Picha: Kukamatwa kwa maiti Morogoro na madawa ya kulevya

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,268
33,040
TASWIRA MZIMA YA TUKIO LA MAITI KUKUTWA NA KETE ZA MADAWA YA KULEVYA MOROGORO NDIYO HII.

DSC08462.JPG


Watuhumiwa waliokuwa na mwili wa marehemu Khalid Kitala katika kituo kikuu cha polisi Morogoro.
DSC08422.JPG


Watuhumiwa wakipanda gari la polisi tayari kwenda kituo kikuu cha polisi.
DSC08435.JPG

Kete zilitolewa katika gari baada ya kupekuliwa
DSC_0740.JPG

Hapa kuna kete aina mbili zinaonekana katika hii picha, za juu nyeupe sana ndizo zilitopatikana katika gari baada ya kupekuliwa na hizo za rangi kama njano kwa mbali ndizo zilitotolewa katika tumbo la marehemu baada ya kupasuliwa.

DSC08427.JPG

Huyo ni Dk Lyamuya ambaye aliwapiga chenga waandishi wakati wakimtaka kueleza alichoona wakati wa uchunguzi wa maiti aliyepasuliwa tumbo ili kuweza kubaini kama ni kweli maiti ilikuwa na kete zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya lakini baadaye aliongea nao
DSC08428.JPG


DSC08437.JPG

Hati za kusafirisia, hiyo ya njano ni ile iliyokuwa ikitumiwa na marehemu Khalid.
DSC08440.JPG

Huyo ndiye anayedaiwa kuwa ndiye ndugu wa marehemu, hizo ni karoti wakati wa zoezi la upekuaji.
DSC08446.JPG

Mmoja wa makachero wa jeshi la polisi akipekua hadi katika injini ya gari.

DSC08467.JPG

Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Morogoro akiongea na waandishi mara baada ya kumalizika kwa kazi ya uchunguzi huku waandishi wakimtaka kutoa taarifa juu ya tukio hilo ofisini kwake mtaa wa Kitope.
 
Duh kazi ipo watu hadi wanadiriki kubebesha maiti madawa ya kulevya? Kweli dunia kwishney! Lakini mimi nataka kuuliza kidogo mnifafanulie hili swala linanitatiza sasa huyu marehemu alimeza haya madawa akiwa hai then akafariki baadae au hawa jamaa waliichukua maiti wakaisokomezea madawa? Manake nina maswali mia mbili kasoro na jibu ni moja!
 
Mkuu, ulivyosema taswira, i expected a graphic thread, lakini sijaona hilo zaidi ya tupicha tutatu tu

Haya shukran
 
Je ni sahihi polisi kuonesha sura za watuhumiwa? Ona polisi wa Macau walivyotreat yule binti. Polisi kuweni profesional kidogo hii unaweza kuwa sababu ya watuhumiwa kuachiwa na mahakama, halafu mnalalamika hoo wanaachiwa wakati ninyi wenyewe hamfanyi kazi kwa weledi

Kwa nini isiwe si sahihi?

Ona hawa punda wa Kiingereza waliokamatwa huko Peru miezi michache iliyopita.



Hata huko Atlanta, USA nako huwa wanaonyeshwa nyuso zao.

 
Last edited by a moderator:
Mungu atusaidie kutuonesha fursa zingine za biashara ili wenzetu waiepuke biashara hii haramu
 
Je ni sahihi polisi kuonesha sura za watuhumiwa? Ona polisi wa Macau walivyotreat yule binti. Polisi kuweni profesional kidogo hii unaweza kuwa sababu ya watuhumiwa kuachiwa na mahakama, halafu mnalalamika hoo wanaachiwa wakati ninyi wenyewe hamfanyi kazi kwa weledi

hutaki sura zikaonekana eh..,hata wewe siku ukivunja sheria watakuonyesha tu......tulia uone...unataka wafichwe ili wakitoka waendelee!??
 
Mie maelezo ya huyo Dk ndio yaliniacha hoi hivi alikuwa najua what she was talking.............

Mwingine juzi juzi kafariki baada ya kete kupasukia tumboni..mwingine tena huyu hapa
 
Hii nchi imekuwa kama ya kimafia na uhuni umekubuhu na huenda ni kweli watawala wanafanya hii biashara kama Kapuya alivyonukuliwa kuwa watoto wao wanauza sembe la Pakistan na Brazil na hakuna wa kuwakamata kwani wao ndio wenye nchi hii!!

Kikwete na utawala wako wakin!a Said Mwema inabidi mbebe hizi lawama ikiwa raisi alishasemaga wauza unga anawajua na ana majina yao halafu yupo kimya na akijikiweka busy na route kama shirika la ndege la kimataifa!!
 
Yani dr anaogopa kuongelea jambo hilo, ni ka vile anaweka shingo yake rehani mbele ya wahusika wasioshitakika bongo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom