PICHA: Lema akiwa Jijini London akikagua chopa jipya la M4C

Hiyo chopper mbona kama mbovu?
Halafu jamaa ki fridge kinakuja fasta kinoma.
Akumbuke tu ametoka wapi na kina nani wamemtoa.
Kitambi kwa mwanaapollo hakikubaliki!!!!
 
CDM ni hodari kwa kupeana ULAJI kikanda, kwa nini kila penye harufu ya pesa awekwe mtu wa Kaskazini???? Lema kila siku yuko safarini na kufaidi RUZUKU!!

Ulitaka nani aende?Vikao vya Bunge wamuachie nani?Mbona hukushangaa JK kwenda kwenye
mkutano wa uzazi wa mpango?
 
Usikwepe hoja yako ya msingi Ritz,
Umesema Lema kapiga picha na Chopa kisha kawatumia wafuasi wake. Nikakuuliza ulitaka ampelekee Nape Nnaye na Mkama? Badala ya kujibu hoja unakuja Chopa imepigwa Rangi. Hoja ya Rangi itakuja baadaye, nakuuliza ulitaka ampelekee nani picha aliyopiga akiangalia Chopa?

Ingekuwa bora kama angezipeleka kwa wana familia yake.
 
MP Aweda,
Kwa nini msiyafanye haya kwa pesa zenu wenyewe wanachama wa vyama hivi? Kwa nini vyama vya SIASA vipewe RUZUKU inayotokana na kodi zetu ambazo baadhi yetu sio wanachama wa vyama hivi? Igeni mfano wa DINI zetu zinavyojiendesha kwa kutumia ZAKA na SADAKA za waumini wao. Huduma za jamii zinazidi kudorora kwa sababu ya kugharamia SIASA na wanaSIASA. Haohao tunaowagharamia bado wanatugharimu zaidi kwa ufisadi, rushwa, ubadhirifu,...
Hivi viwanja vya michezo kama CCM kirumba na Sheikh armi abeid Arusha unajua vimejengwa kwa kodi
ya nani?
 
tunataka mabadiliko yenye tija,hivo hatuwezi kuwatenga wa tz walio nje ya nchi, lema ni jembe,tunamkubali ni mtu makini asiyeogopa vitisho,ni mtu jasiri,ni mtu wa kuigwa kwa kujenga hoja makini, naamini kwa mnaopenda mabadiliko mtaniunga mkono,mtu makini hufanya vitu vilivyo makini. Big up godbles lema god bless u kama jina lako.

yaani kwa jinsi ninavyofuraishwa na utendaji kazi wake ktk chadema, imenibidi kwa kumuenzi nimembatiza mtoto wangu nikamwita godbless.

Nawashauri walio ccm wahamie chadema kungali mapema, maana mpaka 2015 ccm itakuwa haina watu.
 
CDM hayo ni matumizi mabaya ya ruzuku, badala ya kuimarisha ofisi zenu vijijini mnatumia mapesa mengi kununua chopa. Watanzania hawataki chopa , wao wanataka sera mbadala ambazo ni suluhisho la matatizo yao

huwezi kukaa
kwa office na kuongea ni lazima uwafikie watu na useme sera zako,kwa kuwa miundo mbinu ya usafiri ndio tatizo,ni vyema kutumia chopa ili kuwafikia wananchi na kuwapa elimu mbadala,maana kuna sehemu mpaka leo wanaelewa kuwa raisi ni nyerere hawa wanahitaji elimu zaidi na ili wafikiwe ni lazima chopa itumike
 
Hivi viwanja vya michezo kama CCM kirumba na Sheikh armi abeid Arusha unajua vimejengwa kwa kodi
ya nani?
Tunaitofautishaje CHADEMA na CCM endapo yale wanayofanya yanafanana? Kumbuka pia wakati viwanja hivi vinajengwa chama cha SIASA kilikuwa kimoja tu na hali ya huduma zetu za jamii haikuwa hivi ilivyo sasa.
 
MP Aweda,
Kwa nini msiyafanye haya kwa pesa zenu wenyewe wanachama wa vyama hivi? Kwa nini vyama vya SIASA vipewe RUZUKU inayotokana na kodi zetu ambazo baadhi yetu sio wanachama wa vyama hivi? Igeni mfano wa DINI zetu zinavyojiendesha kwa kutumia ZAKA na SADAKA za waumini wao. Huduma za jamii zinazidi kudorora kwa sababu ya kugharamia SIASA na wanaSIASA. Haohao tunaowagharamia bado wanatugharimu zaidi kwa ufisadi, rushwa, ubadhirifu,...

Una wazo zuri, lakini ni vyema ukakumbuka kuwa sheria ya ruzuku ilitungwa na bunge. CCM ndo inapata ruzuku kubwa kuliko chama chochote cha siasa hapa nchini na wanafaidi rasilimali nyingi zilizokuwa za wananchi enzi za chama kimoja. Ili kufanya siasa kwa mlingano, ni vizuri ruzuku ikaendelea kutolewa kwa vyama lakini ni vyema vyama hivyo vikakaguliwa matumizi ya fedha hizo.

CHADEMA wamejitahidi kutumia vizuri ruzuku katika kuwafikia wananchi wengi maeneo ya vijijini.
 
Hoja gani unataka wewe hiyo Chopa ipo kwenye chumba cha rangi nyie mnasema mpya sasa tusijadil unataka kuniziba mdomo..

Hiyo Chopa ndio Lema kapewa na Meya wa London.

Si afadhali yeye akipewa chopa la kufanyia kazi kuliko huyo dhaifu wenu aliyehongwa suti tano na mwarabu

Ingekuwa bora kama angezipeleka kwa wana familia yake.

Kaasheshe! Mkulu alipokuwa ana bembea kule wapi kule, aah Jamaica sijui, Picha zake tuliziona (sisi ambao si wana familia wake)? Naomba kukumbushwa!!
 
Una wazo zuri, lakini ni vyema ukakumbuka kuwa sheria ya ruzuku ilitungwa na bunge. CCM ndo inapata ruzuku kubwa kuliko chama chochote cha siasa hapa nchini na wanafaidi rasilimali nyingi zilizokuwa za wananchi enzi za chama kimoja. Ili kufanya siasa kwa mlingano, ni vizuri ruzuku ikaendelea kutolewa kwa vyama lakini ni vyema vyama hivyo vikakaguliwa matumizi ya fedha hizo.

CHADEMA wamejitahidi kutumia vizuri ruzuku katika kuwafikia wananchi wengi maeneo ya vijijini.
Najua CCM wanachota zaidi ya milioni 600; CHADEMA wanachota zaidi ya milioni 120; CUF zaidi milioni 100;..., kila mwezi! Ni haki?
 
Chama kinatakiwa kieleweke Nanjilinji kwa kuwa na ofisi na uongozi imara, nyie mnakazania kununua Chopa. Ruzuku ni kwa ajili ya kuimarisha chama siyo kumzawadia Lema eti kwa sababu mwatoka pahala pamoja. CDM ni genge la walaji HABARI YAKE MWISHO 2015
 
Hiyo Chopa ndio kapewa na Meya wa London?

Sio meya wewe!!

Hapa kwenu meya huwa kwa jina maarufu mnamwitaje eti??

Hili ni jambo dogo sana kwa M4C.......yapo mengi sana yanatarajiwa hasa kwa vilaza kama Magamba.

Mtaelewa tuu kadri siku zinvyosonga. leo Chopa kesho mnajua ni nini kinakuja??????????????

:A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1::A S-confused1:
 
CCM watakoma , mpaka ifike 2015, povu litakuwa limetoka lote na ndo kifo chao. Go go go CDM
 
Back
Top Bottom