Picha: Kukamatwa kwa maiti Morogoro na madawa ya kulevya

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,305
2,000
TASWIRA MZIMA YA TUKIO LA MAITI KUKUTWA NA KETE ZA MADAWA YA KULEVYA MOROGORO NDIYO HII.Watuhumiwa waliokuwa na mwili wa marehemu Khalid Kitala katika kituo kikuu cha polisi Morogoro.


Watuhumiwa wakipanda gari la polisi tayari kwenda kituo kikuu cha polisi.

Kete zilitolewa katika gari baada ya kupekuliwa

Hapa kuna kete aina mbili zinaonekana katika hii picha, za juu nyeupe sana ndizo zilitopatikana katika gari baada ya kupekuliwa na hizo za rangi kama njano kwa mbali ndizo zilitotolewa katika tumbo la marehemu baada ya kupasuliwa.


Huyo ni Dk Lyamuya ambaye aliwapiga chenga waandishi wakati wakimtaka kueleza alichoona wakati wa uchunguzi wa maiti aliyepasuliwa tumbo ili kuweza kubaini kama ni kweli maiti ilikuwa na kete zinazodaiwa kuwa ni madawa ya kulevya lakini baadaye aliongea naoHati za kusafirisia, hiyo ya njano ni ile iliyokuwa ikitumiwa na marehemu Khalid.

Huyo ndiye anayedaiwa kuwa ndiye ndugu wa marehemu, hizo ni karoti wakati wa zoezi la upekuaji.

Mmoja wa makachero wa jeshi la polisi akipekua hadi katika injini ya gari.


Mkuu wa Upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Morogoro akiongea na waandishi mara baada ya kumalizika kwa kazi ya uchunguzi huku waandishi wakimtaka kutoa taarifa juu ya tukio hilo ofisini kwake mtaa wa Kitope.
 

Shokolokobangoshey

JF-Expert Member
Apr 5, 2013
311
0
Duh kazi ipo watu hadi wanadiriki kubebesha maiti madawa ya kulevya? Kweli dunia kwishney! Lakini mimi nataka kuuliza kidogo mnifafanulie hili swala linanitatiza sasa huyu marehemu alimeza haya madawa akiwa hai then akafariki baadae au hawa jamaa waliichukua maiti wakaisokomezea madawa? Manake nina maswali mia mbili kasoro na jibu ni moja!
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
21,997
2,000
Mkuu, ulivyosema taswira, i expected a graphic thread, lakini sijaona hilo zaidi ya tupicha tutatu tu

Haya shukran
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
87,597
2,000
Je ni sahihi polisi kuonesha sura za watuhumiwa? Ona polisi wa Macau walivyotreat yule binti. Polisi kuweni profesional kidogo hii unaweza kuwa sababu ya watuhumiwa kuachiwa na mahakama, halafu mnalalamika hoo wanaachiwa wakati ninyi wenyewe hamfanyi kazi kwa weledi

Kwa nini isiwe si sahihi?

Ona hawa punda wa Kiingereza waliokamatwa huko Peru miezi michache iliyopita.


Hata huko Atlanta, USA nako huwa wanaonyeshwa nyuso zao.

 
Last edited by a moderator:

ssafari

Senior Member
Jul 17, 2013
177
225
Mungu atusaidie kutuonesha fursa zingine za biashara ili wenzetu waiepuke biashara hii haramu
 

Baba Matatizo

JF-Expert Member
May 5, 2011
334
195
Je ni sahihi polisi kuonesha sura za watuhumiwa? Ona polisi wa Macau walivyotreat yule binti. Polisi kuweni profesional kidogo hii unaweza kuwa sababu ya watuhumiwa kuachiwa na mahakama, halafu mnalalamika hoo wanaachiwa wakati ninyi wenyewe hamfanyi kazi kwa weledi

hutaki sura zikaonekana eh..,hata wewe siku ukivunja sheria watakuonyesha tu......tulia uone...unataka wafichwe ili wakitoka waendelee!??
 

Heaven on Earth

JF-Expert Member
Mar 21, 2013
37,139
2,000
Mie maelezo ya huyo Dk ndio yaliniacha hoi hivi alikuwa najua what she was talking.............

Mwingine juzi juzi kafariki baada ya kete kupasukia tumboni..mwingine tena huyu hapa
 

Abdillahjr

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
694
0
Hii nchi imekuwa kama ya kimafia na uhuni umekubuhu na huenda ni kweli watawala wanafanya hii biashara kama Kapuya alivyonukuliwa kuwa watoto wao wanauza sembe la Pakistan na Brazil na hakuna wa kuwakamata kwani wao ndio wenye nchi hii!!

Kikwete na utawala wako wakin!a Said Mwema inabidi mbebe hizi lawama ikiwa raisi alishasemaga wauza unga anawajua na ana majina yao halafu yupo kimya na akijikiweka busy na route kama shirika la ndege la kimataifa!!
 

KakaJambazi

JF-Expert Member
Jun 5, 2009
17,834
2,000
Yani dr anaogopa kuongelea jambo hilo, ni ka vile anaweka shingo yake rehani mbele ya wahusika wasioshitakika bongo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom