Uchaguzi 2020 Mgombea kupitia CHADEMA, Tundu Lissu achukua fomu za Kugombea Urais wa Tanzania ofisi za NEC Dodoma

PAZIA 3

JF-Expert Member
Jan 30, 2018
1,070
1,842
Kutoka maeneo mbalimbali kwenye viunga vya mji wa Dodoma, Tundu Lissu leo anachukua Fomu ya Urais.

===



Tundu Lissu leo kwa Mara ya kwanza anarejea katika mji wa Dodoma akienda kwa ajili ya kuchukua fomu ya kugombea Urais. Ikumbukwe Tundu Lissu mara ya mwisho kuondoka katika mkoa huu ni baada ya kupigwa risasi.

Fuatilia baadhi ya matukio na picha mbalimbali za tukio hilo.
IMG-20200808-WA0004.jpg
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA Tundu Lissu akiwa amewasili katika Ofisi za CHADEMA Kanda ya Kati zilizopo jijini Dodoma na kupokelewa na viongozi mbalinbali wa Chama, wanachama, wapenzi na mashabiki wa CHADEMA, kabla ya kuelekea Ofisi za Tume ya Uchaguzi kuchukua fomu, leo Jumamosi 08/08/2020.

====

TUNDU LISSU AFIKA OFISI ZA NEC KUCHUKUA FOMU YA UTEUZI

CE769421-FB5E-41A6-A92C-8D4BEEA96F94.jpeg

EBF0E13E-C02D-49C4-B855-8D8FF95B579B.jpeg

C7A71F48-F351-4588-BA22-5948B098731D.jpeg


Mgombea Urais Tanzania kupitia Chama cha CHADEMA, Tundu Lissu amefika katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuchukua fomu ya Uteuzi ya kugombea Urais

Lissu amefika katika Ofisi hizo na Mgombea Mwenza Salum Mwalim huku wakiwa wamesindikizwa na Wanachama wengine. Wamekabidhiwa fomu hizo na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji wa Rufaa (Mst), Semistocles Kaijage

Uchukuaji fomu za kugombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020 umeanza Agosti 5 hadi 25,2020.

Lissu amechukua fomu, wamezihakiki na kujiridhisha kisha wameondoka katika Ofis za NEC ili kuendelea na taratibu nyingine za kichama.

#JamiiForums #Siasa #JFSiasa #Uchaguzi2020
 
Kuna mtindo unaweza kutokea wa kuficha fomu moja kutoka katika begi la fomu ya urais, hakikisha mnakagua kila fomu iliyomo na msisain kitu ambacho hakimo.

Hii itawasaidia wakati wa kurejesha fomu hiyo, ikumbukwe kama kutakuwa na fomu ina-MISS, fomu yenu ya urais haitapokelewa na mtakuwa mmejiondoa katika kinyang'anyiro cha uraisi.

#TANZANIA YA WATANZANIA, VITU BAADAE!
 
Hivi kuna mtu mwenye akili timamu atampigia kura mgombea wa CCM?

CCM inawadanganya Watanzania kuwa ndani ya miaka 4-5 wamejenga viwanda 8477 , viwanda vingi kuliko vile vya Japan vilivyojengwa kwa miaka 100. Very stupid.
Ajira za kwenye miradi mikubwa tu ni zaidi ya milioni 6.

Utawapaje kura watu waongo, wanafiki na wazandiki kiasi hiki.

Ajira zingekuwa nyingi hivi nisingeona classmates wangu wengi wakilishwa na mama zao.
 
Hivi kuna mtu mwenye akili timamu atampigia kura mgombea wa CCM?
CCM inawadanganya Watanzania kuwa ndani ya miaka 4-5 wamejenga viwanda 8477 , viwanda vingi kuliko vile vya Japan vilivyojengwa kwa miaka 100. Very stupid.
Ajira za kwenye miradi mikubwa tu ni zaidi ya milioni 6.
Utawapaje kura watu waongo, wanafiki na wazandiki kiasi hiki.
Ajira zingekuwa nyingi hivi nisingeona classmates wangu wengi wakilishwa na mama zao.

Mkuu katika vitu Magufuli amefanikiwa ndani ya hii miaka mitano, ni kutengeneza wanafiki, waoga na wajinga wengi. Na yote haya ni kwasababu anajenga reli na bwawa la umeme.
 
Back
Top Bottom