifo cha aliyekuwa Mbunge wake Mheshimiwa Nditye.
 
View attachment 1784273hii sio heshima kabisa, Rais kabuli lake limezungushiwa mabati kama kibda cha kupaki gari, inamaana serikali haina hela kujenga vizuri hapo? familia nayo imeridhika?
Hapa wamebugi kabisa haifai kabisa hilo sio Godauni Kabuli lina Heshima yake Wajenge Nyumba nzuri kabisa Napinga kwa ngvu zangu zote Kuzungushia uzio kwa style hii
Rest In Peace JPM
 
Leo makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amezuru kaburi la Hayati JPM. Makamu wa Rais anaelekea Kibondo kwa ajili ya kufunga Kampeni kesho.

IMG_20210514_130534.jpg
 
Tena kama anatumia kodi zetu kufanya hizo ziara za kaburini ni ujinga. Si alikuwepo msibani? Sasa hizi naona ni kama sarakasi tu.
Kijana kuwa muelewa, ameshuka Chato kwa ndege anaunga Kibondo kuna ubaya kupita?
 
Back
Top Bottom