Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,234
Inasema pia wataendelea na kesi yao waliyoifungua huko mambele dhidi ya TanzaniaMkuu, ukiisoma vizuri alicho kiandika Peter, utagundua amesema na akaweka wazi kwamba mazungumzo ya serikali ya Tanzania na Barrick bado yanaendelea.
Lakini kilicho onekana kumkwaza ni serikali ya Tanzania kuwataka ama kuwalazimisha wafanyakazi wa Accacia Dar office na North Mara kutoa maelezo kwa lazima, na akaongeza kuwa amesikitishwa kwa kitendo cha serikali ya Tanzania kuzima computer mbili pamoja na sim.
Hivyo amewataka wafanyakazi wa Accacia wawe watulivu katika kipindi hiki cha hofu kubwa.
Na akaongeza kwamba kwasasa Accacia imejikita hasa kwenye kulinda utu/usalama wa wafanyakazi wao. Na yeyote mwenye maswali ama maoni asisite kwenda kumuona ama kuzungumza na General Manager.